CCM, Polisi na Serikali wasijidanganye, wafikiri kabala ya Kutenda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, Polisi na Serikali wasijidanganye, wafikiri kabala ya Kutenda.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, May 10, 2012.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wana JF,

  Kuna tabia kwa sasa imeibuka ya watendaji serikalini na Wana CCM ya Kufunga macho na kufanya mambo bila kufikiria hasa Jeshi la polisi.

  Mfano wa Matukio yaliyotokea siku za karibuni wabunge wa Majimbo mawili kukatwa mapanga na wafuasi wa CCM kule mwanza ili kutisha wapiga kura na kutengeneza mazingira ya kuiba kura za CDM... na tukio la kumchinja Mwenyekiti wa CDM USA kule Arumeru na matukio ya kuwa teka watu kule Igunga yanasikitisha sana na ni sababu tosha kabisa kwa WaTZ kuichukia CCM Serikali yake pamoja na Jeshi la Polisi.

  Just imagine watu wanauawa hakuna hatua zinazochukuliwa na jeshi la polisi na kibaya zaidi, hadi watu waandamane ndiyo jeshi la polisi linakumbuka kuwa saka watuhumiwa.

  Ila ikitokea mtu katoa maneno fulani juu ya CCM na viongozi wao anapelekwa Cello Ijumaa ilimradi asipate dhamana ili tu akae ndani the whole weekead.
  Hata hivyo kuna tetesi kuwa Nasari watamtia nguvuni over this comming weeked ili wampeleke sello lakini wajue ipo siku viongozi wote wa CDM pamoja na wananchi watadai kwenda selo then sijui watafanya nini.

  Muda wa kuwatishia WaTZ umepita tunachotaka ni haki itendeke, pale ambapo kiongozi ametoa matamshi na kakiri kuwa alikosea asamehewe ila si kueegemea upande mmoja.

  Mfano tuna mawaziri sita waliotafuna mabilions of money hadi leo hii wengine wapo kwenye Vx wanakula viyoyozi hakuna hata mmoja aliyeguswa..
  Watu wameweka rehani maisha ya watanzania kwa kuingiza bidhaa zisizokaguliwa n hakuna action iliyochukuliwa, watu wameingiza mafuta feki, mavyakula feki na bado wapo tu hawguswi lakini Nasari aliyetamka kutomtambua JK anasumbulia as if kaua mtu, wapo waliowadhuru kina mwakyembe, mwandosiya etc wapo wankula kuku na kusherekea na wanaendelea kuwaweka kwenye target wengine wengi...

  Tuache Mzaha TZ ni yetu wote hakuna mwenye haki miliki ya hii nchi.
   
Loading...