CCM, Polisi yafukuza Wageni kwa nguvu Gesti Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, Polisi yafukuza Wageni kwa nguvu Gesti Dodoma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Malafyale, Jul 10, 2010.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Gazeti la habari leoiImeandikwa na Ikunda Erick, Dodoma; Tarehe: 9th July 2010

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Polisi wanawahamisha wapangaji kwa nguvu kwenye nyumba za kulala wageni, kwa walichokiita ni kupisha wajumbe na Mkutano Mkuu wa chama hicho.

  Tafrani hiyo imeanza leo katika baadhi ya nyumba za kulala wageni , mwandishi wa habari hizi ameshuhudia vitendo hivyo.

  Katika nyumba ya Dallas, HABARILEO ilishuhudia wapangaji waliokuwa hapo kwa takribani wiki moja, wakirudishiwa fedha zao za pango kwa siku zilizosalia na kutakiwa kuondoka.

  “Tumekaa kwa wiki na nusu hivi, na tulikuwa tukae hadi Bunge livunjwe, lakini leo tumefukuzwa, viongozi wa CCM wamekuja na polisi na kutaka wapangaji tuondoke,” alisema mmoja wao.

  Mwandishi wa habari wa StarTv, Tom Chilala, ni miongoni mwa waliokumbwa na hatua hiyo, na alisema yeye na wenzake walikuwa wanatafuta mahali pengine.

  Sekeseke hilo pia liliwakumba wapangaji kwenye nyumba ya Capricorn ambapo wateja waliokuwa wamepanga takriban wiki au zaidi nao walitimuliwa.

  Hata hivyo, baadhi ya wapangaji waligoma kuondoka kwenye nyumba hiyo, huku wakichukua funguo za vyumba vyaona kuondoka nazo.

  Baadhi ya wapangaji walioondoka na funguo walisema hawawezi kuondoka kwani nao ni binadamu na wanalipa fedha.

  Hata hivyo, inasemekana mameneja wa nyumba hizo ambao walionesha kusita kuwatoa wapangaji, walipewa vitisho na baadhi yao kuwekwa rumande, kama njia ya kuwatisha.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba baadhi ya nyumba za kulala ziliandikiwa barua na CCM kuwataarifu kuhusu kuwekewa nafasi.

  Kwenye nyumba ya Kilamia, wahudumu walisema hawakusaini mkataba na CCM, ila juzi walifika usiku wakitakavyumba vya watu tisa.

  “Sisi tuliwaambia vyumba vimejaa, nao wakasema ni lazima wapangaji waondoke, ila tuliwagomea tukawaambia wapangaji wapo hadi Bunge livunjwe, hatuwezi kuwatoa,” alisema mmoja wa wahudumu.

  Aliongeza alipowajibu hivyo waliondoka na kusema watarudi jioni na polisi kuwatoa kwa nguvu, kwa maana wanachama wa CCM wamekuja kwenye mkutano wa chama, hivyo wanahitaji malazi.

  Wingi wa watu unatokana na Mkutano Mkuu wa chama hicho unaofanyika leo na kesho.

  Mkutano huo una takribani wajumbe zaidi ya 2,000 kutoka mikoa yote nchini.

  My take;Habari hii imenisikitisha sana,sikujua kuwa TZ tumefikia hatua hii ya uvunjaji wa haki za binadamu;mungu tuhurumie!
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hilo ndio tabaka tawala linavyo-operate kwa staili ya mafioso. True mobsters and ring leadership..nothing less. Sasa still kuna watu eti wana matumaini ya kushindana nao kwene uchaguzi wa wazi na haki Oktoba.?? Stop being delusional people..!
   
 3. m

  matejoo Member

  #3
  Jul 10, 2010
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari hii imeandikwa kama kiini macho kujaribu kuondoa attention ya watu wasi dadisi mambo ya muhimu zaidi kama rushwa, mizengwe etc. Don't take it at first value my friend!! Tangu lini HabariLeo ikaandika "habari"? kama hii??
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Skeptical too.
  Habari Leo!!!
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Jul 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  daaaah niseme nini, ninyamaze, ama kama alivyosema mkuu hapo juu, wanajaribu kuhamisha umakini wa watu kuelekea Rushwa, uvunjaji wa taratibu, uonevu na siasa zao kule kwenye mkutano wa tabaka la wafilisi Dodoma
   
 6. tikotiko

  tikotiko Member

  #6
  Jul 10, 2010
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hii ndiyo CCM ambayo wannchi watairejesha tena madarakani KWA KISHINDO and then wanaishi maisha magumu kwa kishindo pia!! WAF!!
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Hapo sasa! Kumbe na wewe umeshitukia dili eeh?
   
 8. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii inaweza kuwa kweli....kwasababu leo wakati naangalia mkutano hapa nimeona mwenyekiti wa maandalizi ya huu mkutano wa CCM akisema kuwa imebidi wawaondoe baadhi ya watu ambao walichukua nafasi za wageni wa CCM.
   
 9. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Very shameful!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :sick:
   
 11. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Narudia tena na tena kuwa, polisi ni mbwa wa ccm... hii aliwahi kuisema Rev Chris Mtikila na sasa sote ni mashahidi. Inasikitisha sana kuona jeshi la polisi linatumiwa kwenda kuvunja haki za binadamu kisa mkutano wa ccm, shame on this and one day you will pay for it!!

  Cha ajabu hao hao waliotolewa ndo watakao wapigia tena kura ili kuwarudisha madarakani hiyo Oktoba 2010, nasema tena shida tunazopata sasa watanzania ni halali yetu acha tuendelee kutaabika kwani tunastahili, na kwahili Mwenyezi Mungu hahusiki.
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa nini wasiinue uchumi na kuleta ahueni ya maisha kwa njia hizo??? Hivi hili jeshi la Polisi ni la CCM??? nabado utasikia hapo hapo Dom yanapotokea mambo kama haya wataichagua CCM.....TUBADILIKE jamani?? Hii habari imeniharibia siku kabisa.....I need a fresh air.....
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Polisi wenyewe wanakwenda kwa highest bidder unategemea nini? Polisi yenyewe imeoza kabisa, a perfect mafioso's accomplice.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,871
  Likes Received: 83,348
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa Dodoma kikazi miaka ya nyuma. Guest House niliyofikia ilikuwa ni mojawapo ya nyumba za wageni mbali mbali Dodoma ambazo zilipata barua za kuwataka wenye nyumba hizo za wageni kuwaondoa wageni wote ili kuwapisha wahudhuruaji wa mkutano mkuu wa chama. Bahati nzuri mimi na mwenzangu hiyo siku ya mwisho ndiyo ilikuwa siku yetu ya mwisho kuwepo Dom, lakini kulikuwepo pia colleagues wengi tu ambao wengine ndiyo kwanza walikuwa wamefika kuja kufanya kazi zao.
  Walitukana matusi yote wanayoyajua duniani kuilaani CCM na viongozi wake lakini hawakuwa na jinsi ilibidi tu wafungashe virago ili kuwapisha waheshimiwa.

  CCM imeshika utamu haiheshimu wala kuwaogopa Watanzania itafanya chochote kile hata kama kutumia mabavu ya vyombo vya dola kutimiza lile walitakalo. Hali hii inaudhi sana lakini ndiyo hakuna jinsi maana CCM itatawala Tanzania milele.
   
Loading...