CCM Oktoba 2020 tunaomba Ubunge ubaki kuwa nafasi za uongozi si ajira

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Kwanza nianze kutoa maelezo kidogo, wanajukwaa bila kujali itikadi za vyama naomba tuelewane kwa hili nimeonekana kuitumia CCM kuwakilisha sura ya siasa ubunge maana ndiyo wanachukua nafasi kubwa.

CCM Oktoba 2020 tunaomba Ubunge ubaki kuwa nafasi za UONGOZI si AJIRA. Kwanza kabisa naomba kutoa ombi langu kwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mh. ndugu John Joseph Pombe Magufuli ambaye pia rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania . Ombi langu pia limfikie Katibu mkuu wa CCM ndg. Bashiru Ally nawaomba chondechonde mkipata huu ujumbe ufanyieni kazi tafadhali.

Sasa naomba kuelezea dhana ya kubadili Ubunge/uwakilishi ubaki kuwa uongozi na si ajira, kwa mtanzania makini anayewajibika na mzalendo ataungana na mimi katika kushuhudia khali ya bunge letu la Jamuhuri ya Muungano katika utendaji wake wa kazi. Ni wazi tukifanya utafiti wa utendaji kazi wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano nasema hakika iwapo utafiti utakuwa huru na kuzingatia uhalisia bunge letu litapata si zaidi ya 20% katika kutimiza majukumu yake hasa ya uwakilishi wa wananchi. Najua hili linaweza kuwakera wabunge ila ukweli lazima usemwe tu hakuna namna nyingine.

Ni wazi kwamba ibara ya 4 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano inaelezea vyema juu ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mikuu ya serikali ambayo ni serikali kuu, mahakama na bunge. Ugomvi wangu upo katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano naweza kurudia hizi kauli zisizopendwa kuwa bunge letu tukiliweka katika mizania ya uwajibikaji linaonekana kuwa na udhaifu/mapungufu katika dhima nzima ya uwajibikaji katikati kusimamiana hii mihimili mikuu, na binafsi naguswa kwasababu ni mhimili huu wa Bunge upo upande wa wananchi (nikiwemo mimi). Kwa miaka mingi dhana ya uwakilishi wa huu mhimili imepuuzwa sana, sababu kuu ni moja kwamba UBUNGE UMEKUWA AJIRA badala ya UONGOZI/UWAKILISHI.

Viongozi wangu wapendwa CCM ninawataja kuwakilisha viongozi wengine vyama vya siasa ambavyo vinauwezo wa kutoa au kupata wabunge wote wa kuchaguliwa na kuteuliwa ebu angalieni hili kwa umakini mkubwa licha kuwa lina ugumu wake kwasababu ya mazoea yetu kuwapata wagombea au wateuliwa kwa kuzingatia umaarufu, ukwasi, urafiki, undugu, umaarufu wa koo zao, ushikaji na ukabila hivi vitu ndivyo vimetufikisha hapa kuona bunge lisilo wajibika kwa wanachi(bunge kupoteza legitimacy ya uwakilishi).

Naomba kutoa mapendekezo ya namna ya kuwapata wagombea wa ubunge/uwakilishi wa wananchi.

Kwanza ruhusu michakato iwe wazi, kwa kuanza mapema mchato hili litatoa muda mzuri wa kuchakata wagombea bila kukimbizana na muda. Hivyo wacha watu watoe hoja na kujinadi huku mkichuja matumizi mabaya ya madaraka, rushwa, ofisi na udharimu wa namna yeyote.

Pili kuwepo na utaratibu wa wagombea kuandaa ILANI binafsi za wagombea hizi zitasaidia kuwajua kwa undani wagombea na uwezo wao wa kiuongozi na pia mtapata mawazo mbadala na kukidhi ILANI KUU YA CHAMA.

Tatu wagombea wote wapate fursa sawa kusikilizwa namna wanavyojua yale waliyoweka kwenye ILANI ZAO hapa mtawaumbua walioandikiwa hizo ILANI pia mtajua na kutambua kuwa uongozi na ajira ni vitu viwili tofauti.

