CCM sasa vurugu tupu, Mukama akiri ni kama NATO na G8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa vurugu tupu, Mukama akiri ni kama NATO na G8

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 31, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Source Mwananchi

  Chama cha Mapinduzi CCM kimekiri kuwa Makundi yanakiuwa chama na ugomvi na vurugu hizo ni sawa na ugomvi wa Nato na G8 na wakati huo huo Maige kamtaja Nape kama gamba sugu linalotakiwa kung'olewa ndani ya chama na Amemtahadharisha Spika Makinda kuwa katika kikao cha Bajeti atasema madukuduku yake yote yanayomsumbua.

  Nchi zinazounda G8 ni Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Russia na Uingereza ambazo pia baadhi yao, ndizo zinazounda Nato, umoja wenye wanachama 28.

  Mukama alitoa kauli hiyo juzi wilayani Rufiji wakati akizungumza na umati wa wananchi na wanachama wa chama hicho waliofurika katika Viwanja vya Corecu, Kata ya Kibiti.

  Alisema baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa ni wasaka madaraka na wanapokosa huamua kuunda makundi ya uhasama ambayo hawataki kuyavunja pindi mchakato wa kutafuta mgombea unapomalizika.

  “Makundi yaliyoundwa tangu 2005 na 2010 yanaendelea kukitafuna chama, wanachama wakinyimwa uongozi wanaanza uhasama, hatufiki malizeni makundi,” alisema.

  Alisema makundi hayo pia yako katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji, ambako katika ziara yake amebaini mpasuko mkubwa unaotokana na fitina na uhasama miongoni mwa wapenzi na makada wa CCM na kusisitiza kwamba hayafai na ni hatari kwa mustakabali wa chama hicho kikongwe barani Afrika.

  “Nikiwa Mkuranga nilitaarifiwa kuwa kuna makundi ya Nato na G8 na sasa nimefika Rufiji nimeyakuta makundi hayo. Jamani makundi hayo ya nini?”
  Mukama ambaye aliwahi kushika nafasi mbalimbali za kiutendaji zikiwemo za Ukuu wa Wilaya ya Mafia akimrithi mtangulizi wake Hemedi Mkali, alisema aliwahi kugombea ubunge wa viti vya Taifa kupitia Juwata (iliyokuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania), na aliposhindwa alikubali matokeo.

  Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema bila CCM imara nchi yetu itayumba, akimaanisha kuwa hakuna chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi yake.

  Alitoa mfano wa Chama cha Democrat cha Marekani kwamba wanachama wake hawana kadi, bali mapenzi ya chama yako mioyoni mwao na wanapojiunga hawafanyi hivyo kwa lengo la kusaka madaraka... “Hii ni tofauti kubwa na nchi zetu ambako mtu akijiunga na chama kitu kwanza kufikiria ni kusaka madaraka,” alisema.

  Alisema chama hicho kina mkakati madhubuti wa kupambana na watu wachache wanaotaka kukimiliki wakitumia nguvu ya fedha.

  Alisema baadhi ya wanachama wa kawaida wamejiona kuwa hawana nafasi katika chama chao wakiamini kuwa kimetekwa na wenye fedha na kuongeza kwamba mwanachama wa kawaida hawezi kuongoza bila rushwa.  Katika Tanzania Daima Ya Nape na Maige

  KATIBU wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye ametajwa kuwa gamba namba moja linalotakiwa kuvuliwa, kwa kile kilichodaiwa kutoa matamshi mengi ambayo yamekivunjia heshima na kukidhohofisha chama hicho.

  Nape pia ameshutumiwa kwa kushindwa kwake kubuni mbinu za kuingiza wanachama na zaidi kupambana na wimbi la kuhama kwa viongozi, makada na wanachama wa CCM.

  Shutuma hizo nzito zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige (CCM) jana wakati akizindua matawi mawili ya wakereketwa wa chama hicho ambao ni wajasiriamali, katika Kijiji cha Isaka wilayani hapa.

  Maige alisema kuwa Nape amekuwa akitoa kauli ambazo si za msingi, zisizojenga bila kujua kuwa zinakidhohofisha chama hicho tawala.

  Mbunge huyo ambaye amepata kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa la wana CCM wanaohamia vyama vya upinzani, ambalo ilitegemewa kuwepo kwa juhudi za makusudi za kuzuia chini ya usimamizi wa katibu huyo wa itikadi na uendezi.

  “Kitendo cha CCM kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza anasema hajali na eti hao ni makapi,” alisema kwa kushangaa.

