CCM sawa na handaki la uchafu, ukitoka jiangalie kwenye kioo cha CHADEMA.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Mkiwa ndani ya shimo la uchafu lenye giza nene wote mtaonekana wachafu, kama ni harufu wote mtanuka, kama ni uchafu wote mtauzoea hakuna mtu wa kumcheka mwenzake, ila siku mmoja wao atakapotoka nje ya shimo kwenye mwanga ndipo wenzake watapouona uchafu wake wataanza kumcheka bila kujua wao pia ni wachafu, ndivyo Chama cha Mapinduzi CCM kilivyo.

CHADEMA kimekuwa kama kioo cha kujitizama na kujipima kwa kila mwanaCCM atokapo shimoni kama ni msafi ama mchafu.

Ndani ya CCM kuna kila aina ya uchafu unaoweza kuufikiria, watuhumiwa wote wa EPA wako ndani ya CCM, watuhumiwa wote wa TEGETA ESCROW wako ndani ya CCM, waliohusika kununua RADAR mbovu wako ndani ya CCM, aliyehusika kuuza nyumba za serikali kwa hasara yuko ndani ya chama CCM. Walionunua kivuko kibovu wote wako ndani ya CCM.

Waliohusika ku-sign mikataba mibovu ya madini na kutajwa kwenye taarifa ya makinikia, almasi na tanzanite wote wako ndani ya CCM, watuhumiwa wa rushwa kina Mnyeti aliyenunua madiwani kwa rushwa yuko ndani ya CCM na kapanda daraja. Watuhumiwa wa vyeti feki kina Bashite wako ndani ya CCM, Wahujumu wa maliasili wote wako CCM, wanaovunja katiba makusudi wote wako ndani ya CCM, ni uchafu gani ambao utaukosa ndani ya CCM.

Wote hao wako CCM na wanaCCM kwao hawauoni huo kuwa ni uchafu kwa sababu wote ni wachafu, ila siku Bashite atakapoondoka CCM "ndani ya handaki la uchafu" wanaCCM hao hao wataanza kumshambulia kuwa kafoji cheti.

Juzi baada ya Nyalandu kutoka ndani ya handaki la uchafu la CCM na kuomba kuhamia CHADEMA ndipo wanaCCM walipouona uchafu wake, laiti angeendelea kubaki shimoni kama wengine wanaoendelea kumvumilia uvundo hakuna yeyote angethubutu kumpigia kelele.
 
Chadema ni sawa na kichwa cha mwandawazimu mpya... kila kitu anachoona anachekelea tu.
 
Nafikiri Trump aliisoma thread yangu hii kabla ya kusema 'shithole countries'.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom