CCM Taifa ya JK ilivyoisambaratisha CCM Mbeya ili tu kumkabili Prof Mark Mwandosya.

Kuna uzi una trend kwa nini Magufuli hajawahi kwenda Mbeya.

Lakini matukio ya Mbeya yana historia ambayo lazima ielezwe.

Kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2005 haukuuacha mkoa wa Mbeya salama.

Prof Mark Mwandosya alionekana kuwa tishio.
Lakini mwisho wa siku Jakaya Kikwete akashinda urais.

Prof Mwandosya alikuwa na nguvu mkoani Mbeya na alikuwa anapendwa na amewaunganisha vikundi na makabila yote mkoani.
Kichama alikuwa mjumbe wa NEC vile vile.

Nguvu ya Mwandosya ilibidi JK aidhibiti kwa kutumia mtandao wake ambao ndio ulifanikisha kumpeleka Ikulu.

Mwandosya alikuwa na nguvu kiasi kwamba Lowasa, akiwa Waziri Mkuu alipotembelea mkoani Mbeya, wananchi walianza kumwimbia "..raisi...raisi...raisi.."
mbele ya Lowasa.

Ndani ya CCM Mbeya mara yakaanza kuibuka makundi hasimu.
Mwenyekiti wa CCM Mbeya akachaguliwa mfanya biashara mwenye historia ya kutia mashaka na aliye na historia ya ujangili.

Mwandosya aliyezunguka nchi nzima kuomba kura za kupendekezwa, akaanza kuugua ugonjwa ambao mpaka leo haufahamiki.

Timu ya mtandao ya JK ilifanya himework yake vizuri

Mwishoni hata nafasi ya uNEC ya Mwandosya ilitikiswa maana mkuu wa Usalama wa Taifa alipewa jukumu la kumpenyeza mtoto wake Thomas Mwang'onda ili achukue kiti hicho.
Thomas hakufanikiwa, lakini mitikisiko yote ilianza kukidhoofisha sana chama CCM Mbeya.

CCM Taifa ilihusika moja kwa moja na mitikisikonhiyo, ambayo hata dola ilikuwa nyuma yake.

Chini ya Mwenyekiti wa CCM Mbeya aliyekuwapo watu waligawanywa kiukabila na mizengwe mingi.
Mkuu wa mkoa aliyekuwa mwana mtandao alihakikisha base ya Mwandosya ina tikiswa.

Lakini kwa upande wa pili JK na mtandao hawakuliona tatizo kubwa zaidi la vijana kuanza kuihama kabisa CCM.
Na star wao Mwandosya alipopigishwa magoti, siyo siri wakahamia kwa star wa mipasho, Sugu na CHADEMA yake.

Hayo ndo matokeo ya mtandao kuisambaratisha CCM Mbeya.

Mpaka leo hakuna juhudi mahsusi zilizofanywa na CCM Taifa kuondoa mikanganyiko, chuki na ufarakano uliopandikizwa.

Mwaka jana Katibu Mwenezi Polepole kaenda Mbeya.
Bila kujijua hakuusoma mchezo, yeye akaona tu hiyo chuki, mifarakani, ukabila bila kujua chanzo chake.

Ni wakati muafaka sasa Mwenyekiti wa CCM amteue J Kikwete, yeye aliyepanda mbegu zile mbaya mkoani Mbeya, atumike sasa kung'oa magugu aliyopanda ili kuleta umoja Mbeya.
JK na Mwandosya wametoka mbali.

Magufuli karithi mgogoro ambao kwa kweli hahusiki nao, lakini wananchi wengi hasa wazee, wako nyuma ya CCM.
Kinyang'anyiro cha urais hakijauacha mkoa wa Mbeya salama kimaendeleo.
Watu wa Mbeya ni kama wa Tarime, Arusha na Kilimanjaro, CCM ilitengeneza watu wasio na ushawishi ili wamtikise Mwandosya, nakumbuka Kisa cha Mpesya kudondoshwa na Sugu, Zambi nae kule Songwe akadondoshwa, Kule Momba pia. Wanambeya hawataki viongozi wanaopewa kura hafu wanaenda kuishi Dar, viongozi wanaowabagua wenzao kwa misingi ya Elimu, ukabila nk.
Mpesya analitambua hili lilimgharimu katika uchaguzi wa 2010. Katika hii mikoa ya Mbeya na Songwe wilaya ambazo CCM itashinda kiurahisi ni Chunya na Ileje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi tatizo langu ni pale vyama vya upinzani vilipopewa "lifti" na CCM Taifa wakati wa JK kwa kuibomoa CCM Mbeya.
Leo umoja ndani ya CCM Mbeya bado hauja tengemaa kitu ambacho kinaitesa CCM kiujumla.
 
Mwenyekiti wa CCM Mbeya bado ni yule boss wa Rujewa na Usangu?
 
Nashukuru umevitaja vyeo vyote akivyopewa Prof Mwandosya na Rais Jakaya Kikwete.

Mtu katumiwa mamluki wa kumuua kisiasa through mtoto wa aliyekuwa mkuu wa Usalama wa Taifa, nd Apson.

Hivi kwa akili yako hapo ulitegemea nini kama Thomas angeshinda?

Hata hivyo pamoja na Prof ku win the battle ya uNEC, he lost the war!

Kikwete alim mesmerise Prof kwa vyeo huku akijua kuwa amemmaliza kisiasa, he was no longer a threat.
Kumbuka tofauti zao zilianzia wizara ya Maji, Madini na Nishati.

Kiongozi na wewe unaamini kua baada ya Jk kua raisi Mwandosya alikua threat kwake? Yaani waziri anaeteuliwa na raisi awe threat kwa raisi na mwenyekiti wa chama wakati utaratibu wa miaka mihula miwili unajulikana? Yaani mtu akushinde akiwa waziri halafu uje umshinde akiwa raisi na mwenyekiti wa chama? Hicho kitu hakiwezi kutokea ndani ya CCM ninayoifahamu mimi.
 
Kuna uzi una trend kwa nini Magufuli hajawahi kwenda Mbeya.

Lakini matukio ya Mbeya yana historia ambayo lazima ielezwe.

Kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2005 haukuuacha mkoa wa Mbeya salama.

Prof Mark Mwandosya alionekana kuwa tishio.
Lakini mwisho wa siku Jakaya Kikwete akashinda urais.

Prof Mwandosya alikuwa na nguvu mkoani Mbeya na alikuwa anapendwa na amewaunganisha vikundi na makabila yote mkoani.
Kichama alikuwa mjumbe wa NEC vile vile.

Nguvu ya Mwandosya ilibidi JK aidhibiti kwa kutumia mtandao wake ambao ndio ulifanikisha kumpeleka Ikulu.

Mwandosya alikuwa na nguvu kiasi kwamba Lowasa, akiwa Waziri Mkuu alipotembelea mkoani Mbeya, wananchi walianza kumwimbia "..raisi...raisi...raisi.."
mbele ya Lowasa.

Ndani ya CCM Mbeya mara yakaanza kuibuka makundi hasimu.
Mwenyekiti wa CCM Mbeya akachaguliwa mfanya biashara mwenye historia ya kutia mashaka na aliye na historia ya ujangili.

Mwandosya aliyezunguka nchi nzima kuomba kura za kupendekezwa, akaanza kuugua ugonjwa ambao mpaka leo haufahamiki.

Timu ya mtandao ya JK ilifanya himework yake vizuri

Mwishoni hata nafasi ya uNEC ya Mwandosya ilitikiswa maana mkuu wa Usalama wa Taifa alipewa jukumu la kumpenyeza mtoto wake Thomas Mwang'onda ili achukue kiti hicho.
Thomas hakufanikiwa, lakini mitikisiko yote ilianza kukidhoofisha sana chama CCM Mbeya.

CCM Taifa ilihusika moja kwa moja na mitikisikonhiyo, ambayo hata dola ilikuwa nyuma yake.

Chini ya Mwenyekiti wa CCM Mbeya aliyekuwapo watu waligawanywa kiukabila na mizengwe mingi.
Mkuu wa mkoa aliyekuwa mwana mtandao alihakikisha base ya Mwandosya ina tikiswa.

Lakini kwa upande wa pili JK na mtandao hawakuliona tatizo kubwa zaidi la vijana kuanza kuihama kabisa CCM.
Na star wao Mwandosya alipopigishwa magoti, siyo siri wakahamia kwa star wa mipasho, Sugu na CHADEMA yake.

Hayo ndo matokeo ya mtandao kuisambaratisha CCM Mbeya.

Mpaka leo hakuna juhudi mahsusi zilizofanywa na CCM Taifa kuondoa mikanganyiko, chuki na ufarakano uliopandikizwa.

Mwaka jana Katibu Mwenezi Polepole kaenda Mbeya.
Bila kujijua hakuusoma mchezo, yeye akaona tu hiyo chuki, mifarakani, ukabila bila kujua chanzo chake.

