CCM Ombeni Vyama vya Upinzani Viungane ili viwasaidie kuwakumbusha kuliko kuvifuta mkaja kuondolewa kwa Mawe

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JJ

Nimemsikiliza sana Bashiru akihubili kufuta kabisa vyama vingi, bila kukumbuka kuwa havikuanza kwa bahati mbaya, vipo kikatiba. Huyu mwenyewe alitoka huko huko CUF, sijui kwa nini wanapopata madaraka wanakuwa wepesi hivi kujisahau, Yeye Kitilya, Shonza, bila kupitia kwenye moto wa kunolewa na upinzani wasingekuwa huko, kuna huyu dogo Katambi, sasa hivi kashaota kitambi naye ameanza kutoa shutuma za ovyo kama kwamba kuna mtu alikuwa anamjua huko aliko.

CCM ukiweza kupambana na Ufisadi, magonjwa, Njaa ya pesa , Elimu bora, upinzani unaweza kuondoka wenyewe, humo mliko, mnapingana wenyewe kwa wenyewe mnanyamazishana kwa vitisho sio kwa hoja za nguvu, angalia, mmewatisha wale mawaziri wakuu waliokuwa wamejilimbikizia mali wakaja maskini kwa upole, sasa najua mtawatumia kwenye kampaini.

CCM mnapendwa sana tena mno, basi wekeni Tume huru na katiba mpya tuangalie Je, mnapendwa, mkae mkijua kelele za kuwasingizia mabeberu kuwa mnaingiliwa alafu kesho mnazua tambo kuwa wanawaoneo wivu kwa kuwa tuna amani!! Tanzania hakuna Amani bali kuna utulivu wa muda, kungekuwepo Amani watu wasingekuwa wanapotea au kutekwa na wasiojulika.. Dr. Bashiru, badala ya kupambana kuondoa upinzani pambana kuondoa umaskini uliotukuka, walipa kodi wanakamliwa sana na kodi ambazo hazina mpagilia wewe unalilia Tanzania ya Viwanda.

hayo material unayonunua nje na kodi kibao uzalishaji ukitokea watumiaji wataweza hizo bei, au ndio yale yale ya kufungua viwanda vingi ambavyo vinaishi miaka mitatu.

Dr. bashru wewe ni msomi unayetegemewa, usilete ushauri wa mazoea ambayo umeyakuta CCM, bali toa maona sahihi ya kutuondoa kwenye ushindani wa kiitikadi, kwa mbinumpya za siasa ya sayansi na uchumi. Ukiendekeza maneno kama ya PolePole utakuwa unapoteza sifa kama yule aliyetolewa Jalalani, leo akiongea hivi kesho anasema hakuwa yeye.
 
Kufuta upinzani ni kazi ngumu sana,Kwa sababu hata wanaokula nao ni wapinzani wao namba moja,ngoja meza igeuke ndio watajionea wenyewe
 
Na siku watajaribu kufanya hivyo hichi chama chao wataanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe kwa kugombania madaraka
 
Nguvu wanayotumia kupambana na upinzani ingeelekezwa kwenye kulikomboa Taifa na kulipeleka kwenye maendeleo chanya ya Watanzania, wallah sisi tungekuwa Donor kantry.
 
viongozi wetu huku CCM ni mbumbumbu tu.

wanashindwa kutambua kiurahisi kabisa kuwa wapinzani wa wazi (overt opposition) wakizuiliwa badala yake wataibuka wapinzani dizaini ya Bokoharam (covert opposition).

na hawa coverts hawanaga mswalie mtume.... wanachinja kila aliye mbele yao.

viongozi CCM zingatieni angalizo hili mtaipeleka nchi yetu kusiko!!
 
Back
Top Bottom