Nne, chukua fursa ya kupata vingozi vyama na serikali kwa badae maana ni uhakika kuwa si wote watapata uongozi wapo wazuri watabaki baada ya kupata creme wakugombea. Waliosalia wanaweza kutumika katika nafasi za uteuzi ndani ya serikali au ndani ya vyama. Hapa naongelea vyama vyote.

Tano, mchato huohuo utumike katika nafasi za ubunge wa viti maalum, maana huku ndiyo kumebaki kuwa vituko. Tukipata wabunge viongozi tutapata bunge linalobeba dhana bora ya uwajibikaji na uwakilishi mzuri wa wananchi.

Nimalize kwa kusema machache kuwa, muonekano wa bunge tulilo nalo ni matokeo ya kuwa na wabunge waajiriwa badala ya wabunge wachaguliwa/wawakilishi, mnajua dhihiri kuwa wabunge wetu ndani ya bunge ndivyo walivyo katika maeneo yao ya uwakilishi. Inashangaza kuwa na mbuge ambaye hawezi ata ku-mobilize maendeleo wote kila mmoja ni kuona serikali kuu itoe majibu ya maendeleo ya wananchi kila sehemu kitu ambacho hakiwezekani.

Juhudi za mh. rais Magufuli zitaishia pafupi sana maana ukweli ni kwamba hakuna muunganiko na viongozi hasa wa ngazi za chini, si kwa wateuliwa wala wakuchaguliwa kama taifa tunahitaji mabadiliko/mageuzi makubwa kabisa ya kiuongozi hasa kwa kutoa nafasi kwa vijana wazalendo na wenye vipawa vya kiungozi kulijenga taifa.

ASANTENI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,810
2,000
Mkuu,
1. Umeongea mambo mengi ya msingi na ya maana sana.
2. Mengi uliyosema yanatelekezeka kukiwa na dhamira.
3. Umeitumia nafasi yako ya kidemokrasia vizuri ambapo wengi wangefanya kama wewe Tungekuwa na Tanzania bora Zaidi mapema.

Lakini,

Tatizo unalolizungumzia si tatizo la msingi "A root course", bali ni matokeo ya tatizo lingine.Tatizo la msingi ni jamii yetu kuwa na mtizamo usio sahihi juu ya mambo mbalimbali. Kwa mfano kushabikia zaidi mambo ya ajabu ajabu na ya ovyo kuliko mambo ya msingi. Kwa hiyo, hata watu wanapojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi; kwa kuwa wao nao ni zao la jamii hii hii, wengi wao wanakuwa ni changamoto kubwa.

Kwa bahati mbaya zaidi wale ambao wanafanya au kuongea mambo ya msingi hawapati uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa jamii, hivyo kushindwa. Ukumbuke demokrasia ni chaguo la wengi. Kwa hiyo nadhani kutatua tatizo la msingi, tunatakiwa kuikabili jamii zaidi, ikibalidika kila kitu kitabadilika.

Kwa mfano mada yako ni nzuri na ina mambo ya msingi lakini hutapata wachangiaji. Hupati wachangiaji si kwa sababu umekosea bali kwa sababu jamii yetu haipendi kusikia habari nzuri kama inavyopenda kusikia habari mbaya. Kwa kuwa hutapata wachangiaji utadhani labda umekosea na kukata tamaa. Baada ya kukata tamaa, utaamua ama kukaa kimya au kusema lile ambalo watu wanataka kusikia (hata kama la kijinga). Kwa kufanya hivyo utapata uungwaji mkono mkubwa Zaidi na kama ni ubunge utashinda. Hapo nadhani unaweza kuelewa kwamba kwa nini hali inayokushangaza inatokea.

Kwa hiyo tatizo lina upana huo.
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,810
2,000
Huko nyuma tulishawahi kutoa hoja kwamba, siasa za Afrika kwa digrii flani hivi ni kama biashara.

Kwa mantiki hiyo, kuna input - process - output. Kuna demand Vs supply. Kuna 'customer habits'. Kwa hiyo hivyo vitu kwa % kubwa ndio huamua nani awe nani na kipi kiwe kipi (bila kuzingatia sana kipi ni bora na kipi si bora). kwa hiyo ukitaka kuathiri matokeo, lazima uathiri hivyo hitu hapo juu.