  Nape akihutubia vijana mjini Bukoba siku chache zilizopita, alidai kuwa hata kama wanachama wote watahama, yeye (Nape) atabaki peke yake na CCM haitakufa.

  Alidai kuwa kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haiwezi kupuuzwa na kiongozi makini, na kuongeza kuwa zinahitajika busara na bidii za kuwapa moyo waliopo ili nao wasiondoke na si kuwasimanga.

  “Jamani Nape anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama.

  “Ninalolisema hapa lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilionao kwa chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama, tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema kabla mambo hayajaharibika?”

  Maige alimwomba Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja kutumia nafasi yake kuwashauri wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya Nape.

  Wakati Maige akitoa maneno hayo mazito, Mgeja alikuwa ameinamisha kichwa chake chini, lakini mamia ya wana CCM pamoja na wananchi wengine walishangilia kwa nguvu.

  Jk chama kinamfia mikononi mwake
   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi hili lichama mbona halijifii mbali huko aaaaahhhhhhhhhhhhh...................
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Nasikia ccm wameshaanza kufanyia ukarabati monchwari ya muhimbili kwaajili ya kuweza kuhifadhiwa kwani mazishi ni mbali sana 2015
   
 4. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,820
  Likes Received: 4,186
  Trophy Points: 280
  Nape ameahidi kubaki na gamba hata wakijivua wote, ana uchungu na chama kuliko hata waasisi wake!
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Magamba yanaruka na kukanyagana!
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wenyewe watakwambia Chama imara kama Chuma.
   
 7. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  wataumana mpaka basi!hiyo ni lahana tupu,dhulum,ufisadi,uonevu na manyanyaso dhidi ya wanyonge.waende kuzimu mashetani hawa
   
 8. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bora mtupunguzie CDM kazi, muanze kuvuana wenyewe alafu sisi tunakuja kuwaogesha na kuwavalisha magwanda
   
 9. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Jamani tuwaacheni wafu wazike wafu wao,sisi tusonge mbele
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Utangoja sana.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mukama na Nape ni kama misguided missiles ndani ya CCM ni kama wako pale kimakosa hawajui hata wanatakiwa wafanye nini.

  Ni huyu huyu Mukama alisema makundi ndani ya chama ni uhai leo anasema yanakivuruga chama. Nape naye na kauli za kwenye karatasi anatamka lolote analoona linamjia kichwani kwa furaha ya siku moja hajui kwamba matamshi yake ni ya chama si ya familia yake. In short, hawana tangible strategy yeyote ya kujenga chama kinachobomoka kama tulivyokuwa tunaona enzi za kina Makamba na Mangula.
   
 12. K

  KIMBULU Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wakati muafaka saana kwa CHADEMA kujijengwa wakti huu, CCM ikiwa imesambaratika kifikra, kwani hawapo pamoja. Ktk strategic magt, unaangalia weakness za mpinzani wako na capiltalize nazo, Hivyo CHADEMA capiltalize ktk CCM kutoelewana na makundi yao, hata ikibidi penyezeeni watu huko kufuel zaidi. Naona Maige anaenda vizuri ktk hilo.
   
 13. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,312
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ccm wameshindwa kuvuwana magamba sasa waanza kukandamizana masumbwi hapo sawa.kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wakiniambia nitoe hela ya ukarabati I will give them i don't want to hear more about mafisdi jamani they are killing our people.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 30 May 2012 21:00[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  MUKAMA ASEMA KINA MPASUKO MKUBWA KAMA G8, NATO

  Amini Yasini, Rufiji na Ahmed Makongo, Kahama

  HALI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), si shwari na Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama amekiri kwamba hivi sasa kina mpasuko mkubwa unaotokana na makundi yanayofanana na yale ya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato) na Umoja wa Mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani (G8).

  Wakati mtendaji mkuu huyo wa chama tawala akitoa kauli hiyo, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameibuka na kumshambulia waziwazi, Katibu wa Taifa wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akimtuhumu kukiharibu kwa utendaji mbovu, hivyo kutaka ang'olewe haraka akidai kuwa ni gamba.

  Nchi zinazounda G8 ni Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Russia na Uingereza ambazo pia baadhi yao, ndizo zinazounda Nato, umoja wenye wanachama 28.

  Mukama alitoa kauli hiyo juzi wilayani Rufiji wakati akizungumza na umati wa wananchi na wanachama wa chama hicho waliofurika katika Viwanja vya Corecu, Kata ya Kibiti.

