CCM ni Mtaji kwa Watanzania, ndiyo maana inapendwa kama Zimwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ni Mtaji kwa Watanzania, ndiyo maana inapendwa kama Zimwi

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jun 26, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nimekubali, kama ilivyovigumu kwa Ufisadi kuondoka Tanzania kutokana na mfumo wake kuingilia jamii ya Tanzania na kukubalika kuwa ni kitu cha kawaida, ndivyo jinsi CCM ilivyo kwa Watanzania, mtaji wenye faida usioleta usumbufu au kuwalazimisha Watanzania kubadilika hivyo ni heri kwa Watanzania kuendelea kuwa na Zimwi CCM na si mtu mwingine.

  Watanzania ni wagumu sana kukubali mabadiliko, iwe ni mfumo wa maisha, utendaji kazi au jambo lolote. Mfano kama ikiwa ndani ya CCM wanaendeleza mfumo dume wa miaka ya 1970 uliotuletea chama kimoja na mgombea mmoja na leo hii yeyote anayeamka kupingana na aliyeko madarakani huonekana ni adui, vivyo hivyo kaugonjwa haka kametambaa kwa Watanzania.

  Kwa Watanzania wengi, kuendelea kuongozwa na CCM ni heri ya kuendeleza mfumo wao wa kimaisha ambao wameshauzoea na kuridhika nao.

  CCM ni chama ambacho kimeondoka kuwa chama makini na kuwa chama kilicho mkao wa tupo tupo, kuna uzembe, uvivu, ubangaizaji, utegemezi, kila jambo lina sababu la kuhalalisha udhaifu na visingizio vingi.

  Ama ni Chama ambacho hakina nia ya kuleta maendeleo ya kweli zaidi ya kuendeleza maisha na mfumo wa Ubabaishaji pamoja na kuwa kuna maandiko elfu yanaoonyesha kuwa kuna rasimu ya kuleta mapinduzi na maendeleo kuonddoa Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  Lakini kama CCM ilivyo, ndiyo Watanzania tulivyo, inapokuja kwenye utendaji, ni wazito, mgando na hatuna wepesi wa kuwa wenye ufanisi, umakini au ufuatiliaji wa hali ya juu. Kama CCM ya sasa kupenda njia za mkato na utegemezi, ndivyo Watanzania tunavyoendekeza dezo, misheni na kuchukia kutoka jasho, iwe ni kufikiri au kufanya kazi.

  Si kwamba hatufanyi kazi, bali tunafanya kwa kiasi tu, kwa kujihimu na si kwa malengo ya muda mrefu au kwa nyongeza ili kujihakikishia akiba na uhakika wa keshokutwa achilia mbali mwezi na mwaka ujao.

  Hivyo si cha ajabu kuona kuwa Watanzania tunaivumilia CCM kwa kuwa ni Chama pekee ambacho tunafanana nacho na tunaweza jitambulisha rasmi nacho, kimfumo, kiutendaji, kimaadili na hata kimipango.

  Leo hatuwaamini CHADEMA, NCCR, CUF, TLP na ahta kama ingekuwa ni CCJ au Mgombea binafsi kwa kuwa hatujui kama wakija hawa watalazimisha tubadilike na kuanza mfumo mpya ambao utatuwajibisha kwenda zaidi ya kile cha mazoea (above and beyond), kuwa tutakuwa fanisi, tutaachana na utegemezi na itatubidi kubadilika kabisa.

  Kama walivyo Wazee wetu ambao hawataki kubadilika na kung'angania mfumo wa kale, ndivyo sisi kama Watanzania tulivyoridhika na kupenda kuiona CCM inaendela maana tunafanana nayo.

  Tunaogopa kumpa dhamana ya uongozi "Kichaa" atakayekata mirija yetu ya utegemezi, uzembe, uvivu, ubangaizaji, umisheni tauni, ufisadi, urasimu, rushwa, wizi, kuridhika na unyonge, umasikini na hata ujinga.

  Kama ndugu zetu Watindiga, walivyokataa kuachana na maisha asili, ndivyo kama Taifa tunavyoogopa kumpa dhamana mtu mwingine maana tunaogopa umande na kutoka jasho.

  Basi ni wazi Vyama vya Upinzanina yeyote mwenye dhamira ya kuiongoza Tanzania ambaye si kutoka CCM, ana kazi ngumu na inabidi aanze kazi na safari hii si kusubiri wakati wa uchaguzi au kuchagua vitu viwili au vittu kuongea na Watanzani abali ni kuishi maisha na kuonyesha vitendo vya mabadiliko vinavyoleta maendeleo ya kweli na hivyo kujenga wivu mzuri wa maendeleo na si inda, chuki au kubezana.

  Nasikitika kuwa huu ni ukweli usiokwepeka na ni wengi wenu mtakata na kusema si sahihi, lakini jibu moja ni tawapa, subirini matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuthibitisha kuwa si lile la udhaifu wa Wapinzani kama nilivyoongelea kwa muda mrefu au mchezo mchafu wa CCM kwenye uchaguzi, bali ni woga wa Watanzania wa mabadilikouliojenga mapenzi ya ajabu kwa CCM pamoja na udhaifu na kushindwa kwa CCM kutuuondoa kutoka Umasikini, Ujinga, Maradhi, Utegemezi na kuishi kwa maadili.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Reverend,
  Ungesema CCM ni mtaji kwa "wajanja" wa Tanzania. Ukiona vyama vya CCM vinaanzishwa Reading, Oxford, sijui wapi Norway, si kwa sababu CCM inajali maslahi ya Watanzania wa kawaida, ila ni kwa sababu wajanja wachache, wenye tamaa ya kuwa mafisadi, wameshagundua the easiest way to make a living in Tanzania na kuishi maisha ya tambarare.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  Kama ni wajanja wachache, kura zao haziwe kuleta landslide, wao ni kundi dogo sana hata kama ni watoa rushwa. Ukitafakari kwa nini Watanzania ni waoga kukipigia kura chama kingine, si suala la kurubuniwa kwa Pilau bali inabidi tukubali kuwa kuna mengine yanayowafanya Watanzania wawe na mapenzi ya ajabu na CCM
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Reverend,
  Kitu unachosahau ni kwamba CCM is a mass party. Hii ilijengwa na Mwalimu Nyerere. Lakini CCM ya leo imeshatekwa na makanjanja wa kisiasa ambao hata ukiwauliza what a mass party means hawawezi kujibu. Sasa hivi kwao CCM ni mtaji. Wapate ubunge, wachaguliwe mawaziri, waweze kupata 20% zao basi. Majority ya Watanzania hawajalistukia hili jambo na makanjanja wanaotafuta short cuts to riches ndio unaowaona kila kukicha wakifungua matawi ya chama Redding, Oslo, and God knows where else. Hawa si kwamba wana uchu na nchi yao, no way. Wana uchu wa matumbo yao.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,088
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev, kwa maoni yangu asilimia kubwa ya wapiga kura wa Tanzania vijijini hata mijini ni wapumbavu mno na hawana uwezo wa kuchambua mambo. Propaganda zinazoenezwa na CCM kwamba CHADEMA ni chama cha Wachagga wengi wanaamini hilo, na wengi wakishapewa rushwa kidogo tu wenyewe wanaita takrima kama vile vijisenti kidogo, pilau, kilevi na kuimbiwa na yule Komba kwamba CCM ni nambari one, wizi wa kura na unyanyasaji wanaofanyiwa wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani vyote hivi vinachangia katika ushindi wa "kishindo" kama unavoitwa na wenyewe CCM.