Kuna mahali umesema kila mtu awe na ilani yake na ahojiwe isije ikawa amekariri, unadhani jamii iko interested kusikia hoja serios kihivyo? jibu la swali hili fanya tafiti kwenye social media.

Kwa mfano, mimi na wewe tunagombea ubunge, wewe umekuja na hoja za msingi na unaonekana mtu muungwana kweli. Mimi nimekuja na mziki na nakata kiuno vibaya sana na pengine natoa na rushwa, unadhani nani atashinda? sijui kama utakuwa unaona jinsi uhusiano wa vitu unavyokuwa. Kwa hiyo unakuta hata wewe ulie na hoja unaweza kushawishika kuachana na hoja zako na kukata kiuno.

Kwa hiyo, njia pekee ya kuaminika ya kushughulikia tatizo unalosema, ni kuhamisha 'motivation' na kubadili mahitaji ya wateja.
 
christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,329
2,000
Natamani mbinu zilizotumika kumpitisha Mh. Magafuli agombee Uraisi wa hii nchi, zingetumika kutupatia wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi kuanzia mwenyekitiwa mtaa, kijiji, Diwani na Mbunge.

Inavyoonekana watu wengi walioko kwenye uongozi hawaridhiki kutumikia nafasi walizonazo unakuta mtu ni Diwani kakini anawaza ubunge Mbunge naye anawaza Uwaziri au Uraisi ndio maana mambo mengi ya kimaendeleo hayaende sababu watu wanalinda vyeo na sio maslahi ya nchi.

Unakuta kiongozi watu wa chini yake wanaharibu anashindwa kuwahadhibu anaogopa kupoteza uungwaji mkono huko mbeleni.

Nilichokindua ni kuwa watu wengi wenye uwezo wa kuongoza na walio serious na maamuzi, sio rahisi uweze kuwakuta wakijiingiza sana kwenye siasa na kama wakiingia huko wanapata misukosuko sana mpaka kupata uongozi, lakin kama watu makini wangekuwa wanateuliwa kwenye nafasi mbalimbali nchi ingesonga kwa kasi kubwa.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,972
2,000
Wangalau kukiwa na tume huru ya uchaguzi, na mgombea binafsi, watapatikana wawakilishi halisi wa wananchi na sio watetezi wa vyama. Mengi ya matatizo ya sasa yatapungua.
 
gurumeti

Member
Sep 19, 2012
40
95

Umeongea vema hasa kwamba wabunge wamekuwa waajiriwa badala ya wawakilishi.

Ni kweli hakuna ubunifu kabisa majimboni. Mbunge ni kiongozi anatakiwa kumobilise siyo kila kitu kusubiri serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,565
2,000
Nilishaongea humu, inakuwaje mbunge alipwe mshahara kila mwezi wakati siyo mwajiriwa, kama ilivyo kwa madiwani wanapaswa kulipwa posho tu ya kuhudhuria vikao si zaidi ya hapo ndo maana tunatarajia wabunge wawe ni watu wanaojiweza kimapato ili wasipofushwe na rushwa toka kwa mawaziri kupitisha bajeti.

Sasa hawa wabunge wetu tayari wanahongwa mishahara toka kwenye sirikali, sasa hapo wataisimamia vipi sirikali..ideally ilitakiwa wananchi wa jimbo husika ndo wamchangie mbunge posho za kuhudhuria vikao vya kuwawakilisha..
 
Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,804
2,000
Natamani mbinu zilizotumika kumpitisha Mh. Magafuli agombee Uraisi wa hii nchi, zingetumika kutupatia wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi kuanzia mwenyekitiwa mtaa, kijiji, Diwani na Mbunge.

Inavyoonekana watu wengi walioko kwenye uongozi hawaridhiki kutumikia nafasi walizonazo unakuta mtu ni Diwani kakini anawaza ubunge Mbunge naye anawaza Uwaziri au Uraisi ndio maana mambo mengi ya kimaendeleo hayaende sababu watu wanalinda vyeo na sio maslahi ya nchi.

Unakuta kiongozi watu wa chini yake wanaharibu anashindwa kuwahadhibu anaogopa kupoteza uungwaji mkono huko mbeleni.