Ni wakati muafaka sasa Mwenyekiti wa CCM amteue J Kikwete, yeye aliyepanda mbegu zile mbaya mkoani Mbeya, atumike sasa kung'oa magugu aliyopanda ili kuleta umoja Mbeya.
JK na Mwandosya wametoka mbali.

Magufuli karithi mgogoro ambao kwa kweli hahusiki nao, lakini wananchi wengi hasa wazee, wako nyuma ya CCM.
Kinyang'anyiro cha urais hakijauacha mkoa wa Mbeya salama kimaendeleo.
Ni kweli Mwandosya alikuwa na nguvu mkoani Mbeya, lakini kwa siasa za nchi ungewezaje kuishika nchi kwa umaarufu wa mkoa mmoja? Hiyo ilikuwa ni miscalculation ya Mwandosya. Pia kuna jambo muhimu ambalo unakwepa kulisema. Mwandosya alikuja na ajenda ya 'safari hii ni kanda ya nyanda za juu kusini' kwa ujumla aliingia kikabila zaidi ya taifa. Alihangaika sana kuingiza mkoa wa Iringa (iringa+Njombe) lakini walikwisha stuka juu ya lengo lake.

Kwa ujumla Mwandosya hakuwa bora kiasi hicho na unaweza ukathibisha kwa udhaifu wa hotuba yake ya fainali ambao ni kama alikuwa anazungumza na familia badala ya wajumbe wa kitaifa wa CCM. Akiwa waziri pia kuna madhaifu kibao alionyesha ambayo hayakumpa sifa ya kiongozi wa kitaifa. Alijivunia usomi wake wa darsani bila kuangalia nyuma kama kweli yeye ni maarufu. Ukishangiliwa Mbeya, siyo lazima Iringa wakupe hi!

Ubaya wa JK, alidekeza uadui wa miaka nenda rudi. Typical of a village witch behaviour. Yaani kweli unapambana na adui kwa suicide ili mfe wote? Kama ni hivyo, wote Mbeya walikufa na tuliona JK akipopolewa na mawe.
 
Mwenyekiti wa CCM Mbeya bado ni yule boss wa Rujewa na Usangu?
Mkuu ili kutekeleza kuivuruga CCM Mbeya, "alichaguliwa" mwenyekiti wa mkoa ambaye si tu alikuwa na historia ya ujangili, lakini aliwahi kamatwa na meno ya tembo huko Iringa.
Kesi iliisha kimagumashi.
Majuzi aliwekwa ndani kwa matatizo ya umiliki wa kiwanda cha chai huko Tanga.

Thats how low CCM stooped.

Watu wenye heshima zao wakajiweka mbali na kadia hizi.

Leo hapo juzi kati, Pole pole ameenda Mbeya, kakuta kivuli tu cha CCM.
 
Ni kweli Mwandosya alikuwa na nguvu mkoani Mbeya, lakini kwa siasa za nchi ungewezaje kuishika nchi kwa umaarufu wa mkoa mmoja? Hiyo ilikuwa ni miscalculation ya Mwandosya. Pia kuna jambo muhimu ambalo unakwepa kulisema. Mwandosya alikuja na ajenda ya 'safari hii ni kanda ya nyanda za juu kusini' kwa ujumla aliingia kikabila zaidi ya taifa. Alihangaika sana kuingiza mkoa wa Iringa (iringa+Njombe) lakini walikwisha stuka juu ya lengo lake.

Kwa ujumla Mwandosya hakuwa bora kiasi hicho na unaweza ukathibisha kwa udhaifu wa hotuba yake ya fainali ambao ni kama alikuwa anazungumza na familia badala ya wajumbe wa kitaifa wa CCM. Akiwa waziri pia kuna madhaifu kibao alionyesha ambayo hayakumpa sifa ya kiongozi wa kitaifa. Alijivunia usomi wake wa darsani bila kuangalia nyuma kama kweli yeye ni maarufu. Ukishangiliwa Mbeya, siyo lazima Iringa wakupe hi!

Ubaya wa JK, alidekeza uadui wa miaka nenda rudi. Typical of a village witch behaviour. Yaani kweli unapambana na adui kwa suicide ili mfe wote? Kama ni hivyo, wote Mbeya walikufa na tuliona JK akipopolewa na mawe.
Mkuu kiukweli si kwamba Mwandosya alikuwa the best.
Argument mada hii ni kukisambaratisha chama CCM ili kumbomoa Mwandosya.
Thats a political crime.

Leo vijana wengi wamekimbilia kwa mpiga vijembe na mipasho, Sugu.

Tuna lament kwa vile CCM Taifa ya JK imetufikisha hapo.
 
Uko sawa! Ndo maana nikasema JK alidekeza sana uadui na bahati mbaya marafiki aliwapa kichwa hata wasio na uwezo. Mwandosya na JK walikaa wizara moja, nadhani wote walikuwa wapenda mikogo, bahati mbaya mmoja akatangulia mbele.

Kama ni kweli JK aliigawa Mbeya, Mwandosya naye aliigawa Mbeya. Alijionyesha kwamba ktk wabunge wote wa Mbeya yeye ni bora kuliko wengine. Hili alilionyesha miaka yote. Sijui nani alimpa kichwa hicho lakini nadhani kwa kuwa aliachwa akawa waziri muda wote. Akavimba kichwa kwamba wengine wako nyuma yake. Hapo ndo hiyo dhana ya rais wa Mbeya ilipotoka kama masopakyindi anavyoandika.
 
Kuna watu mnaishi kwa hisia Sana

Mh. Mark Mwandosya alikuwa mmoja wa watu waluotumiwa Sana Mh. Kikwete Kwenye Mbio Za Urais 2005

Kuna Mengi ya kuandika lakin kuna watu tutakuwa tumewaanika Na si vizuri ku expose Siri Za watu bila ya sababu Za msingi but let me share with you some hints

1) Meneja wa Mark Mwandosya Kwenye Mbio Za Urais 2005 ndie aliekuja kumsambaratisha Lowassa 2007 Huyu Mtu anaitwa Dr Harrison Mwakyembe

2) Dakika Za majeruhi Za uchaguzi wa Mgombea Urais ngazi ya Chama uliofanya ka May 4, 2005 aliesaidia kutibua mbinu Chafu Za KAMBI ya Fredrick Sumaye iliyohamia kwa Dr Salim alietaka kuunganisha Makundi yote yawe upande wa Salim dhidi ya Jakaya alikuwa Ni Mzee Mwandsya Na kwa Hilo alisadia Sana Sana Na ndio maana Jakaya hakumuacha kipind chote Hata Cha ugonjwa akiwa Nyumbani Na matibabuni aliamua kumpa Uwaziri wa Wizara isiyo Na majukumu ( Ihsaan)

Mark Mwandosya alikuwa Mtu wa Karibu wa Jakaya Na Msiri wake wa Miaka yote

Kwenye Siasa kuna watu wanaweza kujitokeza kugombea Na Wewe nafasi Moja ila lengo Lao Ni kukusaida Na mbinu hiyo hufanywa Sana Pemba kusaidia Wagombea wa CUF

Naandika na kufuta kwa Kuwa Mengine hayaandikiki kwa Kuwa yataharibu uhusiano wa watu ambao mpaka leo wanaheshimiana Sana!

Mzee Mkapa alikuwa Songea Kwenye May Mosi ya 2005 Na Siku nne Baadae akawa anakuja Dodoma kusimamia Uchaguzi wa Mgombea Urais ndani ya Chama

Yaliyotokea ndani ya Siku hizi nne unaweza ukajaza kitabu lakin ndio imebaki Historia ila Fredrick Sumaye na Jakaya Ni Chui Na Paka Kuliko Jakaya Na Lowassa japo wengi hawatambui

Baada ya Jakaya Kuwa Rais ilibidi Sumaye 'akimbie' kwenda kusoma Marekani ili kucheki kasi ya Jakaya Kumbe Jakaya hakuwa Na time ya kulipiza Visasi vya kijinga Na Baada ya kuona Upepo umetulia akirudi kimya kimya

Mzee Mwandosya kilichomuathiri Kisaikolojia ni ile kuitwa Jumba jeupe June 2015 Na kuambiwa 'kachukue form Mengine niachie Mie ' Kumbe hiyo Kauli waliambiwa wengi akiwemo Mzee wetu Mzee Augustine Ramadhan.

Wahuni sio watu wazuri kabisa Na usijaribu kuingia Miadi Na wahuni
Mkuu hebu fungua thread kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnajielewa au siyo ?

Kujielewa kwenu mnaishia kukaa nyumba za matope, kupanda mabasi ya Rungwe Express na Majinja.
Mkipata ajali mnakufa kama mbuzi wa kafara!

Kiwanja cha ndege Songwe , ndege mwazisikia tu.

Mkifika Dsm mnafikia Keko na Mbagala, ndo zenu.
Masikini kimawazo nyie, halafu mwasema mnajielewa.

Safirini Mwanza na Arusha muelewe vijana wenzenu wanafanya nini.
Mkuu hapo umeua vijana wa Sugu.
 
Back
Top Bottom