Ni ukweli usiyofichika kuwa kwa sasa Watumishi wa Umma hawafuraha na kazi zao. Kwani masuala mengi yamejitokeza ambayo kwa njia moja au nyingine yanasababisha Watumishi wa Umma kuwa na maisha ngumu na kupunguza mishahara yao huku ukali wa maisha ukiwa palepale (15% kodi ya Bodi ya Mikopo). Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne Watumishi wa Umma waliona mwanga kwa kuwa mishahara yao ilikuwa inafanyiwa Mapitio kila mwisho wa mwaka wa fedha.
Hali hii ni tofauti kabisa na utawala wa Awamu ya Nne. Watumishi wameshuhudia kwa miaka miwili mfululizo mishahara yao ikiwa ile ile. Kwa sababu moja au nyingine hali hii imehadhili utendaji kazi wa Watumishi Wengi wa Umma ( Baadhi yao wanashindwa kuacha kazi kwa sababu tu ndiyo maisha waliochangua na ni vigumu kuanza maisha mapya).
Aidha, Kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yanawaadhili zaidi Watumishi wa Umma wanaofanya kazi Serikali Kuu na Serikali za mitaa (Ambao ndiyo wengi) na wamekuwa wakilipwa mishahara midogo kwa kiwango cha TGS. Huku ikiwaacha watumishi wanaofanya kazi katika Taasisi za Serikali wakipata maumivu madogo kwa kuwa mishahara yao ni mikubwa (Kiwango cha Taasisi).
Hali iliyofikia sasa ni ukweli usiyofichika kuwa juhudi za makusudi zinatakiwa kufanyika ili kuokoa maisha wa Watumishi wa Umma. Kwani tumeshuhudia Vyama vya Wafanyakazi vikiwa kimya na kuacha kupigania maslahi ya watumishi wa Umma badala yake wanapigania matumbo yao.
Kutokana na hili, Tunaiomba CCM (Chama Tawala ambayo ndiyo waajiri wakuu wa Watumishi wa Umma) fatilieni na kuchukua hatua za makusudi ya kuokoa jahazi la Watumishi wa Umma waliowengi ambao kwa sasa wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Vilevile, Wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya kazi za utumishi wa Umma (Zaidi ya Masaa 12).