Nilichokindua ni kuwa watu wengi wenye uwezo wa kuongoza na walio serious na maamuzi, sio rahisi uweze kuwakuta wakijiingiza sana kwenye siasa na kama wakiingia huko wanapata misukosuko sana mpaka kupata uongozi, lakin kama watu makini wangekuwa wanateuliwa kwenye nafasi mbalimbali nchi ingesonga kwa kasi kubwa.
Waondoe ulazima wa Waziri kuwa Mbunge, ibakie tu Waziri awe na sifa za kuwa mbunge lakini isiwe hitaji la kisheria kwamba Waziri awe mbunge.

Rais atapata wigo mpana wa kuteua watu wenye sifa zilizo njema na rekodi nzuri katika mambo wanayoyafanya. Ila kwa sasa wigo wa teuzi za mawaziri ni finyu, kwa maana kwamba Bunge pekee ndiko Rais anaweza teua mawaziri ukiahana na wale wabunge 10 ambao anaweza wateua yeye.
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Ni kweli mkuu, ila nimeongea hivi sababu kimsingi nchi yetu hairuhusu wagombea binafsi na watu kupitia vyamani kuna fitina na faulu nyingi mno..! Lakini sasa tunyamaze au basi tufanye tunaloweza fanya katika mazingira haya magumu ikiwa ni pamoja na kuwaomba wenye mamlaka wasaidie.
Mkuu,
1. Umeongea mambo mengi ya msingi na ya maana sana.
2. Mengi uliyosema yanatelekezeka kukiwa na dhamira.
3. Umeitumia nafasi yako ya kidemokrasia vizuri ambapo wengi wangefanya kama wewe Tungekuwa na Tanzania bora Zaidi mapema.

Lakini,

Tatizo unalolizungumzia si tatizo la msingi "A root course", bali ni matokeo ya tatizo lingine.Tatizo la msingi ni jamii yetu kuwa na mtizamo usio sahihi juu ya mambo mbalimbali. Kwa mfano kushabikia zaidi mambo ya ajabu ajabu na ya ovyo kuliko mambo ya msingi. Kwa hiyo, hata watu wanapojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi; kwa kuwa wao nao ni zao la jamii hii hii, wengi wao wanakuwa ni changamoto kubwa.

Kwa bahati mbaya zaidi wale ambao wanafanya au kuongea mambo ya msingi hawapati uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa jamii, hivyo kushindwa. Ukumbuke demokrasia ni chaguo la wengi. Kwa hiyo nadhani kutatua tatizo la msingi, tunatakiwa kuikabili jamii zaidi, ikibalidika kila kitu kitabadilika.

Kwa mfano mada yako ni nzuri na ina mambo ya msingi lakini hutapata wachangiaji. Hupati wachangiaji si kwa sababu umekosea bali kwa sababu jamii yetu haipendi kusikia habari nzuri kama inavyopenda kusikia habari mbaya. Kwa kuwa hutapata wachangiaji utadhani labda umekosea na kukata tamaa. Baada ya kukata tamaa, utaamua ama kukaa kimya au kusema lile ambalo watu wanataka kusikia (hata kama la kijinga). Kwa kufanya hivyo utapata uungwaji mkono mkubwa Zaidi na kama ni ubunge utashinda. Hapo nadhani unaweza kuelewa kwamba kwa nini hali inayokushangaza inatokea.

Kwa hiyo tatizo lina upana huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Ninachomanisha Ilani zao, wanazipresent kwa wanachama kwa njia ya vikao vya kichama ili kuwachuja hukohuko walau wakuwadhibiti hukohuko ili watakao fika kwenye kinyanganyiro wame walau wanaojielewa kwa vyama vyote.
Huko nyuma tulishawahi kutoa hoja kwamba, siasa za Afrika kwa digrii flani hivi ni kama biashara.

Kwa mantiki hiyo, kuna input - process - output. Kuna demand Vs supply. Kuna 'customer habits'. Kwa hiyo hivyo vitu kwa % kubwa ndio huamua nani awe nani na kipi kiwe kipi (bila kuzingatia sana kipi ni bora na kipi si bora). kwa hiyo ukitaka kuathiri matokeo, lazima uathiri hivyo hitu hapo juu.

