CCM Ruvuma yathibitisha kweli haiwezi kufanya maamuzi magumu kama ya CHADEMA!

NDOFU

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
656
144
Kamati kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma imethibitisha kuwa maamzi magumu hayawezi kufanyika ndani ya CCM. Hii ni baada ya kuyatupilia mbali maamuzi ya kamati ya siasa wilaya kuhusiana na kuwavua uanachama madiwani watano wa ccm wanaoendelea na msimamo wao wa kutokumtambua Meya wa manispaa ya Songea!

Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma jana alitangaza uamuzi wa kuwarudishia uanachama madiwani ambao tiyari kamati ya siasa ya wilaya ilikuwa imewavua uanachama.

NATAMANI KUSIKIA MAONI YA PINDA, NAPE, MKUCHIKA NA WANACHAMA WENGINE WA CCM WALIOKUWA WANAWAUNGA MKONO MADIWANI WALIOTIMULIWA NA CHADEMA HUKO ARUSHA.
 
MKuu madiwani watano ukiwafukuza unataka Peoples Power huko wakaweke camp ? Ngumu hiyo maana watapoteza kila kitu so wameona bora kuwa wanyonge na wadogo mama sisimizi .
 
Wanafiki siku zote utawaona tu, nani amefukuzwa CCM? magamba ni geresha tu
Join Date : 23rd August 2011
Posts : 20
Rep Power : 0
Kajipange mkuu vinginevyo utabadili ID humu.
Mbona sielewi post yako?
Nawasubiri kwa hamu namie hao kina pinda
 
CHADEMA wakati wanawafukuza madiwani wa Arusha walitamka kwamba ni heri wakose viti vyote vya udiwani lakini heshima inabaki kwenye chama!
 
Join Date : 23rd August 2011
Posts : 20
Rep Power : 0
Kajipange mkuu vinginevyo utabadili ID humu.
Mbona sielewi post yako?
Nawasubiri kwa hamu namie hao kina pinda

Hata mie ni kama sijamuelewa. Ni kama anajipinga pinga vile. Au kama hakujiandaa. Kiufupi CCM mkoa wameshausoma mchezo, wakifukuza wale madiwani watano na zile kata zimekwenda upinzani. Kata moja ya Lizaboni ambayo iko wazi baada ya kifo cha Meya inawakosesha usingizi kuikomboa ni majaliwa! Tatizo la CCM songea mjini ni uongozi wa hovyo.
 
Na Arusha CHADEMA lazima waendelee kutunza heshima yao kwa kushinda tena kwa kishindo
 
Hiki chama hakina budi kukumbatia kila mwanachama hata kama ni mbaya kiasi gani.Kisipofanya hivyo hakifiki kesho.
 
Au basi tuanze kusikia maoni ya akina FF,MWITA25,RITZ,KISHONGO,MZEE nawengineo!
 
Au basi tuanze kusikia maoni ya akina FF,MWITA25,RITZ,KISHONGO,MZEE nawengineo!

MWITA 25 alishajivua gamba mkuu lakini bahati mbaya amekula BAN na bado tulikuwa tumemuweka under probabation
 
MWITA 25 alishajivua gamba mkuu lakini bahati mbaya amekula BAN na bado tulikuwa tumemuweka under probabation


Mkuu, Mwita 25 ndiye Topical na ni mnafiki tu! Hakuna cha kujivua gamba wala nini! Ameona amekuwa na jina baya sana akaamua kujitangaza kwamba amejivua gamba. Mnafiki mtupu!
 
Kinachovutia Chadema ina madiwani 7 tu lakin wale watano wa ccm wanatoa msaada mkubwa sana kwa hawa wachache wa chadema! Sijui ccm mkoa ndo wanauogopa zaidi huu ushirikiano mpya!
 
Back
Top Bottom