CCM sasa yasaka fedha za uchaguzi kwa simu za mikononi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa yasaka fedha za uchaguzi kwa simu za mikononi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,427
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  Na Sadick Mtulya

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinaonekana kimeanza kuziogopa fedha za mafisadi, baadala yake kimeanza kuchangisha fedha kupitia kwa wananchama wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2010 kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (meseji).

  Hatua hii ya CCM inafuatia chama hicho kutuhumiwa kufadhiliwa katika uchaguzi mkuu na fedha zilizopatikana kwa njia ya ufisadi.

  Hatua hiyo pia ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliyewahi kukigiza chama hicho kutafuta vitega uchumi ili kisitegemee misaada kutoka kwa wafadhili.

  Mweka Hazina wa CCM taifa, Amos Makala alitangaza mpango huo juzi katika Uwanja wa majimaji, wilayani Songea, Ruvuma wakati akiwasimika makanda watano wa Umoja wa vijana UVCCM mkoani humo ambazo ziliambatana na kupongezana kwa kupata ushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Makala alisema CCM imefikia uamuzi huo ili kutoa fursa kwa wanachama wake wote kupata nafasi ya kukichangia chama hicho na kuondokana na kutegemea fedha za wafadhili ambazo nyingine ni ufisadi.

  "Kuanzia hii leo (juzi) CCM inatangaza rasmi kuanza kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, na miongoni mwa mbinu tutakazozitumia ni kuchangia kwa njia ya simu za mkononi kupitia ujumbe mfupi(meseji)," alisema Makala.

  Mweka hazina huyo alisema kutokana na CCM kuwa na wanachama milioni nne wanatarajia kupata zaidi ya Sh40 bilioni kwa kupitia mpango huo.

  "Kwa kuwa tunawanachama milioni nne nchini kote na kila mmoja akichangia Sh1000, tuna uhakika kwa mwaka mmoja kupata Sh40 bilioni," alisema.

  Makala alifafanua kwamba mpango huo pia utasaidia kuondoa dhana ya kuwa CCM ni chama kinachoendeshwa na mafisadi.

  Katika sherehe za kusimikwa ukamanda mbunge wa Piramiho, Jenister Mhagama alisimikwa kuwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Songea.

  Mwenyikiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja amesema uamuzi wa CCM kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2010 njia ya ujumbe wa mfupi (meseji) ni kipimo tosha cha kuonyesha kama chama hicho kinakubalika au la.

  "Siku zote chama si kampuni na kinajengwa na wanachama na hao wanachama pamoja na wakereketwa ndio vyanzo tegemezi vya chama chochote duniani. Sasa utaratibu huu ni kipimo tosha cha kuonyesha kama CCM inakubalika au la,"
  alisema Mgeja.

  Mgeja alisema pamoja na wazo hilo kuchelewa lakini limefika katika wakati muafaka na linakwenda na wakati.

  Tayari Chama Demokarsia na Maendeleo (CHADEMA), kilishaanzisha mpango wa kupata wanachama wake kwa kutumia ujumbe wa simu ambao unatarajiwa kukipatia chama hicho fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi.

  CCM hivi sasa inahusishwa na makada wake ambao ndio wachagiaji wakubwa wa chama hicho katika uchaguzi kuhusishwa na tuhuma za ufisadi hali ambayo chama hicho kinaonekana kukumbia uhalifu.

  Katika hali ya kujisafisha zaidi chama hicho hivi sasa kimeamua kufanya uchunguzi maalumu wa kuwabaini wanachama wake wanaovujisha siri mbalimbali kutoka katika vikao nyeti vya chama hicho.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya siri mbalimbali zikiwemo za kuchafuana na kudhalilishana miongoni mwa mawaziri na wabunge wake katika vikao vya ndani vya chama kuwekwa hadharani.

  Hali hiyo ilijitokeza mara nyingi ikiwa ni pamoja na zilizotovunjiwa hivi karibuni mjini Dodoma katika vikao vilivyofanyika chini ya kamati ya Mzee Mwinyi inayotafuta kiini cha mgawanyiko ndani ya CCM.

