CCM sasa kwisha! - Kingunge Ngombale-Mwiru

nashukuru Mungu ata hawa wazee wa siasa wanaona haya maana hayawezi wala hayafai kufumbiwa macho, Mungu awalinde wazee wetu
 
Pamoja na kwamba maneno yake yana ukweli fulani lakini kuna jambo amelisema kwa mafumbo,anaposema "CDM inafanya operation sangara uvccm na ccm wakiangalia tu'' hapa sijaelewa anamaanisha nini,nadhani anataka wawadhibiti au anataka nao wapite mitaa na vitongoji kujinadi?Tumeshuhudia vyombo vyote vya dola vikiwaandama wapinzani na kuwawekea vipingamizi wasifanikishe malengo yao na sehemu nyingine wamesababisha vifo.Je hayo hayajamridhisha Kingunge? je anataka Tendwa avifungie vyama hivi ndo ataona wanafanya kazi? Siamini kama mzee huyu kazeeka bali anahamasisha vurugu,anaposema ccm anamaanisha polisi na wengineo na anaposema uvccm anamaanisha green guard ambapo tumeshuhudia vikundi hivi vikitenda kinyume cha sheria dhidi ya vyama vya upinzani.
Mimi naamini kiongozi yeyote mstaafu anayetoa mawazo natamani azungumze juu ya kuijenga tanzania na siyo chama fulani maana hakuna chama chochote kitakachotawala milele katika zama hizi za demokrasia.
 
Nasikiavyo kwamba Kingunge analalmika eti kuhusu hiyo stori eti gazeti limemnukuu vibaya.
 
Back
Top Bottom