CCM ni kama mlokole anayetumia chupa ya valuu kumnywesha mtoto juice!

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,296
Kajitathmini kagundua kuwa amejaa uovu na dhambi (ufisadi), kikaamua kuokoka (kujivua gamba). Katika mfano huu nichukulie gamba lililofanikiwa kutoka kama ulevi wa kileo cha valuu (Rostam).

Cha kushangaza, wakati 'mlokole' wetu huyu aliyezaliwa upya (japo dhambi zingine za uzinzi, wizi zimekuwa ngumu kuziacha), akituletea juice kama kinywaji mbadala kwa valuu, anaitumia chupa ile ile ya valuu kuchukulia juice (Kafumu)!!!

Kitendo cha CCM kumtumia Rostam kumuombea ubunge Kafumu, ni sawa na mlokole kutumia chupa ya valuu kumnywesha mtoto juice...

Lakini kwa upande mwingine tujiulize, Kafumu ni juice kweli? CCM ni mlokole kweli? Ana wabunge zaidi ya 200, je ameshindwa kuujaribu 'ulokole' wake kwa kuamua kufa shahidi, kwa kumkataa Rostam na mambo yake yote, hata kama jimbo litapotea? Hivi umuhimu wa Rostam ni kwa ubunge wa Igunga pekee au bado 'mnae' chamani? Ndani ya CCM Rostam ni taasisi ambayo ndani yake wapo wengi (Lowassa, S. Simba, Lusinde, Makinda, + viongozi wengine na wabunge zaidi ya 50). Hivi CCM, mmeokoka kweli?

Samwel Sitta, C. Sendeka, A. Kilango, H. Mwakyembe, hivi kweli mmeogopa kumkataa Rostam na mambo yake yote, na fahari zake zote, na mamlaka yake yote? mmejidharau kiasi hicho? Nilidhani nyie ndiyo chupa ya 'orange juice' ambayo ingetumika kutunywesha kakinywaji ketu kapya (Kafumu). Nilitegemea muongoze mapambano Igunga! Sasa mipaka yenu ni wapi, majimboni kwenu tu? Kama nyie mmezuiwa kwenda Igunga, nambieni Rostam amezuiwa kwenda wapi? Mamlaka yenu nyie yako wapi hasa? Kyela, au Urambo?

Ni jambo la kawaida siku hizi kuona mtu anayejitangaza kuokoka, lakini chumbani kwake na usiku 'akajikumbusha' kidogo ka-valuu, lakini mchana akailaani pombe kwa kifungu cha maandiko ...'ole wake ampaye mwenzie kileo'... Kwa CCM nisingeshangaa kama mngeendelea kumtumia Rostam 'ndani kwa ndani' huku kwa nje mkituhadaa kuwa gamba limetoka. Lakini kitendo cha kutoka chumbani kwenda kumnywesha mtoto juice hadharani mkitumia chupa ya valuu, kinatufanya mtuulize hata hiyo mnayotunywesha ni juice au ni Valuu?
Na je, ina maana hamtumii kinywaji cha aina nyingine ndani mwenu kiasi kwamba hamkupata chupa nyingine?

Oneni sasa 'juice' mnayotunyesha imejaa harufu na ladha valuu!!! Hata hatujui tena labda ni kuwa imechanganyika na valuu iliyobaki humo ndani, au juice yenyewe nayo ni valuu ikatiwa tu sukari!!!

Aaah, tupa kule...
 
Hurricane

Member
Aug 5, 2011
52
13
Sijui kama wenzako watakuelewa katika fumbo hili. Mie nimekupata vizuri mzee. Hiyo bado ni valuu, imetiwa sukari tu mkuu.
 
Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
Makundi haya mawili sasa yamenuniana. Kundi la akina SIX linasema waacheni wahangaike wenyewe huko ingunga na wanatamani hata kuitwa kusaidia upinzani. Kundi la pili linapambana kuzuia aibu iliyoko mbele yao ikiwa jimbo litaenda upinzani.

Kama jimbo litaenda upinzani huenda kundi la SIX likafikiria mara ya pili ile move ya CCJ, yetu macho.

Mimi ninafurahi maana hata wapinzani wakipoteza Igunga haitauma kama CCM ikipoteza wapinzani watawacheka sana CCM kwa kijasho walichowatoa hata kama watarejesha jimbo.

Cha kufurahisha ni kwamba CCM hawajiamini tena katika chaguzi zilizoko mbele yao.
Nadhani tutaona tofauti kubwa sana kwenye bunge lijalo maana itakuwa imetoa fundisho kali kwa wabunge wa CCM ya kwamba wamekalia kuti kavu 2015 ambalo linaweza kukati tu hivyo washiklie kwa makini sana. Nitafurahia sana maana najua wabunge wengi watafuata upepo wa wabunge CDM. Lakini hii inamaanisha nini kwa serikali sasa? Inamaana maadui wawili wataikabili serikali ambao ni wabunge wa CCM wenyewe na Upinzani.

Chadema gogogogogogogogogogogogoogogogogoogogo....... you guys are making us proud!
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Thread nyingine kama zingekuwa hazina neno CCM zisingestahili kuwa humu. Lakini ndiyo hivyo tena!
 
Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Makundi haya mawili sasa yamenuniana. Kundi la akina SIX linasema waacheni wahangaike wenyewe huko ingunga na wanatamani hata kuitwa kusaidia upinzani. Kundi la pili linapambana kuzuia aibu iliyoko mbele yao ikiwa jimbo litaenda upinzani.

Kama jimbo litaenda upinzani huenda kundi la SIX likafikiria mara ya pili ile move ya CCJ, yetu macho.

Mimi ninafurahi maana hata wapinzani wakipoteza Igunga haitauma kama CCM ikipoteza wapinzani watawacheka sana CCM kwa kijasho walichowatoa hata kama watarejesha jimbo.

Cha kufurahisha ni kwamba CCM hawajiamini tena katika chaguzi zilizoko mbele yao.
Nadhani tutaona tofauti kubwa sana kwenye bunge lijalo maana itakuwa imetoa fundisho kali kwa wabunge wa CCM ya kwamba wamekalia kuti kavu 2015 ambalo linaweza kukati tu hivyo washiklie kwa makini sana. Nitafurahia sana maana najua wabunge wengi watafuata upepo wa wabunge CDM. Lakini hii inamaanisha nini kwa serikali sasa? Inamaana maadui wawili wataikabili serikali ambao ni wabunge wa CCM wenyewe na Upinzani.

Chadema gogogogogogogogogogogogoogogogogoogogo....... you guys are making us proud!

Inasemekana kuwa kundi la akina SIX linafanya kila wawezalo kuhakikisha jimbo halichukuliwi na CCM. Sababu ni kuwa walikuwa wameplan kuonyesha nguvu zao Igunga kwa kwenda kuweka mgombea wao na kuongoza kampeni lakini wakazidiwa nguvu na wapambe wa Rostam, hivyo chama kikaamua kiwape kina Rostam nafasi. Kinachowauma kina Sitta ni kuwa endapo CCM itashinda then utakuwa ushindi kwa team inayomsapoti Lowassa for 2015.

Hii ndiyo maana Nape alitaka akina Sita ndio waende Igunga akakataliwa, na hata yeye akakatazwa kwani timu inayocheza huko siyo timu yake.
 
Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,591
434
Ngoja uchaguzi uishe uone kitu CCM watamfanya Rost-Tam, hataamini....kutumikia CCM ni sawa na kutumikia Freemason..ipo siku tu watakufanya kweli.....
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom