CCM: Ruksa kumvaa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Ruksa kumvaa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Feb 18, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280
  VIGOGO wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wenye ubavu wa kumvaa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, wataanza kujulikana Julai Mosi, mwaka huu, takriban siku 23 kabla ya kuvunjwa rasmi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeelezwa wiki hii mjini Dodoma.

  Wagombea hao wa urais watatakiwa kuchukua fomu na kuzirejesha siku saba baadaye, yaani Julai 8 mwaka huu na majina yao yatafikishwa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM, Julai 18, mjini Dodoma, kwa ajili ya uteuzi, ikiwa ni siku mbili baadaye, baada ya mgombea urais wa Zanzibar kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Mteule wa kugombea urais Zanzibar tofauti na urais wa Jamhuri, hutangazwa na NEC ambayo safari hii katika kumpata Rais wa saba wa Zanzibar, itafanya kazi hiyo Julai 16, 2010.

  Katika nafasi za kugombea urais wa Muungano ni Mbunge wa Maswa pekee, John Shibuda ndiye aliyetangaza nia ya kutaka nafasi hiyo na kwa upande wa urais wa Zanzibar, viongozi kadhaa wanatajwa akiwamo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi Shamshi Vuai Nahodha na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud Mohamed.

  [​IMG]

  John Shibuda

  Wengine wanaotajwa kuwania kuongoza Visiwani ni Naibu Waziri Kiongozi, Juma Shamuhuna, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Muungano, Muhammed Seif Khatibu na aliyekuwa Waziri Kiongozi, Dk. Gharib Bilali.

  Kwa upande wa Bunge, litavunjwa rasmi Julai 23, mwaka huu takriban miezi mitano ijayo, mapema zaidi kuliko ilivyokuwa ikifanyika awali.

  Wakati Bunge hilo likivunjwa Julai 23, wabunge wa CCM wenye kutaka kutetea nafasi zao watapaswa kuchukua fomu kwenye chama chao siku tatu baada ya Bunge kuvunjwa, yaani Julai 26 na kulazimika kurejesha fomu hizo siku mbili baadaye, yaani Julai 28.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa saa nane usiku wa kuamkia Jumanne, wiki hii, mjini Dodoma na Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi, Kapteni mstaafu John Chiligati, siku hizo za uchukuaji na urejeshaji fomu kwa wanaotaka kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM zinawahusu pia wagombea wa ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

  Akizungumzia kuhusu madiwani, Chiligati aliwaambia waandishi wa habari kuwa wagombea watachukua fomu Julai 10 na kuzirudisha Julai 14 na kwamba kuanzia Julai 31 hadi Agosti 7, ni siku za wagombea ubunge, uwakilishi-Zanzibar na udiwani kufanya kampeni kwenye matawi ya chama hicho.

  “Watapiga kura za maoni katika matawi yote nchini Agosti 8, kwa wagombea wote wa ubunge, uwakilishi na udiwani.

  Akifafanua kuhusu kura za maoni, alisema NEC imehimiza kila wanachama wa CCM kujiorodhesha kwenye daftari la wanachama katika tawi lake na mwisho wa kujiorodhesha ni Julai 30, mwaka huu na baada ya hapo upokeaji wanachama wapya utasitishwa hadi mchakato wa kura za maoni uhitimishwe.

  “Watakaopiga kura za maoni ni wale tu watakaokuwa wamejiandikisha kwenye daftari katika tawi,” alisema Chiligati na kuongeza kuwa wagombea wote wa ubunge bila kujali nyadhifa zao za sasa watatembezwa wakati wa kuomba ridhaa kwa wanachama kwa kutumia magari ya chama yatakayokodiwa na watakula chakula kilichoandaliwa na chama.

  “Hatutaki mtu ashindwe kugombea au kufanya kampeni za kuomba kura za maoni kwa kuwa hana gari kama mwingine, hana pikipiki au baiskeli. Wote watatumia usafiri wa chama, chakula cha chama na watazunguka pamoja, katika kila tawi ambako kila mmoja atajieleza,” alisema Chiligati.

  Katika hatua nyingine, NEC imekata mzizi wa fitina na hasa malumbano yaliyoanzia katika Umoja wa Wanawake (UWT) wa chama hicho wa kutaka Wabunge wa Viti Maalumu waliokaa kwa mihula zaidi ya miwili kuachia nafasi hizo ama wakagombee kwenye majimbo au wajiengue kabisa kwenye ubunge.

  Katika uamuzi wake wa sasa, NEC imekubali Viti Maalumu iwe na ukomo wa mihula miwili lakini utaratibu huo utaanza rasmi kutumika mwaka 2015, ili wahusika wa sasa wajiandae, ikiwa ni kinyume na alivyotarajia Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba, aliyekuwa akipigania utaratibu huo uanze, katika uchaguzi wa mwaka huu.


  Source: Raimwema
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona hakuna jipya hapo kila mwaka ndo ivyo ivyo wanaruhusu watu wachukue form then wanawaengua baadae bila hata kura....kwani hukumbuki ya Dr. bilali?
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,424
  Likes Received: 26,272
  Trophy Points: 280
  Si Ikulu walishasema maoni ya Sheikh Yahaya yaheshimiwe, kwamba atakaye mpinga JK atakufa ghafla? sasa NEC vipi tena wanaruhusu watu wachukue fomu halafu wafe? kwanini wasizuie vifo visivyo lazima? Usanii wetu bwana! loh!
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  JK anafanya ziara za kutafuta wafadhili wa kumsaidia wakati wa kampeni zake, je hao watakaojitokeza watakuwa wamejipanga kiasi gani, au wanafanya hivyo ili kuwaonesha watu kuwa kunademokrasia ndani ya CCM?
  yangu macho na masikio.
   
 5. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  NEC kuweni makini kidogo jana tumezika watanzania 16 huko Musoma bado hamjaridhika mnataka watanzania wengine wafe kwasababu zinazoweza kuepukika ?.Mnasahau Sheikh Yahaya alishatabiri atakaempinga Kikwete ndani ya CCM atakufa.Ebu kuweni makini kidogo mmeshindwa kuwafukuza Chenge,Lowassa & Co kwa ufisadi mnataka watanzania wafe kwa uzembe,nasema safari hii hakuna wa kumpata nilikuwa kwenye mkakati wa kuchukua fomu lakini utabiri wa sheikh Yahaya umenikimbiza kabisa.

  Kazi ipo siku Sheikh Yahaya atakaposema asiempigia kura Kikwete atakufa>
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...