CCM ni Mtaji kwa Watanzania, ndiyo maana inapendwa kama Zimwi

Pamoja na kwamba wataimba kra ili washinde, Kura yangu sitawapa kabisa.:clock:
 
Mkuu Padri Kishoka heshima kwako. Mara nyingi huwa nafikiri kama wewe lakini najirudi kidogo na kujiuliza hivi watu wazima na akili zao wanawezaje kufikia hali ya kushindwa kuona ukweli na kukubali kuongozwa na kada ya mabaradhuli kiasi hiki? Majibu yanayonijia (ambayo baadhi yamegusiwa na wakuu humu) ni kwamba (1) watanzania wamedhikishwa kiasi cha kutoona zaidi ya mlo ufuatao; (2) wameaminishwa kuwa wao (kura zao) si factor katika ushindi wa watawala - wawapigie, wasiwapigie wao wana namna ya kujipa ushindi; na (3) chama tawala kinaonyesha dalili zote za kutishia amani ya nchi endapo itadhihirika kwamba kuna juhudi za dhati za kukinyima dhamana ya uongozi hodhi (dominant position) - hakisiti kutishia nguvu ya vyombo vya dola kwa yeyote anayetishia mustakabali wa watawala.

Hivi sasa kwetu sisi wengine ni vigumu kutofautisha kati ya uongozi wa chama, serikali, majeshi, tume ya uchaguzi na msajili wa vyama. Kidogo tumeona nafuu kwenye uongozi wa Bunge na mahakama. Katika mazingira ya aina hiyo, ni yule aliye tayari kujitoa mhanga ndiye atakayeweza kuendesha mapambano ya dhati dhidi ya uongozi mbovu wa chama tawala tulio nao hivi sasa. Huwa namuona Dk. Slaa kama mtu wa aina hiyo. Tatizo ni kuwa naye anapuuzwa tu nafirkiri kwa vile wameshaona ni mtu mmoja peke yake ambaye wengi bado hawako tayari kumuunga mkono.

Kwa upande wa vyama vya upinzani, wao ndio walitakiwa wahamasishe mshikamano wa kutokubali ujinga nchini. Hebu ona wanavyotofautiana. Utawezaje kuwaweka CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP, n.k. pamoja? Angalau ajenda ya kisiasa inaonekana CHADEMA na CUF. Wengine hapo ni kama NGO tu na wengine ni kama ma-vuvuzela wa CCM!
 
Mchungaji,

... Wapigaji wa aina hii wakipewa chakula cha wiki moja na kuambiwa waipigie CCM, watafanya hivyo bila kuwa na mapenzi yoyote kwa CCM. ...

Hapo lazima na ujinga wa aina fulani uwepo. Leo hii mtu ukinifilisi kiasi cha kuwa ombaomba ukanidondoshea kilo za unga na mboga ya wiki basi ndio nisahau adha uliyoniletea na kukupigia kura? Au ndio nimepata na ganzi ya kufikiri kura inatoka automatiki!
 
Jasusi,

Sijasahau kuwa CCM ni chama cha Wakulima na Wafanyakazzi, ila ninachoendelea kushangaa ni Upumbavu wa Wana CCM na Watanzania kama BAK anavyouzungumzia na ndiyo maana nikiangalia kwa undani haya mapenzi yasiyo na msingi, ni dhahiri Watanzania wameridhika na CCM.

Si kwamba ni Wajinga, bali ni Upumbavu wa kuridhika na ukipima kuridhika kwao ndiko utaona hayo niliyoyaeleza juu, kuwa ni woga wa mabadiliko.

ReverendK,

Wantanzania si waoga tu wa mabadiliko bali ni ujinga ambao CCM wameshawajaza watanzania kuwa UPINZANI maana yake "VITA". Nakumbuka sana 2005, yale matangazo ya TV ambayo yalikuwa yanarushwa it was a total lies!! Sasa watanzania wengi ni product hiyo!! Na ndo wale wa kule kwetu!! Kwa kuwa mfumo wa chama kimoja haujawahi kutofautisha na huu wa vyama vingi, mambo yanajiendea tu, ukiangalia tunaburuzwa kwenye vitu vingi sana!! Ili mradi mambo yaende.

Kinachonikatisha tamaa zaidi ni yale maamuzi ya Justice Ramadhani ya jopo lake; wameshindwa kutafsiri vizuri katiba kama sheria mama na kurudisha bungeni suala ambalo liliwahusu wao!!!

Hakuna uchawi.........
 
Hivi mpaka wakati huu, ni vipi mada hii inaelekea? Baada ya CCM kujitangaza kujivua gamba na kuwa karibu zaidi na wananchi, je bado CCM ni mtaji kwa Watanzania?
 
Hivi mpaka wakati huu, ni vipi mada hii inaelekea? Baada ya CCM kujitangaza kujivua gamba na kuwa karibu zaidi na wananchi, je bado CCM ni mtaji kwa Watanzania?

Very much so, Sir! Kama wengi wetu bado tuna akili ya mishen-taun kama mtindo wa maisha, ni vigumu kufikiria mfumo mbadala zaidi ya unaolelewa na CCM. Tumaini letu ni kuongezeka kwa kada ya vijana wanaotaka mabadiliko wakihamasishwa na vyama kama CDM.
 
Jasusi,

Kama ni wajanja wachache, kura zao haziwe kuleta landslide, wao ni kundi dogo sana hata kama ni watoa rushwa. Ukitafakari kwa nini Watanzania ni waoga kukipigia kura chama kingine, si suala la kurubuniwa kwa Pilau bali inabidi tukubali kuwa kuna mengine yanayowafanya Watanzania wawe na mapenzi ya ajabu na CCM

Natumaini ni Rev. wa kweli. Waliopiga kura ni 40% ya waliojiandikisha. 61% za Rais wa Nec ni sawa na kura za waliojiandikisha 24.4% ina maana 75.6% ya wapiga kura hawakumpigia kura rais wa nec. Kwa hesabu ndogo tu hiyo naomba uwatake radhi watanzania.

Kura hizo 61% kwa taarifa sahihi ya matokeo halali zilikuwa ni 27% ikiwa ina maana 34% ziliibwa toka vyama vya "upinzani"/vingene ukirudia hesabu kwa 40% ya wapiga kura alipata 10.8% ya waliojiandikisha. 89.2% ya waliojiandikisha hawakumchagua. Kwa hilo pia tafadhali tutake radhi watanzania.

Vyama vya "upinzani"/vingine viliibiwa 34% za waliopiga kura ukijumlisha na na 39% zilizotangazwa unapata 73% ya waliojiandikisha walichagua vyama vya upinzani ambayo ni sawa na 29.2% kwa 40% yawapiga kura.

Tafadhali utuelewe baadhi yetu Watanzania na ujiulize maswali mawili tu.

1. Kwa nini 60% hawakupiga kura? Jibu ni kwa sababu ya uchaguzi dola

2. Kwa nini kura za urais haziwi contested mahakamani? Jibu ni lile lile la hapo juu.

TUFANYE

1. Hakuna kukata tamaa kwani kila jambo lina mwisho

2. Mabadiriko ya katiba kama hayatakuwa na mizengwe ya kidola hapo utatuhukumu. Lakini yakienda bila mizengwe ya kikatiba utapata kauli sahihi ya Watanzania wote watakaopiga kura

Mwisho nakushauri REV. kuna mabadiriko ya aina mbili:-
  • Ya uasilia (evolutionery) haya yana nguvu kuliko dola.
  • (Revolutionery) ambayo ya msuguano mkali na yana athari.
NADHANI SISI WATANZANIA TUNAPITIA KWENYE MCHANGANYIKO WA HAYO YOTE. MSHINDI NI TANZANIA YENYE NEEMA
 
natumaini ni rev. Wa kweli. Waliopiga kura ni 40% ya waliojiandikisha. 61% za rais wa nec ni sawa na kura za waliojiandikisha 24.4% ina maana 75.6% ya wapiga kura hawakumpigia kura rais wa nec. Kwa hesabu ndogo tu hiyo naomba uwatake radhi watanzania.

Kura hizo 61% kwa taarifa sahihi ya matokeo halali zilikuwa ni 27% ikiwa ina maana 34% ziliibwa toka vyama vya "upinzani"/vingene ukirudia hesabu kwa 40% ya wapiga kura alipata 10.8% ya waliojiandikisha. 89.2% ya waliojiandikisha hawakumchagua. Kwa hilo pia tafadhali tutake radhi watanzania.

Vyama vya "upinzani"/vingine viliibiwa 34% za waliopiga kura ukijumlisha na na 39% zilizotangazwa unapata 73% ya waliojiandikisha walichagua vyama vya upinzani ambayo ni sawa na 29.2% kwa 40% yawapiga kura.

Tafadhali utuelewe baadhi yetu watanzania na ujiulize maswali mawili tu.

1. Kwa nini 60% hawakupiga kura? Jibu ni kwa sababu ya uchaguzi dola

2. Kwa nini kura za urais haziwi contested mahakamani? Jibu ni lile lile la hapo juu.

Tufanye

1. Hakuna kukata tamaa kwani kila jambo lina mwisho

2. Mabadiriko ya katiba kama hayatakuwa na mizengwe ya kidola hapo utatuhukumu. Lakini yakienda bila mizengwe ya kikatiba utapata kauli sahihi ya watanzania wote watakaopiga kura

mwisho nakushauri rev. Kuna mabadiriko ya aina mbili:-
  • ya uasilia (evolutionery) haya yana nguvu kuliko dola.
  • (revolutionery) ambayo ya msuguano mkali na yana athari.
nadhani sisi watanzania tunapitia kwenye mchanganyiko wa hayo yote. Mshindi ni tanzania yenye neema

kweli wewe baba, maono na hekima ni ushahidi tosha.
 
Back
Top Bottom