Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
WanaJF:
Hili suala la Phili Mangula kukubali kwenda Igunga kufanya kampeni na Makongoro Nyerere kukataa kwenda mnalionaje? Ni vyema tukalijadili.
Kwa mtazamo wangu kukubali kwa Mangula kunatokana na kubanwa au kutishwa kwamba kwa kuwa anabeba tuhuma za ufisadi (msisahau EPA) ameambiwa ni bora akakubali kwenda tu vinginevyo Hivyo imebidi asalimu amri.
Makongoro yeye hana tuhuma zozote za ufisadi, kwa hivyo mara moja kawatolea nje CCM na hawawezi kumfanya kitu chochote.
Na hili pia ndiyo lilimsukuma Rostam kukubali kufanya kampeni Igunga alitishwa bila shaka, maana anazo tuhuma nyingi tu za ufisadi.
Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba CCM wanazitumia vizuri tuhuma za ufisadi zinazobebwa na baadhi ya viongozi wake katika kuwekana kwenye mstari.
Hivyo kulindana kwa malipo ndiyo kunaifanya CCM iendelee kupumua hadi sasa.