CCM, punje ya ngano isipoanguka katika udongo ikafa; hukaa hali ileile?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
943
1,000
Hii ni kanuni ya asili ya mbegu, haijarishi unaipenda au pengine hupendi hata kuisikia, lolote kati ya mawili haya linaloendana na utashi wako halitobadili chochote hapo!

Ili mbegu ya mmea wa aina yoyote ile ijizae upya ni lazima kwanza ife; ndipo itaweza kuota tena kama mche mchanga unaoweza kuanza maisha ya uzazi upya!
Naam pasipo mambo kuwa hivyo, hali ya mbegu huendelea kubaki vilevile!
Ni muda mrefu sasa shauku chama cha mapinduzi kwa namna furani imekuwa kutafuta namna ya kujizaa upya bila ya mafanikio yaliyotarajiwa kutimia!

Mimi sitokaa nisahau, ingawa kitambo sasa, tangazo lao la kujivua gamba jinsi lilivyokitikisa chama hiki kikongwe barani afrika!
Sote tunafahamu kuwa dhamira ya viongozi wa chama ilikuwa njema tu ingawa mara zote tatizo hubaki kuwa ni gharama ya kufanya hivyo!

Hebu tujiulize swali hili fikirishi kuwa; tatizo lao ni lipi?

Hawa jamaaa muda wote, kadri jua liendavyo mawio na kuyarudia machweo yake endapo hawatakubali kuiishi kanuni ya mbegu kamwe wasitegemee mabadiriko ya aina yoyote, wakati wowote!

Tabu ya iko hapa tu!

CCM hii inataka mabadiriko bila maumivu!
Wanataka kuzaa bila utungu!
Wanataka kupata bila kupoteza!

Wamefanana na punje ya ngano inayotaka kubadirika kuwa mche ilihali haitaki kuoza na kuharibika uchakavu wake!

Kanuni ya asili inawaambia leo kuwa haiwezekani, na wala haitawezekana kujizaa upya bila ya kale kuharibika kwanza!

Viongozi wa kale kuharibika na kupotea kabisa!
Maslahi ya kale kusambaratika kabisa!
Mipango ya urais ya kale kufutika kabisa!
Mitandao ya kale kusahaulika kabisa!

Ili kuruhusu CCM mpya kuchipuka upya kabisa!
Ili kuruhusu sura mpya kabisa!
Mawazo mapya kabisa!
Uungwaji mkono mpya kabisa!
Katika ushindi mpya, usio wa kimagumashi kabisa!

Kubarini tu ili wale wazamani wafe kama mbegu na kuruhusu wapya wachipuke kama mche!

Hii si langu bali ni kanuni za asili tu!

Sasa kama kuna yeyote aliyekomaa kiubishi hata kufikia kupingana na kanuni za asili anakaribibwa azibeze!
 

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,482
2,000
Mtoa mada jifunze kuhusu hydroponics inawezekana kabisa mawazo yako ni sahihi lakini yakawa yamelalia katika theory za zamani technologia inaweza ikakujuza vitu tofauti na unavyoamini vya asili na kuaapa haviwezekani. Mfano wako kuhusu ngano tazama technologia zinavyokujuza kwamba mmea mche mchanga unaweza kuanza maisha mapya bila kupitia huu mchakato.

Usiwalazimishe CCM wapiti njia unazoita za asili kwenda hatua nyingine, kufanikiwa kwa chama cha siasa ni pamoja na kushika dola kitu ambacho CCM hawajapoteza na mengine ni kurukaruka kwa maharage tu. Kanuni za asili ndio ulikuwa mwisho wa kufikiri kwa watu hao sasa hata kahawa wenzio wanazalisha miche bila ya kutumia mbegu, miti ya matunda we mwenyewe ni shahidi yanapita denge kwa grafting na budding zote hizi hazipo kwenye hizo kanuni za asili.

Katika siasa budding ni kama Kenya watu wameweza na Tanzania japo vyama vimebadili magear angani lakini bado wanachechemea na mabadiliko ya tabia nchi yanalazimisha kanuni za asili zisiwe ndio njia pekee.
 

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
943
1,000
Ndiyo nakubaliana na wewe kuwa huko maabara waweza kutotumia udongo kabisa, lakini hata hivyo hutatuongopea kuwa ile punje ya awali itadumu pamoja na mmea mpya! Katu hilo haliwezekani.
Ni lazima punje ya mbegu ife ili kuruhusu mche mpya kuendelea iwe ni maabara au kwenye udongo hiyo haijalishi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom