unprejudiced
JF-Expert Member
- Jan 27, 2017
- 3,506
- 2,862
Kati ya wajumbe wote wa kamati kuu ni watu watatu tu pamoja na msemaji wao ndiyo waliounga mkono Membe kufukuzwa. Hata aliyeongoza Tume ya Maadili, yaani Mzee Philip Mangula alipinga Membe kuvuliwa uanachama wa chama hicho, imedokezwa.
Wajumbe wengi walipendekeza Benard Membe kufungiwa kufanya siasa ndani ya chama hicho kwa muda maalum kama adhabu mbadala ili kuepuka kukigawa chama.
Adhabu kama hiyo ndiyo alipewa Kinana ambaye hata hivyo haiwezi kumuathiri kwa lolote lile kwani alishaachana na mambo ya siasa. Adhabu hiyo mbadala ilipingwa kwa nguvu zote na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Bashiru Ally ambaye alisimamia Membe na Kinana kufukuzwa.
Taarifa zilizovuja ndani ya kamati hiyo zinadai kuwa wajumbe wa kikao hicho waliondoka bila ya kupata muafaka wa pamoja huku wababe wanne ambao walisimamia Membe kufukuzwa wakitoka na maamuzi yao.
My take: Upo uwezekano kuwa ndani ya CCM kuna mgogoro unaoendelea licha ya wachache kutuaminisha kuwa wanachama wake ni wamoja. Tusubiri tuone watakaoanza kuunga mkono msimamo wa Membe wazi wazi.
Wazee wa kale hawajawahi kukosea. Ukiona. Mke wa jirani anafuatilia sana ya ndani mwenu ujue HATOSHEKI aliko. So tell us mkuu. Shida yako hasa nini. Tufanye yote hayo kweli. Wewe unahitaji Nini. Mana kama Ni mpinzani wa hicho chama. Bado haitakusaidia.
Sent using Jamii Forums mobile app