  "Kwa kweli tunasikitishwa na tabia ya wana CCM kuvujisha siri za vikao halali vya chama. Kutokana na mwenendo huu tunafanya uchunguzi maalumu ili kuweza kuwabaini wanaovujisha siri zetu,"
  alisema Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa juzi jijini Dar es Salaam.

  Msekwa alisema pamoja na kuwepo kwa tabia ya uvujishaji wa siri hizo, bado hawajapata sababu za siri hizo kuwekwa hadharani.

  Bila kuzitaja mbinu watakazo zitumia kuwabaini wanaovujisha siri hizo, Msekwa alisema tabia hiyo wataithibiti.

  "Pamoja na kuwa bado hatujapata sababu za siri zetu kutolewa kabla ya muda, tunaamini tabia hii tutaithibiti na kuiondoa ndani ya CCM," alisema Msekwa.

  Msekwa alisema katika kurejesha maadili kwa wanachama wake CCM imeamua kuvirudisha vyuo vya mafuzo ya uongozi wa siasa nchini.

  Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika kuwepo kwa madhara makubwa ya kimaadili katika siasa na pia chama hicho kupata uwezo wa kifedha.

  Msekwa alifafanua kwamba, madhara hayo yametokana na viongozi wengi wa siasa hivi sasa kutopitia katika vyuo maalum vya mafunzo ya uongozi.

  "Kwa kuanzia, CCM inatarajia kufungua chuo chake kipya cha mafunzo ya uongozi mkoani Iringa na chuo hiki si tu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanasiasa pekee bali hata kwa wafanyakazi wengine wa chama ambao watakuwa wanakwenda kupata mafunzo mbalimbali," alisema Msekwa.

  Makamu mwenyekiti huyo alisema ujengaji wa chuo hicho umetokana na CCM kupata uwezo wa fedha wa kuendesha chuo hicho ikiwemo kuwalipa walimu.

  Alisema awali vyuo vya mafunzo ya uongozi ikiwemo cha Malimu Nyerere vilikuwa vikiendeshwa kwa fedha za ruzuku iliyokuwa ikitolewa na Serikali lakini vilikufa kutokana kuacha kuchukua ruzuku hiyo mara baada kuingia kwa vyama vingi vya siasa 1992.

  "Mbali na chuo cha mafunzo ya uongozi cha Mwalimu Nyerere ambacho watu wengi ndio wanakikumbuka hadi leo. Tulikuwa na vyuo sita vya namna hiyo katika kanda, vilikufa kwa sababu CCM kupitia Nec iliamua kuacha kuchukua ruzuku ya kuviendesha kutoka serikalini," alisema Msekwa
   
 2. l

  libaba PM Senior Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  LABDA WANATAKA KUACHANA NA FDHA ZA KINA RA , Manji na Jeetu Patel.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,427
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  mbona wameshateua timu ya wapambe wa uchaguzi na hao juu wapo wote...hawa wanawapiga wabonogo mchanga wa macho pesa zinachotwa pale pale kwa NDULU Gavana AMINI USIAMINI nyie mbaki na masahairi walizipata toka kwenye sms
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,427
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka hadharani mkakati wake wa kupata fedha za kugharamia Uchaguzi Mkuu ujao ambapo kuna uwezekano Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akahusika kutembelea mikoa kuhamasisha harambee ya kukichangia chama hicho.

  Aidha, chama hicho pia kinapanga kutumia hazina ya wanachama wake karibu milioni nne, kujipatia karibu Sh bilioni 40 kupitia mchango wa Sh 10,000 kwa kila mwanachama. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Uchumi na Fedha, Amos Makalla, alitoa mkakati huo mwishoni mwa wiki na kuwataka wana CCM nchini kote kujiandaa kujitolea kukichangia chama fedha ili kifanikishe uchaguzi huo.

