CCM ni lazima ibadilike chaguzi za 'Kitemi' zimepitwa na wakati, Rais Samia yuko sahihi kukijenga upya chama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,761
CCM itaendelea kutegemea dola ili ishinde uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hadi lini?

CCM itaendelea kutegemea mbeleko ya Wakurugenzi na wakuu wa wilaya hadi lini ilhali katika uhalisia mioyo ya wapiga kura huwezi kuisemea wala kuiamulia?

Ni wakati sasa CCM ijijengee uhalali wa kuchagulika kidemokrasia na kukubalika mioyoni mwa wananchi.

Tumpe nafasi mwenyekiti mama Samia akitengeneze chama

Hayati Magufuli alikuwa na approach yake ambayo imetujazia akina Babu Tale bungeni.
Tumwache mama Samia afanye mabadiliko stahiki ili kuendana na maono ya uongozi wake.

Eid Mubarak!
 
Mama Samia anaweza kuirudisha CCM kwenye Mioyo ya Wananchi, arudishe mchakato wa Katiba mpya na Tume HURU ya Uchaguzi
 
Kila awamu ya urais inafanya jambo kubwa kuiimarisha CCM

Hapa tulipofikia hata wana Jf kuungana kuijenga tanzania moja nimeanza kuilewa ile kauli mbiu isemayo "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"

CCM miaka200 tena💣💥🙏
 
Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kati ya ccm ya mwenda zake na CCM ya Mama yetu. Mabadiliko yaliyotokea kwenye mifumo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni kama zilikuwa CCM mbili tofauti.
 
Uchumi gani unaongelea?

Kwa wenzetu wangekuaj na data hata. Ngoja tukusikilize zaid.
 
Usitukumbushe machungu tulipo toka, acha twende na mama lazima aongezewe atake astake
 
Mwendazake alikuwa jembe, hawa wa sasa hata siwaelewielewi. Nikikumbuka zaidi ya 400m zilizoliwa bure na mashabiki wa Simba na Yanga uwanjani napata kichefuchefu.
 
Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kati ya ccm ya mwenda zake na ccm ya Mama yetu...mabadiliko yaliyotokea kwenye mifumo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni kama zilikuwa CCM mbili tofauti.
Hao ccm sasa
JamiiForums-617387687.jpg
 
Back
Top Bottom