Tetesi: CCM si wamoja, hamna siri. Kumbe kamati kuu yenu iligawanyika pakubwa kuhusu sakata la kufukuzwa Membe?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Kati ya wajumbe wote wa kamati kuu ni watu watatu tu pamoja na msemaji wao ndiyo waliounga mkono Membe kufukuzwa. Hata aliyeongoza Tume ya Maadili, yaani Mzee Philip Mangula alipinga Membe kuvuliwa uanachama wa chama hicho, imedokezwa.

Wajumbe wengi walipendekeza Benard Membe kufungiwa kufanya siasa ndani ya chama hicho kwa muda maalum kama adhabu mbadala ili kuepuka kukigawa chama.

Adhabu kama hiyo ndiyo alipewa Kinana ambaye hata hivyo haiwezi kumuathiri kwa lolote lile kwani alishaachana na mambo ya siasa. Adhabu hiyo mbadala ilipingwa kwa nguvu zote na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Bashiru Ally ambaye alisimamia Membe na Kinana kufukuzwa.

Taarifa zilizovuja ndani ya kamati hiyo zinadai kuwa wajumbe wa kikao hicho waliondoka bila ya kupata muafaka wa pamoja huku wababe wanne ambao walisimamia Membe kufukuzwa wakitoka na maamuzi yao.

My take: Upo uwezekano kuwa ndani ya CCM kuna mgogoro unaoendelea licha ya wachache kutuaminisha kuwa wanachama wake ni wamoja. Tusubiri tuone watakaoanza kuunga mkono msimamo wa Membe wazi wazi.
 
Bwana miwani anapiga penati!
Screenshot_20200301-091022-picsay.jpeg
 
Bashiru anatumika na jiwe kusimika udikteta ndani ya chama. Bashiru ipo siku atajuta anayoyafanya ndani ya chama.

Ni aibu kwa mhadhiri aliyewahi kuheshimika siku za nyuma. Anaaibisha taaluma yake na anajiwekea alama ya kudumu atakayokufa nayo kwa majuto. Lakini majuto ni mjukuu. Pole sana kadikteta kabashiru.
 
Hapo ndo huwa naona CCM ina intelejensia ya hali ya juu. Kumwacha Membe ilikuwa hatari zaidi. Huenda Membe mwenyewe alitegemea angefungiwa ila hii ya kumfukuza ni kama imemshtua. Ndo maana kajikuta anaropoka vitu nje vya taaluma yake.
 
Kati ya wajumbe wote wa kamati kuu ni watu watatu tu pamoja na msemaji wao ndiyo waliounga mkono Membe kufukuzwa. Hata aliyeongoza Tume ya Maadili, yaani Mzee Philip Mangula alipinga Membe kuvuliwa uanachama wa chama hicho, imedokezwa.

Wajumbe wengi walipendekeza Benard Membe kufungiwa kufanya siasa ndani ya chama hicho kwa muda maalum kama adhabu mbadala ili kuepuka kukigawa chama.

Adhabu kama hiyo ndiyo alipewa Kinana ambaye hata hivyo haiwezi kumuathiri kwa lolote lile kwani alishaachana na mambo ya siasa. Adhabu hiyo mbadala ilipingwa kwa nguvu zote na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Bashiru Ally ambaye alisimamia Membe na Kinana kufukuzwa.

Taarifa zilizovuja ndani ya kamati hiyo zinadai kuwa wajumbe wa kikao hicho waliondoka bila ya kupata muafaka wa pamoja huku wababe wanne ambao walisimamia Membe kufukuzwa wakitoka na maamuzi yao.

My take: Upo uwezekano kuwa ndani ya CCM kuna mgogoro unaoendelea licha ya wachache kutuaminisha kuwa wanachama wake ni wamoja. Tusubiri tuone watakaoanza kuunga mkono msimamo wa Membe wazi wazi.
2010 Shibuda alifukuzwa mbona maneno hayo hayakuwepo au yeye hakuwa binadamu?
 
Ayo anayoyafanya Bashiru msimlaum ni maagizo ya Magufuli na hata yeye mwenyewe na Polepole hawakubaliani na kufukuzwa kwa Membe Ccm.
Hata wewe ungekuwa Magufuli usingetoka nje ya hicho maana ana taarifa nyingi kuhusu hilo jambo kuliko mwingine yeyote huenda hata kuliko Membe mwenyewe
 
48 Reactions
Reply
Back
Top Bottom