CCM sasa waikumbuka TANU; Nape Nnauye chama kukumbuka kazi ya kupigania Uhuru iliyofanywa na Tanu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa waikumbuka TANU; Nape Nnauye chama kukumbuka kazi ya kupigania Uhuru iliyofanywa na Tanu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 4, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 03 July 2011 20:25 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Raymond Kaminyoge

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kinapita katika hatua ngumu ya mabadiliko, kimetangaza kurejea kwenye mizizi yake kwa kufanya kumbukizi la Tanu.

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa chama hicho kimekusudia kuanza kujitathmini kwa kukumbuka kazi ya kupigania Uhuru iliyofanywa na Tanu.

  Tanu (Tanganyika African National Union) ni chama ambacho kiliundwa Julai 7, 1954 na kilitumika kupigania Uhuru wa iliyokuwa nchi ya Tanganyika (sasa Tanzania Bara).

  Ilipofika Februari 5, 1977 Tanu kilingana na ASP (Afro Shiraz Party) cha Tanzania Visiwani na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali hadi sasa.

  "Itakumbukwa TANU ilizaliwa tarehe 7 Julai, 1954 hapa Dar es Salaam, New Street mtaa ambao sasa unafahamika kama Lumumba, mahali ambapo kuna Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu. Huo ukawa ndio mwanzo wa harakati za kudai Uhuru, Utu na Heshima ya Mwafrika katika nchi yetu,"alisema Nape na kuongeza:

  “Kwa kuwa chama hiki ndicho kilicholeta uhuru hapa nchini, na mwaka huu tunatimiza miaka 50 ya Uhuru tumeamua kufanya sherehe za kuzaliwa kwa Tanu”.

  Rais Kikwete kushiriki
  Kwa mujibu wa Nape, mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atashiriki maadhimisho hayo kwa kuzungumza na mabalozi wa nyumba kumi wa mkoa wa Dar es Salaam ili kujadili changamoto na mafanikio ya chama hicho.

  Alisema katika mkesha wa kuamkia Alhamisi ijayo, Rais Kikwete atashiriki katika sherehe hizo ambapo Alhamisi asubuhi atakutana na mabalozi wa nyumba kumi wa jijini Dar es Salaam.

  “Usiku huo wa mkesha wanachama wa CCM watakuwa kwenye matawi yao katika maeneo mbalimbali kufanya shamrashamra za kuzaliwa kwa Tanu, kutakuwa na shughuli kadhaa ikiwemo kuwasha mafataki,” alisema Nape.

  Alisema Alhamisi hiyo, wanachama watakutana kwenye matawi yao na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo kufanya usafi, kusaidia ujenzi, kupanda miti na kutembelea wagonjwa hospitalini.

  Aidha, Nape alisema siku hiyo pia wanachama watatakiwa kufanya mikutano ya hadhara matamasha ili kujikumbusha mafanikio yaliyopatikana kwa kila mkoa, wilaya katika kipindi cha miaka 50.

  “Tumekuwa tukiambiwa CCM haijafanya kitu, siku hiyo viongozi wetu watumie nafasi hiyo kuwaelewa wananchi ni mafaniki gani yamepatikana katika ngazi za wilaya na mikoa,” alisema Nape.

  Nape aliongeza, “ viongozi wa CCM muwaeleze wananchi kabla ya uhuru, tulikuwa na barabara zenye urefu kiasi gani na sasa ziko vipi, pia sekta ya elimu na afya mkilinganisha kabla ya uhuru na baada ya miaka 50 ya uhuru.”

  Mapito ya CCM
  ​CCM kinafanya kumbukizi hilo la Tanu wakati ambao kinapita katika hatua za mabadiliko ambayo tayari yameanza kusababisha mivutano ya ndani kwa ndani miongoni mwa viongozi wakuu wa chama hicho.

  Moto huo wa mabadiliko ulianza Aprili mwaka huu wakati kikao cha halmashauri kuu ya CCM iliporidhia kuvunjwa kwa Kamati Kuu na Sekretarieti yake, kisha vyombo hivyo kuundwa upya chini ya kaulimbiu maarufu ya ‘kujivua gamba’.

  Wakati wa maadhimisho ya miaka 34 tangu kuzaliwa kwa CCM, Rais Kikwete alisema chama hicho kinalazimika kuachana na wanachama na viongozi ambao ni mzigo kwake, hivyo kukifananisha na nyoka ambaye huwa anajivua gamba linapochakaa.

  Mabadiliko hayo ndiyo ni kama yamezua mvutano wa chini chini kutokana na kauli za dhihaka ambazo zimekuwa zikitolewa dhidi ya uamuzi huo wa CCM kwamba hauwezi kuwa na tija, huku sekretarieti mpya ikiongozwa na Wilson Mukama ambaye ni Katibu Mkuu ikitoa matamshi makali dhidi ya kejeli hizo.

  Hivi sasa kinachosubiriwa ni hatua zitakazochukuliwa na NEC ya CCM ambayo inaweza kukutana wakati wowote mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao, dhidi ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi ambao tayari wamekutana kwa faragha na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Pius Msekwa.

  Mazungumzo baina ya watuhumiwa hao, Andrew Chenge, Rostam Aziz na Edward Lowassa bado ni siri kubwa na kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CCM, kilichozungumzwa katika faragha hiyo kitakuwa “ni taarifa ya Msekwa katika vikao vikuu vya chama hicho”.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Vipi Kumbukumbu ya ASP?
   
 3. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  eti zimebaki siku ngapi kutimia siku tisini za nape? au deadline ni lini? magamba yamegoma?
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama sikosei trh 6 au 7 ndiyo deadline ya RACHEL siku wanaomboleza sijui anazaliwa marehemu TANU.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nnape kafanya kosa la mwaka kawatenga ASP ina maana siku hiyo kama wewe ulikuwa ASP siyo siku yako.
   
 6. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  zimebaki siku sita duu kwa hili sijui wananchi kama watatuelewa maana hakuna gamba hata moja lililong'oka.!!!
   
 7. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Jamani kipindi hicho tulikuwa bado tunamsomesha NNAPE, hilo swali mmulize mkama ndo atalijibu vizuri NNAPE mnamuonea tuu!!!
   
 8. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Hapana mimi siku hiyo nilikuwepo ndani ya kikao, ni tarehe 9 mwezi huu ndo deadline ya RACHELO
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hata kama alikuwa hajazaliwa ina maana hajui ASP iliungana na TANU mbona anawatenga wana ASP
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hata mimba ya mtoto huyu ilikuwa bado haijatungwa.
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hao wanaleta matani, wanaleta mizaha mbele ya tanu yetu ya watanganyika wote! Toka lini mafisadi wakakumbuka wanyonge? Nepi anatuzingua!
   
 12. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Swali langu ni je kama sherehe hizo zitafanywa na wanachama wote wa CCM, wanachama waanzilishi wa ASP kilichoungana na TANU watakuwa upande gani, wageni waalikwa? Je hili haionekani kama Nape anataka kuzalisha mtafaruku mwingine ndani ya chama chake.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  ASP haikuzaliwa tarehe 7/7.
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Itakapofika tarehe iliyozaliwa ASP kumbukizi itafanyika. TANU ilizaliwa tarehe 7. 7. 1954. Hata serikalini tunaadhimisha 9/12 na 12/1 kila mwaka separately na haina madhara kwa yeyote.
   
 15. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unaweza kutuambia ilizaliwa lini na siku hiyo ya sherehe 7/7 wao watakuwa watazamaji au wageni waalikwa
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sijui ASP ilizaliwa lini. Wazanzibari wako humu watusaidie. Kwani miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Wazanzibari watakuwa watazamaji au wageni waalikwa?
   
 17. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na wazanzibar wakifanya sherehe, sis bara tunasema wanataka kuvunja muungano. Hiki nini nepi anafanya. Halafu na wewe kiwete unaangalia tu. Mbwiga wewe.
   
Loading...