CCM sio tuu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sio tuu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Aug 19, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  Salaam wana jamvi,
  Nimesoma maazimio ya kikao cha NEC ya Chama cha Mapinduzi, yameniacha na maswali bila majibu.
  Kuna uwezekano kuwa CCM sio tuu ni chama tawala, bali pia ni chama dola?
  Hivi kweli CCM kama chama kina uwezo wa kuhoji spika wa legistlature jinsi anavyoliendesha bunge?.
  Kimeunda kamati ya wenye busara kufuatilia uendeshaji wa bunge!.
  Madudu yote ya the executive CCM haijayaona wala kuyahoji kwa vile mkuu wa executive ni mwenyekiti wa CCM hivyo CCM ni excutive party kinachodhibiti bunge na kudhibiti juditiary kunafuatia!
  jee tunarudi tena kwenye party supremacy?
  Swali ni jee CCM chama Dola?.
  CCM na Bunge nani zaidi!
  Naomba kuwasisha.
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sioni cha kujadili hapo.
  Wafu wanaendesha Misa ya kumzika mfu mwenzao, sisi tulio hai tufanye nini??

  "Uimara wa kammba imara ni Imara sawsawa kabisa na pale penye ubovu na udhaifu mkuu"

  CCM hawawezi kujiokoa wao kama CCM kwa kujitoa kafara mikia yao, masikio yao,makalio yao au tupu zao, damu na uhai wao unaitwa dhidi ya uovu ulozidi haki.

  Wakimla Mzee Six mzimamzima wajue mwingine kati yao zamu yake itawadia.
   
Loading...