CCM, picha za umwagaji damu Uchaguzi 2020 zinazosambazwa mitandaoni na wanachama wenu kupongeza waliomwaga damu, si dalili njema

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tuna vyombo vya dola na chama dola, wenzenu kuanzia jana wanatoa makovu yaliyotokana na uchaguzi wa mwaka jana. Zipo tuhuma za kupigwa Risasi kukatwakatwa na kulazimishwa kwa watu kurejea CCM na walipokataa walimwagwa damu.

Wakati Taarifa hizi zikisambaa kwa kasi zikiwa na majina na maelezo toshelezi ya waliotendewa unyama huo, wapo viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kupitia real accounts zao wanashabikia na kufikia mahali kusema wafe kabisa. Wapo wanaosema walioumizwa na dola walifanya vurugu bila kuonyesha vurugu hizo na wengine kufikia mbali zaidi kusikitika kwanini walioumizwa hawakufa.

Posts hizi zinaandikwa Twitter, Instagram na FB na watu ambao yulitegemea hata kama wanafurahia damu kumwagika basi wasifike mahali wakaandika hisia zao hadharani. Lakini pia hakuna mtu ayekamatwa watu kiongozi aliyejitokeza kuwakanya wanaoshabikia umwagaji damu. Ukimya wa Viongozi una tafsiri mbaya sana miyoyoni mwa watu, wapo walioumizwa ambao mama zao ni CCM, wake au waume zao ni CCM na may be watoto wao wanapoona wanachama na Viongozi wao wanashangilia ndugu zao kuumizwa tusitegemee kama chama kitasonga mbele, kitatawaliwa na wasaliti.

Hizi picha ni mbaya sana kwa jamii yenye dini. Lakini pia kibaya zaidi hata Viongozi wa dini haya hawakemei kwa maana kwamba viongozi wengi wa dini wanaona uovu lakini kwasababu awajawahi kumwona Mungu wanayemwamini na wamewaona wanadamu wakiwemo watu wkatili kama hawa wamwaga damu basi wao wamejitolea kuogopa wamwaga damu bila kujua wanaomwaga damu ni waumini wao na waliomwagwa damu ni waumini wao. Kama hatuwezi kumtukuza Mungu hadharani tukaogopa wanadamu taifalitaingia vitani au machafuko.
 
Huu niunafiki wa hali ya juuu mtoa post unatakiwa ushitakiwe kwa kuzua taharuki hakuna kitu kama hicho mitandaoni weka picha hizo tuone kama kweli wewe ni kidume kama huweki we ni mhuni tu
 
huu niunafiki wa hali ya juuu mtoa post unatakiwa ushitakiwe kwa kuzua taharuki hakuna kitu kama hicho mitandaoni weka picha hizo tuone kama kweli wewe ni kidume kama huweki we ni mhuni tu
Anakiri dhambi kiaina.

lakini pia anataka kuwakumbusha wanaccm wenzao kile walichofanya wasijikaushe
 
ili tukuamini weka picha siumeziona kwenye mitandao weka kama huweki wqewe ni muongo na unania mbaya na nchi yetu yenye amani nchi ya asali na maziwa
 
CCM watakua na mwisho mbaya sana

IMG_20210923_171514.jpg

IMG_20210923_180327.jpg
 
Mtoa mada hizo stori zako za vijiweni peleka kwa watu wa kijiweni wenzako tuambie ni nani aliyeteswa na aliteswa na nani aliteswaje maana neno kuteswa lina maana pana tutajie pia waliteswa wakiwa wapi nani mtesaji pia aliwatesa tarehe ngapi mwezi wa ngapi.
 
Ukweli UNAUMA kunywa Sumu sepa
 
Tuna vyombo vya dola na chama dola, wenzenu kuanzia jana wanatoa makovu yaliyotokana na uchaguzi wa mwaka jana. Zipo tuhuma za kupigwa Risasi kukatwakatwa na kulazimishwa kwa watu kurejea CCM na walipokataa walimwagwa damu.

Wakati Taarifa hizi zikisambaa kwa kasi zikiwa na majina na maelezo toshelezi ya waliotendewa unyama huo, wapo viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kupitia real accounts zao wanashabikia na kufikia mahali kusema wafe kabisa. Wapo wanaosema walioumizwa na dola walifanya vurugu bila kuonyesha vurugu hizo na wengine kufikia mbali zaidi kusikitika kwanini walioumizwa hawakufa.

Posts hizi zinaandikwa Twitter, Instagram na FB na watu ambao yulitegemea hata kama wanafurahia damu kumwagika basi wasifike mahali wakaandika hisia zao hadharani. Lakini pia hakuna mtu ayekamatwa watu kiongozi aliyejitokeza kuwakanya wanaoshabikia umwagaji damu. Ukimya wa Viongozi una tafsiri mbaya sana miyoyoni mwa watu, wapo walioumizwa ambao mama zao ni CCM, wake au waume zao ni CCM na may be watoto wao wanapoona wanachama na Viongozi wao wanashangilia ndugu zao kuumizwa tusitegemee kama chama kitasonga mbele, kitatawaliwa na wasaliti.

Hizi picha ni mbaya sana kwa jamii yenye dini. Lakini pia kibaya zaidi hata Viongozi wa dini haya hawakemei kwa maana kwamba viongozi wengi wa dini wanaona uovu lakini kwasababu awajawahi kumwona Mungu wanayemwamini na wamewaona wanadamu wakiwemo watu wkatili kama hawa wamwaga damu basi wao wamejitolea kuogopa wamwaga damu bila kujua wanaomwaga damu ni waumini wao na waliomwagwa damu ni waumini wao. Kama hatuwezi kumtukuza Mungu hadharani tukaogopa wanadamu taifalitaingia vitani au machafuko.
Ukishajua unaongoza watu wa aina gani,ni rahisi Kuwaitreat accordingly.. Watz hatujitambui
 
ili tukuamini weka picha siumeziona kwenye mitandao weka kama huweki wqewe ni muongo na unania mbaya na nchi yetu yenye amani nchi ya asali na maziwa
Kama asali na maziwa ndiyo haya basi hata kwenda mbinguni hakuna haja maana matumaini ya asali kwa wafuasi wa ccm pekee siyo matunda ya amani ,umoja,mshikamano na upendo.
 
HIVI NI NCHI GANI WATU WANATAMANI KUISHI KAMA SIYO TANZANIA KATIKA UKANDA HUU WA AFRICA ? ACHENI KUZUSHA TAHARUKI BADI NI CHI NZURI NA SALAMA SANA HII
Tembea uone wewe fara kama hujaenda hata Uganda utajuaje kuwa kuna watu wana furaha na maisha kuliko Tanzania??? Nchi pekee inayoweza kutamani maisha ya Tanzania kati ya hizi tulizopakana ni Burundi kwa vile na wao ni mafara kama sisi.
 
Back
Top Bottom