  Akielezea mikakati hiyo mjini Songea mwishoni mwa wiki, Makalla ambaye alipokea maandamano yaliyoandaliwa kusherehekea ushindi wa chama hicho kilichojinyakulia asilimia 97 ya viti vya vitongoji na vijiji katika Mkoa wa Ruvuma, kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni, pia alitamba kuwa CCM itaendeleza ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu 2010.

  Katika hotuba yake hiyo, Katibu huyo alieleza kwa undani mikakati mitatu ya idara yake itakayopendekezwa katika vikao vya chama hicho hivi karibuni kama njia ya kukipatia chama fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo.

  Mikakati hiyo inahusisha kuchangisha michango hiyo ya Sh 10,000 ambayo ni ya hiari kwa wanachama, kufanya harambee za mikoa na kuhamasisha michango mingine kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi.

  "Hapa nina maanisha kama mwanachama mmoja mmoja wa CCM akichangia elfu kumi tena alipe kidogo kidogo kwa miezi sita, chama kina uhakika wa kupata Sh bilioni 40," alisema Makalla.

  Amewata viongozi wa mikoa na wilaya kuimarisha kamati zao za uchumi na kuandaa harambee za mikoa na ikibidi katika harambee hizo, mgeni rasmi awe Mwenyekiti wa Taifa na kuhimiza maandalizi hayo yaanze sasa.

  Kuhusu njia ya kutuma ujumbe kwa njia ya simu, Makalla alisema si muda mrefu chama kitazindua utaratibu utakaotumika mara baada ya kufanyika vikao hivyo.

  Amewataka Watanzania wenye mapenzi na CCM kujitokeza kwa wingi kutuma ujumbe mara baada ya uzinduzi huo kwani kufanya hivyo ni kukijenga chama chao.

  Amewahakikishia wanachama kuwa CCM itashinda uchaguzi ujao kwa kishindo kwa sababu ya mikakati kabambe ambayo wameanza kujiandaa nayo.

  Ameipongeza serikali kupeleka muswaada bungeni wa uwazi wa mapato na matumizi wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi na kuongeza kwamba muswaada huo umekuja muda muafaka sana na utasaidia vyama kuwa wazi katika mapato na matumizi.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,427
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  matapeli watupu nyie endeleeni kutulipua hapo bot achaneni na siasa zenu za sms..kwa nini watu wasipige simu kabisa wawaingizie nyingi zaidi...yaani
  najuta kukufahamu ccm chama changu
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na hawa nao kwa kuiga ..wameona CHADEMA wameanzisha hii nao wanataka yaani ubunifu sifuri...waongo hawa wanajifanya kuchangisha hela kwa meseji kumbe mijizi mikubwa
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Watatumia zaidi kampuni gani kukusanyia hizo pesa? nadhani ni VODACOM :confused:
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  nilitaka kusema hilo mkuu.haya ni majizi tuu yanataka kutudanganya eti yamechanga hela za kampeni kwa sms???kweli sisi ni wadanganyika..MAJIZI haya
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani CCM majizi sana..kwa kweli mkuu hauko peke yako unayejuta kuwafahamuu...Juzi wameunda kamati au ndo ya kuhesabu wamepata sms ngapi na ni sh ngapi?haki ya mungu tutakuja kuwaomba watoe print out ya hizo sms tuhesabu ni shilingi ngapi wamekusanya kama hatujastaajabu ya musa
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo nimeamini kuwa Chadema ni wabunifu na jamaa zutu wakongwe wameshazeeka na wanakopi vitu katika kuzuga. Hili wazo la kuongeza mapato ya chama kuelekea uchaguzi kwa njia ya sms ni la Chadema kama sikosei na walishazindua mpango huo baada ya mkutano wao mkuu. Sasa jamaa ndio wanakurupuka toka usingizini na kusema hayo bila hata tafiti yeyote. Ama kweli wamezeeka na kuchoka.
   
 11. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CCM hawahitajii pesa kutoka kwa wanachama wake hiyo ni danganya toto (Amka)
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hawana lolote ni danganya toto tu. Wanataka baadaye waje waseme kuwa wamepata fedha kwa kuchangiwa na wanachama kumbe waliochangia ni hao hao fisadis
   
Loading...