Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Kajitathmini kagundua kuwa amejaa uovu na dhambi (ufisadi), kikaamua kuokoka (kujivua gamba). Katika mfano huu nichukulie gamba lililofanikiwa kutoka kama ulevi wa kileo cha valuu (Rostam).
Cha kushangaza, wakati 'mlokole' wetu huyu aliyezaliwa upya (japo dhambi zingine za uzinzi, wizi zimekuwa ngumu kuziacha), akituletea juice kama kinywaji mbadala kwa valuu, anaitumia chupa ile ile ya valuu kuchukulia juice (Kafumu)!!!
Kitendo cha CCM kumtumia Rostam kumuombea ubunge Kafumu, ni sawa na mlokole kutumia chupa ya valuu kumnywesha mtoto juice...
Lakini kwa upande mwingine tujiulize, Kafumu ni juice kweli? CCM ni mlokole kweli? Ana wabunge zaidi ya 200, je ameshindwa kuujaribu 'ulokole' wake kwa kuamua kufa shahidi, kwa kumkataa Rostam na mambo yake yote, hata kama jimbo litapotea? Hivi umuhimu wa Rostam ni kwa ubunge wa Igunga pekee au bado 'mnae' chamani? Ndani ya CCM Rostam ni taasisi ambayo ndani yake wapo wengi (Lowassa, S. Simba, Lusinde, Makinda, + viongozi wengine na wabunge zaidi ya 50). Hivi CCM, mmeokoka kweli?
Samwel Sitta, C. Sendeka, A. Kilango, H. Mwakyembe, hivi kweli mmeogopa kumkataa Rostam na mambo yake yote, na fahari zake zote, na mamlaka yake yote? mmejidharau kiasi hicho? Nilidhani nyie ndiyo chupa ya 'orange juice' ambayo ingetumika kutunywesha kakinywaji ketu kapya (Kafumu). Nilitegemea muongoze mapambano Igunga! Sasa mipaka yenu ni wapi, majimboni kwenu tu? Kama nyie mmezuiwa kwenda Igunga, nambieni Rostam amezuiwa kwenda wapi? Mamlaka yenu nyie yako wapi hasa? Kyela, au Urambo?
Ni jambo la kawaida siku hizi kuona mtu anayejitangaza kuokoka, lakini chumbani kwake na usiku 'akajikumbusha' kidogo ka-valuu, lakini mchana akailaani pombe kwa kifungu cha maandiko ...'ole wake ampaye mwenzie kileo'... Kwa CCM nisingeshangaa kama mngeendelea kumtumia Rostam 'ndani kwa ndani' huku kwa nje mkituhadaa kuwa gamba limetoka. Lakini kitendo cha kutoka chumbani kwenda kumnywesha mtoto juice hadharani mkitumia chupa ya valuu, kinatufanya mtuulize hata hiyo mnayotunywesha ni juice au ni Valuu?
Na je, ina maana hamtumii kinywaji cha aina nyingine ndani mwenu kiasi kwamba hamkupata chupa nyingine?
Oneni sasa 'juice' mnayotunyesha imejaa harufu na ladha valuu!!! Hata hatujui tena labda ni kuwa imechanganyika na valuu iliyobaki humo ndani, au juice yenyewe nayo ni valuu ikatiwa tu sukari!!!
Aaah, tupa kule...