CCM Poleni. Hili la uandikishaji wapiga kura ni KANSA mliyoitengeneza wenyewe

Kwa kazi nzuri inayofanywa uende kuchagua nini? Acha CCM insonge mbele kwa utendaji mzuri. Tutachagua wakikosea.
 
Watakaojiandikisha ndio watakao piga kura.
Hata mjinga analijua hilo. Lakini ufahamu wananchi wenye akili, pamoja na kulijua hilo, wameamua walichoamua.

Ni wakati mzuri kwa CCM kutangaza kuwa nchi nzima wagombea wa CCM wameshinda. Na CCM wafanye sherehe nchi nzima kufurahia ushindi wa kishindo.

Wakitaka watangaze pia Rais aliyepo ameshinda kwa 1010% kwa uchaguzi ambao ungefanyika mwakani.
 
Rais alikwishawaita watendaji wote wa kata nchi nzima kuwapa maelekezo, maelekezo hayo hayakuhusisha namna ya kutangaza pale watu wote watakapokuwa wameamua kusaidia ushindi wa chama chetu kwa kuamua kutojiandikisha?
 
Jana nimeenda kujiandikisha, watu wanaendelea tu na mambo yao...
Muandishi akaniuliza "utakuja kupiga kura kweli?"
Nikajibu, kujiandikisha ni haki yangu pamoja na kupiga kura pia, ila inategemea mazingira....
 
Kumbe kaka Kuna wakati huwa unaandika Ujumbe mrefu?
Jana nimeenda kujiandikisha, watu wanaendelea tu na mambo yao...
Muandishi akaniuliza "utakuja kupiga kura kweli?"
Nikajibu, kujiandikisha ni haki yangu pamoja na kupiga kura pia, ila inategemea mazingira....
 
Huu ni upumbavu uliopitiliza. Watu kutojiandikisha mnamlaumu mtu na kushinda kwenye mitandao.
Wakati hata ulaya na marekani mnapofikiri demokrasia imekuwa wanapita Nyumba Kwa Nyumba kuomba watu wajiandikishe.
Na siku ya kupiga kura volunteers wanaenda Nyumba Kwa Nyumba kupeleka watu vituoni.

Ninyi wapinzani mabwege pelekeni ujinga nyumbani.
Kwanini unateseka wakati ni fursa kwenu kupita Bila kutumia nguvu Wala kuua akina akwilina wengine?

Mbona Mmepita Bila kupingwa majimbo mengi Sana Na mnaongoza fresh tu Na Uchumi unakua!!!

Acheni uoga
 
Huu ni upumbavu uliopitiliza. Watu kutojiandikisha mnamlaumu mtu na kushinda kwenye mitandao.
Wakati hata ulaya na marekani mnapofikiri demokrasia imekuwa wanapita Nyumba Kwa Nyumba kuomba watu wajiandikishe.
Na siku ya kupiga kura volunteers wanaenda Nyumba Kwa Nyumba kupeleka watu vituoni.

Ninyi wapinzani mabwege pelekeni ujinga nyumbani.
Mabwege ni familia yako, wazaa bwege
 
Shindeni ata gadaffi alishinda hivyo hivyo.Yaani wewe unawazuhia wenzeko kuingia darasani kuchukua notes then unataka ushindane nao kwenye mitihani? PUMBAVU
🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️
 
Watu wa kusifu ni wabunifu sana,usishangae wakaja na kubwagizo kwamba watu wameona haina haja ya kujiandikisha kwakuwa awamu ya tano inachapa sana kazi.
 
Habarini Wadau,

Ninasema wazi kabisa ninachokishuhudia katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, yaani Wenyeviti wa Kijiji, wenyeviti wa Kitongoji na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya vijiji.

Kwakweli katika Wilaya nyingi wananchi HAWAJIANDIKISHI KABISA, kwa anayebisha apite katika vitongoji karibu vyote, Wananchi hawataki kujiandikisha.

SABABU WANAZOTOA :- Wengi wa wananchi wanalalamika kwa kubanwa kwa wagombea wao wa vyama vya upinzani ambao walikuwa tayari kuwachagua.

Unakutana na wananchi wanakuambia wazi kabisa ''Sina muda mchafu'' wa kujiandikisha na kupiga kura kwasababu watakaoshinda kwa hila na nguvu wanajulikana.

Nailaumu CCM, hususan Mwenyekiti wao aliyewanyima wapinzani haki yao ya kujieleza kwa Wananchi wao.

Sasa naona wanaoweweseka sana ni haohao viongozi wa CCM, kwa kulaumu mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuwa ndio hawajafanya uhamasishaji kwa wananchi ili wajiandikishe.

Mh. Suleiman Jaffo, Waziri wa Nchi O.R TAMISEMI amewashitaki kwa Rais wasimamizi wote wa mikoa hii ya Kaskazini kwamba uandikishaji ni hafifu Mnoo kwakuwa hawajahamasisha. Haijatosha ametoa agizo kuwa sasa ni lazima wananchi waandikishwe kwa zaidi ya 50%

Kingine tena, Leo wasimamizi wameagiza tena waandikishaji wapite nyumba kwa nyumba kuandikisha.

Waandikishaji nao wanagoma kwenda mpaka walipwe kwasababu sehemu nyingi zipo remoted na mbali...na pia ni kazi ngumu kwakuwa mwanzoni walikubaliana kukaa katika vituo rasmi vya kuandikishia.

SWALI LA MSINGI : Kwanini mnalazimisha watu kujiandikisha?

Hata sehemu isiyo na Upinzani kabisa kama Same na tambarare ya Mwanga ambapo CCM inatawala siku zote pia wananchi wengine hawajiandikishi.

TATIZO NI NINI?

Siku zote ''Mshahara wa Dhambi ni Mauti''

Haya ni Mauti kwa upande wa kaskazini.
Ukweli ni kuwa wameona hakuna haja ya Uchaguzi sabbu serikali iliyopo inafanya kazi ile waliyo kuwa wakiitaka pale ambapo wanaona kuna umuhimu wa kufanya mabadiriko bila shaka utawaona wakiwa wamejiandikisha kwa idadi kubwa.
Na hili lina akisi kile kitakachotokea 2020..

NINATABIRI 2020 MH, RAIS JPM ATAPITA BILA KUPINGWA...!!

sbbu katika hali halisi hakuna mpinzani atakayesimama kwa Nafasi ya Urais.
Lets wait and see.
 
Wenyewe walishatangaza kuwa mitaa yote ni mali ya ccm. Leo wanahimiza watu eti wajiandikishe kushiriki uchanguzi; uchaguzi wa kuchagua nini?
 
Huu ni upumbavu uliopitiliza. Watu kutojiandikisha mnamlaumu mtu na kushinda kwenye mitandao.
Wakati hata ulaya na marekani mnapofikiri demokrasia imekuwa wanapita Nyumba Kwa Nyumba kuomba watu wajiandikishe.
Na siku ya kupiga kura volunteers wanaenda Nyumba Kwa Nyumba kupeleka watu vituoni.

Ninyi wapinzani mabwege pelekeni ujinga nyumbani.
Acha upimbi wewe Marekani au Ulaya hawahamasishi nyumba kwa nyumba au kuwapeleka watu wakapige kura. Hiyo kitu hakipo.
 
Back
Top Bottom