   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jun 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mchungaji,

  Sidhani kama kweli watanzania wengi wana "mapenzi ya ajabu kwa CCM" kama unavyodai. Mimi nijuavyo kulingana na population ya kijijini kwangu, ambao ni wapigaji wakuu wa CCM, kuna watanzania wa aina mbili wanaoipigia CCM. Kuna ile aina ambayo inaihusisha CCM na Serikali, na kuamini kuwa usipoipigia CCM basi serikali itaanguka na kuwapo machafuko. Watu hawa huipigia CCM kwa sababu ya woga na siyo kwa sababu ya mapenzi. Aina nyingine ya watanzania ni wale ambao hawajaui wajibu wao kama raia. Kwao wao kitendo cha kupiga kura si cha muhimu kabisa, anaweza akapiga kura na anaweza asipige kura; nguvu yake yote ameilekeza kwenya kutafuta chakula cha familia yake kusudi wawezea kuiona kesho na kesho kutwa. Wapigaji wa aina hii wakipewa chakula cha wiki moja na kuambiwa waipigie CCM, watafanya hivyo bila kuwa na mapenzi yoyote kwa CCM. Kwa bahati mbaya makundi hayo mawili yanafikia jumla ambayo ni zaidi ya asilimia themanini za watanzania wote!!
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  Sijasahau kuwa CCM ni chama cha Wakulima na Wafanyakazzi, ila ninachoendelea kushangaa ni Upumbavu wa Wana CCM na Watanzania kama BAK anavyouzungumzia na ndiyo maana nikiangalia kwa undani haya mapenzi yasiyo na msingi, ni dhahiri Watanzania wameridhika na CCM.

  Si kwamba ni Wajinga, bali ni Upumbavu wa kuridhika na ukipima kuridhika kwao ndiko utaona hayo niliyoyaeleza juu, kuwa ni woga wa mabadiliko.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kishoka,
  Hiyo ndiyo changamoto ya wapinzani. They have to prove that thay can do better than CCM without bringing any upheavals.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,088
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev pamoja na upumbavu wa wapiga kura walio wengi, vyama vya upinzani navyo labda vimeshindwa kujieleza mbele ya wapiga kura kwanini wawapigie kura wao na kuleta mabadiliko nchini. Pia kama utakumbuka Watanzania wengi walivishauri vyama vya upinzani viungane na kuunda chama kimoja chenye nguvu lakini hadi leo hii hakuna sababu zozote za muhimu zilizotolewa na vyama vya upinzani zinazosababisha kushindwa kuungana.

  Nakumbuka mwishoni mwa mwaka 2008 Raila Odinga alitembelea nchini na kukutana na viongozi wote wa juu wa upinzani na katika mkutano huo aliwashauri kwamba kama wanataka kuishinda CCM kimojawapo cha muhimu kukifanya ni kuungana.

  Pia wapinzani wenyewe kuna mamluki chungu nzima kama akina Mrema ambaye badala ya kukipigia debe chama chake sasa hivi amekuwa mpiga debe maarufu wa Kikwete, yule Cheyo naye.

  Kwa hiyo ukiangalia kuna vitu vingi vinachangia hali ya tuliyonayo nchini inayosababisha CCM kuendelea kuwepo madarakani pamoja na kuwa utendaji wao ni hovyo kabisa.
   
 10. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Very good analysis. Nimekuwa nikijiuliza sana kwanini Watanzania hawaoni maovu yanayotendeka chini ya CCM na kuyakataa na kuikataa CCM. Mchango wako umeweza kunifafanulia. Asante.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Reverend, naomba nikusahihishe kidogo, kusema CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi ni overstatement, CCM inaendeshwa kutoka mjini na wajanja wachache ambao daima wanapenda kuwa madarakani. Wakulima hawana sauti kabisa CCM na wafanyakazi mwenyekiti wa CCM kisha sema hahitaji kura zao kwani wako laki tatu or thereabout. Kwa hiyo sio kweli unachosema.

  Mtu anayesema anataka kugombea anaongelea toka Dar es salaam na anaongea na watu wa Dar es Salaam toka jimbo analolitaka wakulima wenyewe wanapelekewa pilau, kanga T shirt na Kofia wanakuwa wameridhika kabisa.

  At the bottom line tatizo la watanzania ni njaa iliyokithiri, kwa shillingi 10,000/= unanunua kura bila hiyana. Reverend poverty level tanzania iko juu mno haina mfano. Ninaposema njaa nina maana ukosefu wa chakula na hela ya kulipia matibabu, ada ya watoto, kujenga nyumba yenye hadhi na kununua angalau mtumba mtu alitokea na kutoa hivyo anaonekana mungu kwa watu wa vijijini.

