masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Wanajamvi heshima kwenu,
Katika hali isiyo ya kawaida chama tawala kimekuwa kimya sana tangu kifo cha kada wake, diwani wa Kisesa, Clement Mabina. Wanajamvi kuna yeyote ameshatoa tamko rasmi (msemaji wa chama) kuhusiana na hili? Tumezoea sana kupata taarifa rasmi kupitia kwa Katibu Mwenezi kwenye vyombo vya habari, kupitia kwenye mitandao na blog mbalimbali hususan ya Michuzi kila mara kunapokuwa na jambo linalohusu viongozi wa chama tawala. Mmepata kigugumizi gani? Ama mnafikiri kwa kukaa kimya tutasahau?
Tulio wanachama wa CCM toka enzi za TANU kulikuwapo na msemo uliokuwa unaaminiwa kama sala miaka hiyo.
CHEO NI DHAMANA.
Tukio la kusikitisha lilotokea eneo la Kisesa nje kidogo ya mjo wa Mwanza, ambalo lilisababisha vifo vya watu wawili lazima liangaliwe katika msimamo unaostahili.
Mpaka sasa tunapata habari kutoka vyanzo vya habari toka sehemu mbali mbali, pamoja na taarifa ya polisi.
Clement Mabina -aliyekuwa Mwenyekiti waCCM wa Mkoa wa Mwanza , mpaka kifo chake, saa 3 au nne hivi asubuhi, alienda kulishughulikia shamba ambalo wananchi wa karibu walikuwa na ugomvi naye , ugomvi wa umiliki wa shamba hilo.
Kosa la kwanza ni kulishughulikia shamba ambalo Mabina ni dhahiri alikuwa na ugomvi na majirani zake.
Pili . wananchi waliokaribu wakahoji ni vipi Mabina aingie kwenye shamba, tena bila kutoa taarifa kwa wagomvi wake na kuendelea kulishughulikia shamba hilo.
Tatu katika inaelekea mabishano na wanakijiji waliohoji , Bwana Mabina aliktumia bunduki aina ya shotgun kumuua mmoja wa wanakijiji aitwae Temeli Malemi, kijana wa miaka 13-14 hivi.
Wana kijiji wakacharuka na kujichukulia hatua ya kumpopoa muheshimiwa huyu mpaka mauti.
Kwa wanaouelewa mkoa wa Mwanza , jiwe ni a weapon of choice, huendi mita moja bila kukuta jiwe l aina yoyote.
CHEO NI DHAMANA, na mwenzetu huyu hatuna haja ya kumhukumu lakini alitumia cheo chake bila ridhaa ya waliomuweka madarakani-wananchi.
Mbaya zaidi yaliyofanyika na mwenzetu huyu ni masuala ya JINAI, masuala ambayo CCM hairidhii wala haikumtuma.
Ametumia ubabe, na ubabe wa wanachi umedhihiri.
Ni kwa vile nchi hii ni ya sheria , lakini CCM kujihusisha na tabia za namna hii ni kujitakia kifo.
CCM lazima ijitenge na kifo cha mwenzetu huyu, ambaye alitumia dhamana yake vibaya.