bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,668
Kwanza nianze kutoa maelezo kidogo, wanajukwaa bila kujali itikadi za vyama naomba tuelewane kwa hili nimeonekana kuitumia CCM kuwakilisha sura ya siasa ubunge maana ndiyo wanachukua nafasi kubwa.
CCM Oktoba 2020 tunaomba Ubunge ubaki kuwa nafasi za UONGOZI si AJIRA. Kwanza kabisa naomba kutoa ombi langu kwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mh. ndugu John Joseph Pombe Magufuli ambaye pia rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania . Ombi langu pia limfikie Katibu mkuu wa CCM ndg. Bashiru Ally nawaomba chondechonde mkipata huu ujumbe ufanyieni kazi tafadhali.
Sasa naomba kuelezea dhana ya kubadili Ubunge/uwakilishi ubaki kuwa uongozi na si ajira, kwa mtanzania makini anayewajibika na mzalendo ataungana na mimi katika kushuhudia khali ya bunge letu la Jamuhuri ya Muungano katika utendaji wake wa kazi. Ni wazi tukifanya utafiti wa utendaji kazi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano nasema hakika iwapo utafiti utakuwa huru na kuzingatia uhalisia bunge letu litapata si zaidi ya 20% katika kutimiza majukumu yake hasa ya uwakilishi wa wananchi. Najua hili linaweza kuwakera wabunge ila ukweli lazima usemwe tu hakuna namna nyingine.
Ni wazi kwamba ibara ya 4 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano inaelezea vyema juu ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu ya serikali ambayo ni serikali kuu, mahakama na bunge. Ugomvi wangu upo katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano naweza kurudia hizi kauli zisizopendwa kuwa bunge letu tukiliweka katika mizania ya uwajibikaji linaonekana kuwa na udhaifu/mapungufu katika dhima nzima ya uwajibikaji katikati kusimamiana hii mihimili mikuu, na binafsi naguswa kwasababu ni mhimili huu wa Bunge upo upande wa wananchi (nikiwemo mimi). Kwa miaka mingi dhana ya uwakilishi wa huu mhimili imepuuzwa sana, sababu kuu ni moja kwamba UBUNGE UMEKUWA AJIRA badala ya UONGOZI/UWAKILISHI.
Viongozi wangu wapendwa CCM ninawataja kuwakilisha viongozi wengine vyama vya siasa ambavyo vinauwezo wa kutoa au kupata wabunge wote wa kuchaguliwa na kuteuliwa ebu angalieni hili kwa umakini mkubwa licha kuwa lina ugumu wake kwasababu ya mazoea yetu kuwapata wagombea au wateuliwa kwa kuzingatia umaarufu, ukwasi, urafiki, undugu, umaarufu wa koo zao, ushikaji na ukabila hivi vitu ndivyo vimetufikisha hapa kuona bunge lisilo wajibika kwa wanachi(bunge kupoteza legitimacy ya uwakilishi).
Naomba kutoa mapendekezo ya namna ya kuwapata wagombea wa ubunge/uwakilishi wa wananchi.
Kwanza ruhusu michakato iwe wazi, kwa kuanza mapema mchato hili litatoa muda mzuri wa kuchakata wagombea bila kukimbizana na muda. Hivyo wacha watu watoe hoja na kujinadi huku mkichuja matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ofisi na udharimu wa namna yeyote.
Pili kuwepo na utaratibu wa wagombea kuandaa ILANI binafsi za wagombea hizi zitasaidia kuwajua kwa undani wagombea na uwezo wao wa kiuongozi na pia mtapata mawazo mbadala na kukidhi ILANI KUU YA CHAMA.
Tatu wagombea wote wapate fursa sawa kusikilizwa namna wanavyojua yale waliyoweka kwenye ILANI ZAO hapa mtawaumbua walioandikiwa hizo ILANI pia mtajua na kutambua kuwa uongozi na ajira ni vitu viwili tofauti.
Nne, chukua fursa ya kupata vingozi vyama na serikali kwa badae maana ni uhakika kuwa si wote watapata uongozi wapo wazuri watabaki baada ya kupata creme wakugombea. Waliosalia wanaweza kutumika katika nafasi za uteuzi ndani ya serikali au ndani ya vyama. Hapa naongelea vyama vyote.
Tano, mchato huohuo utumike katika nafasi za ubunge wa viti maalum, maana huku ndiyo kumebaki kuwa vituko. Tukipata wabunge viongozi tutapata bunge linalobeba dhana bora ya uwajibikaji na uwakilishi mzuri wa wananchi.
Nimalize kwa kusema machache kuwa, muonekano wa bunge tulilo nalo ni matokeo ya kuwa na wabunge waajiriwa badala ya wabunge wachaguliwa/wawakilishi, mnajua dhihiri kuwa wabunge wetu ndani ya bunge ndivyo walivyo katika maeneo yao ya uwakilishi. Inashangaza kuwa na mbuge ambaye hawezi ata ku-mobilize maendeleo wote kila mmoja ni kuona serikali kuu itoe majibu ya maendeleo ya wananchi kila sehemu kitu ambacho hakiwezekani.
Juhudi za mh. rais Magufuli zitaishia pafupi sana maana ukweli ni kwamba hakuna muunganiko na viongozi hasa wa ngazi za chini, si kwa wateuliwa wala wakuchaguliwa kama taifa tunahitaji mabadiliko/mageuzi makubwa kabisa ya kiuongozi hasa kwa kutoa nafasi kwa vijana wazalendo na wenye vipawa vya kiungozi kulijenga taifa.
ASANTENI
Sent using Jamii Forums mobile app