  Wanachi wa tanzania hawajaridhika hata kidogo wana matatizo mengi hayana mfano, wengi wanatumia magadi badala ya chumvi, sukari ni hekaya za abunuwasi, matibabu ni ndoto, elimu ndo usiseme.

  Inatisha, inasikitisha hasa ukizingatia rasilimali ambazo nchii hii tunayo.

  Upinzani, umejitahidi sana ila serikali haiko willing kuwa level nao, ndo maana wanaogopa kusajili CCJ hawataki mgombea huru, sio bure kabisa wanajua wakikubali basi wamekwisha.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ngambo Ngali,
  Ingewezekana ningekuwekea senks 2.
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Pata nafasi uongee na mtu ambaye unaona n down trodden muulize amejiandikisha atasema ndio, muulize atagiga kura atasema hapana ukimuuliza kwa nini jibu atalokupa utaelewa ni kwa nini CCM inapeta.

  Opposition wangekaa na kufanya postmoterm haihitaji hata hela people are miserable, tired and disillusioned.
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Thats the reality Jasusi, on a light touch hata hiyo moja hujanipa
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,088
  Trophy Points: 280
  I second you opinion Jasusi lakini mimi ningemuwekea 3. Uchambuzi mzuri sana Ngambo Ngali, michango yako hapa jamvini imetulia mno na huwa unaandika kwa umakini mkubwa. Hongera sana Mkuu.
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Bubu asante sana kwa hakika ukweli ni kwamba watu wengi tuko isolated na realities of life, hatujui upande mwingine wa mtanzania ukoje tujaribu kufanya hivyo na mabadiliko yatakuwepo tu. Viongozi wa upinzani na wanachama wao waende kwa wananchi, wakae nao, wasikie kilio chao, waone matatizo yao, waone ndoto zao.

  Redio, magazeti na TV ni uongo wa hali ya juu, tunavyosikia, kuona na kusoma sio maisha ya mtanzania.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naomba nitofautiane kidogo kuhusu hilo suala la Watz kutopenda mabadiliko. Nadhani tumesahau huko nyuma wakati wa uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 ambapo Watz almanusra waing'oe CCM madarakani.

  Hakika CCM ilikuwa inaenda na maji pasipo kutokea vitu viwili:

  1. Kukataa kwa Mwl Nyerere kuwa above party politics na hivyo kuikampenia CCM vikali kwani naye aliyaona maji marefu. Kuna hoja kwamba Nyarere alifanya hivyo kwa kujihami yeye mwenyewe binafsi kwani alikuwa na hofu kwamba kama angeshika nchi, Mrema angepata ushawishi/msukumo mkubwa wa kumpandisha kizimbani, kwani Nyerere naye alikuwa na madhambi yake kwa Watz, tena mazito tu.

  2. Uvurugwaji wa uchaguzi by NEC katika mkoa wa Dsm ambako kulikuwa na wapiga kura karibu laki tisa na ambako Mrema ilikadiriwa Mrema pekee angezoa zaidi ya laki sita (nazungumzia kura ya urais) hivyo kumuweka Mkapa (ambaye hakuwa anajulikana kabisa) katika hofu kubwa. Lengo la uvurugwaji wa uchaguzi ktk mkoa wa Dar ni ilikuwa ni kuangalia kwanza Mkapa ana-fare vipi huko mikoani ki-kura. Strategy hii ilimsaidia sana Mkapa kwani uchaguzi uliporudiwa hapa Dar ni wapiga kura chini ya laki tatu walipiga kura (wengi walisusa, walipoteza, walichana (kwa hasira) shahada zao, na NEC kutokuwa na mpango serious na wa wazi wa kuwaandikisha upya wale waliopoteza shahada.

  Hoja ya msingi ninayotaka kusema ni kwamba Watz wanao uwezo wa kubadilika na kuiondoa CCM, tatizo ni kutokuwa na serious and credible leadership katika upinzani.

  Kwa mfano, kitokee kitu kama vile cha mwaka 1995 – yaani senior cabinet minister – mwenye record thabiti ya kupinga ufisadi kwa waziziwazi na kwa dhati katika serikali ya chama chake aondoke CCM na kujiunga na chama kingine credible (kama vile Chadema kwa mfano) na kule wampokee na kumpa uongozi. Nasisitiza awe waziri mwandamizi na siyo Wabunge tu wa CCM kama vile akina Dr M wakyembe, Mpendazoe au Anne Kilango. Hawa wangekuwa mawaziri labda.

  Kwa sasa hivi waziri gani anaweza kufanya hivyo na kukubalika na umma? Labda Pinda pekee, au Magufuli? Hali kadhalika Dr Shein – iwapo tu Upemba wake hautatiwa maanani sana na watu wa Bara. Batila Burian? Labda.

  Speaker Sitta na viongozi wengine wakuu wamechelewa sana na hivyo tayari wamechafuliwa kwa kiasi kikubwa.

  (Wana-JF wenzangu mnaweza kuiongeza orodha hii).

  CCM inalijua sana hili kwamba mbaya wao atatoka humo humo miongoni mwao na bila shaka wanaweweseka sana hilo kutokea.

  Kwa kumalizia tu post hii, ingawa Mrema aliweza kuzoa wafuasi wengi mwaka 1995, alikuwa na dosari nyingi tu na angeshinda kura ya urais angeweza kuwa dikteta mbaya. (kwani wametokea, na wako madikteta wazuri duniani hapa). Lakini ukweli mmoja tu ungebakia – kwamba CCM isingekuwa tena chama kama kilivyo hivi sasa, ingetokomea mbali kama vile KANU (Kenya) na UNIP (Zambia).
   
 18. T

  Tata JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na uchambuzi wako kuwa watanzania wengi kimsingi hatutofautiani na viongozi wetu mafisadi kwani wanatokana na jamii yetu. Ni wavivu, hatupendi mabadiliko yatakayo tulazimisha kufanya kazi kwa bidii, tunapenda viongozi wenye mizaha na maneno mengi wasio tenda yale wanayoyasema, mwizi wa mali za umma anaitwa "sharp" au mwenye akili, kutumia bongo maana yake ni kuiba au kujishirikisha katika rushwa, kukwepa kodi na wizi mwingine, tunavumilia wezi wa mabilioni ya fedha za umma lakini tunachoma moto vibaka na wezi wa kuku mitaani. Kwa ufupi tunapenda status quo.

  Ila hali hii haikutokea kwa bahati mbaya ni mfumo uliojengwa tangu wakati uhuru na TANU na baadaye CCM na tunachoshuhudia sasa ni matunda tu.
   
 19. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev,

  Maneno yako ni kweli kabisa.

  Lakini mimi naona mambo yanabadilika japo taratibu. Kadri idadi ya watanzania inavyozidi kuongezeka na utandawazi unazidi kushika kasi, Watanzania tunaanza kuwa makini. Pamoja na kua CCM itabaki madarakani, lakini lazima itabadilika. Wale Watanzania watakaoshindwa kubadilika watakufa kwa njaa na maradhi kwasababu ya uvivu na ujinga wao. Kama kasi ya kubadilika kwa CCM itakua chini kuliko kasi ya kubadilika kwa Watanzania kwa ujumla, basi hapo lazima itapigwa chini.

  One thing is for certain, change is inevitable for CCM and Tanzanians as a whole.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nimeshuhudia hizi mnazoita "chaguzi" tangu mwaka 1975. Ukweli ni kwamba ni sehemu ndogo sana ya Tanzania na Watanzania ambako kura za kweli zinapigwa na zinahesabika kihalali hasa kwenye kura za URAIS.
  CCM haijawahi na haitashinda Zanzibar, lakini kila uchaguzi tangu 1995 tunatangaziwa mgombea wake ndiye mshindi! Mkisubiri CCM ishindwe kwa sanduku la kura nawapa miaka 25 ijayo kwa uchache.
   
Loading...