CCM Sasa Waanza Kuikubali CHADEMA

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Walianza kizota baada ya kuitumia kunadi sera kwa wapiga kura wa wajumbe wa NEC katika zile nafasi 10, kila aliyenadi sera kwa wapiga kura alitoa ahadi ya kupambana na CHADEMA

Jana nimemsikia Waziri mstaafu Edward Lowasa akisema elimu ya sekondari kutolewa bure inawezekana, kumbuka hiyo ilikuwa ni sera ya CHADEMA iliyopingwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu 2010

Ni kamsikia tena Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyekiti wa CCM viwanja vya mnazi mmoja akisema kwa wanachama tukazane kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi kama wenzetu wanavyofanya (CHADEMA) vinginevyo chama chetu kitaangamia

Nawasilisha
 
Mkuu hivi kweli wewe hujasome UPE,(Universal Primary Education), seara ya mwanzo kabisa CCM.
 
chadema inatakiwa ibuni mikakati mingine hasa ya ushindi bila hivyo mambo yatakuwa magumu 2015
 
chadema inatakiwa ibuni mikakati mingine hasa ya ushindi bila hivyo mambo yatakuwa magumu 2015

Mikakati ipi ebu jaribu kufafanua zaidi, lakini si umeona jamaa walishakubali, wamebana sasa wameacha kuachia , 2015 nyavu lazima zitikisike
 
Mkuu hivi kweli wewe hujasome UPE,(Universal Primary Education), seara ya mwanzo kabisa CCM.

Kama ni hivyo na wanajua hayo yanawezekana kwa nini ? 2010 walibisha sana kuwa kusomesha bure haiwezekani , Mbona EL kaenda zaidi kuwa secondary pia inawezekana ?
 
Wanawakubali cdm muda mrefu tu ila wanafanya shingo zao ngumu, na katibu wao pia si ameitaka serikali kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi ili wananchi wa kipato cha chini wawe na makazi bora, nakumbuka na hii pia ilikuwa sera ya CDM.......NA BADO WATAKOPY KILA KITU.......CCM WABAYA.
 
ccm vichwa maji tu sera hii ilikuwepo kwa mwalimu Nyerere walimuona hana akili lakini leo hii wameshaanza kuwakubali na kurudia kile Nyerere alichokuwa anakifanya.
 
Viongozi wengi wa TZ hawana experiences za kuwa challenged katika jambo lolote - hata katika ajira. Kwa hiyo kunapotokea challenges wanakimbilia kulalamika kuwa AAAHHH so and so anataka CHEO CHANGU. Na hili linaonekana ni tatizo kwa siasa za TZ. Badala ya kushindana kwa lengo la kutoa alternatives solution to the problems facing the nation - wamekaa kuangalia nani anataka kuwa rais wa nchi - kufilisika mawazoo!
 
Kama ni hivyo na wanajua hayo yanawezekana kwa nini ? 2010 walibisha sana kuwa kusomesha bure haiwezekani , Mbona EL kaenda zaidi kuwa secondary pia inawezekana ?
Kama unakubali UPE ilikuwepo(ambayo ni sera ya CCM),basi ni vema ukakubali kuwa CDM imekopi na kupesti.
 
Kama ni hivyo na wanajua hayo yanawezekana kwa nini ? 2010 walibisha sana kuwa kusomesha bure haiwezekani , Mbona EL kaenda zaidi kuwa secondary pia inawezekana ?

walipinga kwa vile hawa kuwatayari kupunguza mgawo wa kifisadi.
 
Kama unakubali UPE ilikuwepo(ambayo ni sera ya CCM),basi ni vema ukakubali kuwa CDM imekopi na kupesti.

Na kama cdm ilicopy na kupaste waliiga yale ya Mwalimu Nyerere amboyo kwa CCM ya leo hayaonekani kuwa ya maana, sasa mpaka hapo unafikiri nani zaidi kati ya CCM ya leo ya wezi na CDM ?
 
Kwa kichwa hiki cha habari CCM hapo wanamaanisha vita/uadui literary. Utaniambia.

CCM hawajakomaa kisiasa kwa kukubali changamoto na ushindani wa kweli ktk uwanja sawa. Na CHADEMA wanalijua hili vizuri, ingawa sina hakika wamejipanga vipi kuhakikisha wanavuka na kushinda 2014 na 2015.
 
Ujenzi wa chuo cha Dodoma hakikwepo ktk ilani ya ccm 2005 ni agenda ya Cdm, elimu bure, vifaa vya ujenzi kupunguza kodi ili wananchi waepukane na nyumba za tembe, Mtikila na mgombea binafsi ni hoja ya wapinzani, kwann wasikabidhi nchi sasa 2015 mbali mali zinazidi kutoroshwa.
 
Na kama cdm ilicopy na kupaste waliiga yale ya Mwalimu Nyerere amboyo kwa CCM ya leo hayaonekani kuwa ya maana, sasa mpaka hapo unafikiri nani zaidi kati ya CCM ya leo ya wezi na CDM ?

Chama makini kinapaswa kutenda sawa sawa na maneno yake,ninakumbuka hii hoja ya elimu bure iliyo ktk ilani ya Chadema(uchaguzi 2010)ilipingwa sana tena kwa nguvu zote na baadhi ya viongozi wa ccm(Stephen Wasira/Nnape)na wengine wengi na kusema Chadema iache kuwahadaa wananchi kwa kusema kuwa itatoa elimu bure.Kama ccm ilipinga hakuna elimu bure na leo wanakuja kula matapishi yao sasa hapo nani popompo kati ya Chadema au ccm?Siku zote ukweli hujitenga ktk uongo.
 
Na kama cdm ilicopy na kupaste waliiga yale ya Mwalimu Nyerere amboyo kwa CCM ya leo hayaonekani kuwa ya maana, sasa mpaka hapo unafikiri nani zaidi kati ya CCM ya leo ya wezi na CDM ?

Naona hujajipanga vizuri.
Hoja kuwa CCM ina iga sera za CDM nimelikanusha kwa kukuletea mpango wa UPE.

Sasa hoja yako haijulikani ni ipi sasa maana si kweli kuwa elimu ya bure kama sera iliasisiwa na CDM.
Waulizeni viongozi wenu CDM karibu wote walisoma bure enzi ya Mwalimu.

Sasa ukianza kuongea juu ya ufisadi basi anzisha thread nyingine uchangiwe.
 
Back
Top Bottom