  Alisema baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa ni wasaka madaraka na wanapokosa huamua kuunda makundi ya uhasama ambayo hawataki kuyavunja pindi mchakato wa kutafuta mgombea unapomalizika.

  "Makundi yaliyoundwa tangu 2005 na 2010 yanaendelea kukitafuna chama, wanachama wakinyimwa uongozi wanaanza uhasama, hatufiki malizeni makundi," alisema.

  Alisema makundi hayo pia yako katika Wilaya za Mkuranga na Rufiji, ambako katika ziara yake amebaini mpasuko mkubwa unaotokana na fitina na uhasama miongoni mwa wapenzi na makada wa CCM na kusisitiza kwamba hayafai na ni hatari kwa mustakabali wa chama hicho kikongwe barani Afrika.

  "Nikiwa Mkuranga nilitaarifiwa kuwa kuna makundi ya Nato na G8 na sasa nimefika Rufiji nimeyakuta makundi hayo. Jamani makundi hayo ya nini?"
  Mukama ambaye aliwahi kushika nafasi mbalimbali za kiutendaji zikiwemo za Ukuu wa Wilaya ya Mafia akimrithi mtangulizi wake Hemedi Mkali, alisema aliwahi kugombea ubunge wa viti vya Taifa kupitia Juwata (iliyokuwa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania), na aliposhindwa alikubali matokeo.

  Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema bila CCM imara nchi yetu itayumba, akimaanisha kuwa hakuna chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi yake.

  Alitoa mfano wa Chama cha Democrat cha Marekani kwamba wanachama wake hawana kadi, bali mapenzi ya chama yako mioyoni mwao na wanapojiunga hawafanyi hivyo kwa lengo la kusaka madaraka... "Hii ni tofauti kubwa na nchi zetu ambako mtu akijiunga na chama kitu kwanza kufikiria ni kusaka madaraka," alisema.

  Alisema chama hicho kina mkakati madhubuti wa kupambana na watu wachache wanaotaka kukimiliki wakitumia nguvu ya fedha.

  Alisema baadhi ya wanachama wa kawaida wamejiona kuwa hawana nafasi katika chama chao wakiamini kuwa kimetekwa na wenye fedha na kuongeza kwamba mwanachama wa kawaida hawezi kuongoza bila rushwa.

  "Hapana! Chama chetu hakitakubali hali hiyo. Ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu na nchi yetu," alisema na kuongeza kuwa wanachama wa kawaida wanatakiwa kugombea hata kama hawana fedha.

  Alisema chama kipo katika uchaguzi wake wa ndani na kuwataka wanachama kufanya uamuzi sahihi wa kuchagua viongozi waadilifu wasiotumia rushwa, kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha kuingia watu katika uongozi waliotoa rushwa.

  Katika mikutano yake hiyo, Mukama alitamba kuwa chama chake hakitishwi na wapita njia akimaanisha wapinzani wanaodai kuwa hakijafanya kitu.

  Alisema CCM ni chama makini na sikivu katika kusikiliza kero za wananchi akitamba kwamba kimejenga Daraja la Mkapa ambalo limekuwa kiunganishi kati ya Mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam na umeme wa gesi unaotoka kusini ambao wananchi wa Rufiji wananufaika nao kwa sasa.

  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji, Mrisho Matimbwa alisema katika uchaguzi uliopita wa chama hicho kulikuwa na makundi mawili, ya Bush na Al Qaeda ambayo kwa sasa yamekufa na kubakia mpasuko katika halmashauri kuu ambako aliahidi kuutatua.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Magamba meng'emeng'e....yanajifia kifo cha taratibu.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Yaani makundi hadii Rufiji!! Tena makundi mabaya kweli yaani G8 na NATO. Mimi nilikuwa nadhani makundi yako ngazi ya taifa tu kumbe hadi Rufiji na Mkuranga.

  Mukama anafanya nini sasa kuondoa hayo makundi? Kuishia kusema tu kwamba Baba wa Taifa alisema bila CCM imara nchi itayumba sijui kama kuna tija. Watu siku hizi hawaogopi hata nchi ikiyumba na si lazima iyumbe. CCM inatakiwa ijitakase na iondoe makundi vinginevyo 2015 CCM itakuwa sawa na KANU. Kwa afya na ustawi wa nchi inatakiwa CCM iwepo imara; iwe Upinzani ama Madarakani.
   
 18. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Muvi inaendelea,steling sijui atafia wapi
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tafunaneni tu ili mtawaliwe kirahisi!!!
   
Loading...