Kuna mahali umesema kila mtu awe na ilani yake na ahojiwe isije ikawa amekariri, unadhani jamii iko interested kusikia hoja serios kihivyo? jibu la swali hili fanya tafiti kwenye social media.

Kwa mfano, mimi na wewe tunagombea ubunge, wewe umekuja na hoja za msingi na unaonekana mtu muungwana kweli. Mimi nimekuja na mziki na nakata kiuno vibaya sana na pengine natoa na rushwa, unadhani nani atashinda? sijui kama utakuwa unaona jinsi uhusiano wa vitu unavyokuwa. Kwa hiyo unakuta hata wewe ulie na hoja unaweza kushawishika kuachana na hoja zako na kukata kiuno.

Kwa hiyo, njia pekee ya kuaminika ya kushughulikia tatizo unalosema, ni kuhamisha 'motivation' na kubadili mahitaji ya wateja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Kuna shida kubwa sana, huwa najiuliza hivi wabunge kazi zao hasa ni nini, hawana strategy yeyote kuleta maendeleo katika majimbo yao.
Natamani mbinu zilizotumika kumpitisha Mh. Magafuli agombee Uraisi wa hii nchi, zingetumika kutupatia wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi kuanzia mwenyekitiwa mtaa, kijiji, Diwani na Mbunge.

Inavyoonekana watu wengi walioko kwenye uongozi hawaridhiki kutumikia nafasi walizonazo unakuta mtu ni Diwani kakini anawaza ubunge Mbunge naye anawaza Uwaziri au Uraisi ndio maana mambo mengi ya kimaendeleo hayaende sababu watu wanalinda vyeo na sio maslahi ya nchi.

Unakuta kiongozi watu wa chini yake wanaharibu anashindwa kuwahadhibu anaogopa kupoteza uungwaji mkono huko mbeleni.

Nilichokindua ni kuwa watu wengi wenye uwezo wa kuongoza na walio serious na maamuzi, sio rahisi uweze kuwakuta wakijiingiza sana kwenye siasa na kama wakiingia huko wanapata misukosuko sana mpaka kupata uongozi, lakin kama watu makini wangekuwa wanateuliwa kwenye nafasi mbalimbali nchi ingesonga kwa kasi kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Hapa kuna issue kubwa haswa kukosa wagombea binafsi..! Ila tubambane kupaza sauti labda tunaweza kubadili hali kwa nafasi yetu.
Wangalau kukiwa na tume huru ya uchaguzi, na mgombea binafsi, watapatikana wawakilishi halisi wa wananchi na sio watetezi wa vyama. Mengi ya matatizo ya sasa yatapungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Nilishaongea humu, inakuwaje mbunge alipwe mshahara kila mwezi wakati siyo mwajiriwa, kama ilivyo kwa madiwani wanapaswa kulipwa posho tu ya kuhudhuria vikao si zaidi ya hapo ndo maana tunatarajia wabunge wawe ni watu wanaojiweza kimapato ili wasipofushwe na rushwa toka kwa mawaziri kupitisha bajeti. Sasa hawa wabunge wetu tayari wanahongwa mishahara toka kwenye sirikali, sasa hapo wataisimamia vipi sirikali..ideally ilitakiwa wananchi wa jimbo husika ndo wamchangie mbunge posho za kuhudhuria vikao vya kuwawakilisha..
Hili jambo linachukuliwa kirahisi ila lina madhara makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,338
2,000
Kimsingi mbuge hapaswi kuwa waziri maana analeta double standard, hawezi kuikosoa serikali ambayo yeye ni mmoja wao.
Waondoe ulazima wa Waziri kuwa Mbunge, ibakie tu Waziri awe na sifa za kuwa mbunge lakini isiwe hitaji la kisheria kwamba Waziri awe mbunge.

Rais atapata wigo mpana wa kuteua watu wenye sifa zilizo njema na rekodi nzuri katika mambo wanayoyafanya. Ila kwa sasa wigo wa teuzi za mawaziri ni finyu, kwa maana kwamba Bunge pekee ndiko Rais anaweza teua mawaziri ukiahana na wale wabunge 10 ambao anaweza wateua yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom