CCM ni Mahututi-Dr Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbrod Slaa amesema kumteua Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni sawa tu na kumhamisha mgonjwa mahututi-CCM kutoka hospitali ya Mukama na kumhamishia hospitali ya Kinana ambapo mwisho wake ni kifo tu kwa huyo mgonjwa.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Karagwe jana Dr Slaa anayetambulika kama Rais wa mioyo ya watu alisema kwa sasa CDM imekuja na mkakati mpya ambao ni kuwahamasisha wananchi maeneo ya vijijini na kuepuka kasumba ya kufanya mikutano mijini tu.Amesema ataliongoza jeshi la CDM kujichimbia vijijini ili kazi ya kuizika CCM 2015 iwe nyepesi kabisa.

Katika mkutano huo wanachama 324 walijitoa CCM na kujiunga na CDM.Pia CDM ilitoa kadi kwa wanachama wapya 1836.

Kwa takriban siku tatu sasa Dr Slaa amekuwa gumzo katika wilaya ya Karagwe kutokana na jinsi alivyoiteka wilaya hiyo tangia awasili ambapo kila anapoonekana maelfu ya watu hujipanga na kutamani walau kumshika mkono kama ishara ya kumtakia kila la kheri na kumuunga mkono.

Wachunguzi wa siasa za Karagwe wanasema mikutano ya CDM jimboni humo imevunja rekodi na kwa hakika CCM wilaya imepata hofu kubwa.Katika miji ya Kayanga na Karagwe ilipofanyika mikutano ya CDM wananchi walisimamisha shughuli zote na kuungana na makamanda wa CDM.

Source:Tanzania Daima
 
Ndio, Ukilinganisha picha za mkutano wa CCM Arusha mjini na zile za Karagwe. Utasema hivi CCM is dead indeed. Nashauri CCM wajipange kuwa wapinzani, na wasipofanya hivyo, watatoweka kama UNIP na KANU.
 
Dr Slaa ni mwiba kwa CCM na hakika CCM wanajua hawako salama chini ya CDM inayoongozwa na Dr Slaa.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbrod Slaa amesema kumteua Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni sawa tu na kumhamisha mgonjwa mahututi-CCM kutoka hospitali ya Mukama na kumhamishia hospitali ya Kinana ambapo mwisho wake ni kifo tu kwa huyo mgonjwa.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Karagwe jana Dr Slaa anayetambulika kama Rais wa mioyo ya watu alisema kwa sasa CDM imekuja na mkakati mpya ambao ni kuwahamasisha wananchi maeneo ya vijijini na kuepuka kasumba ya kufanya mikutano mijini tu.Amesema ataliongoza jeshi la CDM kujichimbia vijijini ili kazi ya kuizika CCM 2015 iwe nyepesi kabisa.

Katika mkutano huo wanachama 324 walijitoa CCM na kujiunga na CDM.Pia CDM ilitoa kadi kwa wanachama wapya 1836.

Kwa takriban siku tatu sasa Dr Slaa amekuwa gumzo katika wilaya ya Karagwe kutokana na jinsi alivyoiteka wilaya hiyo tangia awasili ambapo kila anapoonekana maelfu ya watu hujipanga na kutamani walau kumshika mkono kama ishara ya kumtakia kila la kheri na kumuunga mkono.

Wachunguzi wa siasa za Karagwe wanasema mikutano ya CDM jimboni humo imevunja rekodi na kwa hakika CCM wilaya imepata hofu kubwa.Katika miji ya Kayanga na Karagwe ilipofanyika mikutano ya CDM wananchi walisimamisha shughuli zote na kuungana na makamanda wa CDM.

Source:Tanzania Daima

Sijui kama kuna watu makini wanajua au wameshajua athari za kuandika CDM badala ya CHADEMA vs CCM. Nimeshtuka sana kuona wapiganaji makini kama molemo na wengine hapa akina fmpiganaji na wengine kibao, wengine hata wameanza kuandika makala kwenye mainstream media, kwa kutumia abbreviation hiyo ya CDM! Hivinkuna chama hicho Tanzania?

Nawaombeni watu makini wote tutumie abbreviation sahihi, CHADEMA. So superb. Nawatakia uwasilishaji mwema wa hoja na mijadala.
 
Ngoja wale wenye hoja Dhaifu utasikia wakisema Mara dr slaa kaoa ooh Mara kibabu mara hana sera mara Josephine hizo ndio hoja za ccm
 
Kama hivyo basi CDM waachane na kupiga kelele ma chama dume waelekeze nguvu zao kwa Chama cha kina Dovutwa.
 
Sijui kama kuna watu makini wanajua au wameshajua athari za kuandika CDM badala ya CHADEMA vs CCM. Nimeshtuka sana kuona wapiganaji makini kama molemo na wengine hapa akina fmpiganaji na wengine kibao, wengine hata wameanza kuandika makala kwenye mainstream media, kwa kutumia abbreviation hiyo ya CDM! Hivinkuna chama hicho Tanzania?

Nawaombeni watu makini wote tutumie abbreviation sahihi, CHADEMA. So superb. Nawatakia uwasilishaji mwema wa hoja na mijadala.
Mkuu tunatumia simu kwahiyo hii ni njia mojawapo ya kuspeedup wakati wa kuandika
 
Huyu babu anajifariji anaujua fika mziki wa gamba, itakuwa aibu kwa maneno haya halafu CDM ije kuangushwa na chama mahututi kwenye chaguzi mbalimbali zijazo.
 
Sijui kama kuna watu makini wanajua au wameshajua athari za kuandika CDM badala ya CHADEMA vs CCM. Nimeshtuka sana kuona wapiganaji makini kama molemo na wengine hapa akina fmpiganaji na wengine kibao, wengine hata wameanza kuandika makala kwenye mainstream media, kwa kutumia abbreviation hiyo ya CDM! Hivinkuna chama hicho Tanzania?

Nawaombeni watu makini wote tutumie abbreviation sahihi, CHADEMA. So superb. Nawatakia uwasilishaji mwema wa hoja na mijadala.

Tumaini Makene

Noted mkuu wangu.Ni kweli huwa na mimi nina kilema hicho.Thanks alot will change.
 
watu wanaohudhuria mikutano hiyo hata ukiwauliza ni mangapi ambayo slaa anaweza kuyateleza zaidi ya kuwachekesha jukwaani ni hakuna, anaweza kujaza watu kwa kuwa anafanya comedian kwani anayoyatamka ni kufurahisha watu tuu na hana mbinu ya kuyatekeleza.
 
Huyu babu anajifariji anaujua fika mziki wa gamba, itakuwa aibu kwa maneno haya halafu CDM ije kuangushwa na chama mahututi kwenye chaguzi mbalimbali zijazo.
Tokea kimeungana na majangili ya kisomali kwenye uongozi kimejishusha sana
 
Mkuu Molemo
Babu bado anamuota Kinana? Anaogopa nini mwambie amwage sera kama anazo mziki wa Kinana hauwezi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Kila nikipita ni kinana tu kila niendapo ni kinana tu,watu hawapati usingizi wanaishia kuimba na kucheza kinana kinana.muziki wake ni munene mno
 
Mzee tangaza sera acha kuhangaika na kinana humuwezi,atakupiga tu penda usipende
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom