Elections 2010 CCM Rukwa yambembeleza mgombea wa CHADEMA awaachie

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,679
20,433
Habari zilizonifikia zinasema kwamba matokeo ya ubunge Sumbawanga mjini yameshakamilika ila CCM imemleta Mizengo Pinda na sasa hivi kuna kikao kinachoendelea cha kumbembeleza mgombea wa CHADEMA asaini form nyingine kuonyesha kwamba ameshindwa. Hadi sasa mgombea huyo hajawakubalia, ila tume ya uchaguzi jimboni humo imesema itatangaza matokeo saa sita usiku, wakati yale ya urais yameshatangazwa tayari. CHADEMA makao makuu mpoo?
 
tafadhali jamani msikubali hili tunahitaji ukombozi chadema msiuze nchi kwa mafisadi wananchi wamewaaamini ninyi!
 
Jamani CHADEMA inabidi kuwasiliana na wabunge wetu wateule, kununuliwa ni jinai!!!

They should stick to what we have decide...
:rip:CCM...
 
Akikubali kununuliwa maana yake atakuwa amewasaliti watanzania wote wanaotaka mabadiliko ole wake...
 
Asithubutu kufanya hivyo, maana atakuwa pia anahatarisha maisha yake machoni pa washabiki!
People mean business these days bana!
 
Acha mizengwe wewe....si Ze Utamu hii:A S angry:
Aisee mimi sileti habari za kubuni hapa, I'm serious kwamba nimepata habari kutoka kwa mmoja ya watu wanaosubiri matokeo tangu asubuhi nje ya ukumbi. PCCB kama wapo wamkamate Pinda. Kuna vigogo wengine wa CCM mkoani hapa (sitawataja majina), wao pia wapo upande wa mgombea wa CHADEMA, wamemwambia usikubali kuachia kabisa! Kama huamini mtafute mtu yeyote aliyepo Sumbawanga Mjini unayedhani ni mfuatiliaji wa mambo ya siasa umpigie simu kumuuliza
 
hebu tuwekee data hayo mtokeo yakoje kwanza?maana naona maelezo mengi lkn ioni namba
 
wanamuomba mbunge wa chademakivipi wakati wananchi ndio waliofanya maamuzi? wasimame wawaombe wananchi kwamba tuachieni jimbo hili tuongoze sisi.wanataka kuwanyang'anya wananchi haki yao?

wamepewa kuongoza wao waliweka maslahi yao binafsi mbele,hali ya nchi mbaya sasa hivi na wananchi wameamua kuamua kutaabika chini ya uongozi wa ccm au kutafuta mafanikio sehemu nyingine.
 
Sisi ndio tumefanya maamuzi wanamuomba Mbunge wa Chadema ili iweje na huyo pinda asipoangalia naye atapindwa ashikilie la kwake aache kushupalia ya wenzake mbona wanahangika hivyo utafikiri wameambiwa watakufa au ndio mwisho wa maisha pole yao
 
Habari zilizonifikia zinasema kwamba matokeo ya ubunge Sumbawanga mjini yameshakamilika ila CCM imemleta Mizengo Pinda na sasa hivi kuna kikao kinachoendelea cha kumbembeleza mgombea wa CHADEMA asaini form nyingine kuonyesha kwamba ameshindwa. Hadi sasa mgombea huyo hajawakubalia, ila tume ya uchaguzi jimboni humo imesema itatangaza matokeo saa sita usiku, wakati yale ya urais yameshatangazwa tayari. CHADEMA makao makuu mpoo?

Hizi ndio habari za kichochezi. Haiwezekani CCM na CHADEMA wakakaa meza moja kunegotiate kuachiana madaraka in the first place. Acheni kutuletea habari za kizushi!!!

Hapa tunapata data concrete tu na sio kama hizi zinazojaza threads humu JF.!!

Kuna mtu alidai JK yuko Mwanza ila mpaka sasa sijamsikia wala kumuona hapa zaidi ya mabomu acheni hizo jamani hii nchi bado twahitaji amani...
 
Yule mzee Yamsebo wa CHADEMA alikuwa Headmaster wangu, kwa ninavyomfahamu najua hawezi kuwakubalia hawa akina Pinda ambao wanadhani kila jimbo ni haki yao. Akikubali kwa kweli atakuwa hajatutendea haki wananchi tuliompa kura!
 
Habari zilizonifikia zinasema kwamba matokeo ya ubunge Sumbawanga mjini yameshakamilika ila CCM imemleta Mizengo Pinda na sasa hivi kuna kikao kinachoendelea cha kumbembeleza mgombea wa CHADEMA asaini form nyingine kuonyesha kwamba ameshindwa. Hadi sasa mgombea huyo hajawakubalia, ila tume ya uchaguzi jimboni humo imesema itatangaza matokeo saa sita usiku, wakati yale ya urais yameshatangazwa tayari. CHADEMA makao makuu mpoo?

Tuwe wakweli basi, hapa wa Chadema inasemekana kagoma kusaini
 
Hilo haliwezekani ingawaje taarifa nilizonazo mbona CCM imenyakuwa karibu madiwani wote kasoro wawili?

Hizi taarifa ni za kweli kuwa Chadema imelishinda hilo jimbo?
 
wananchi wamemwamini yeye.......asije akawaamini tena ccm........akatae rushwa
 
Back
Top Bottom