CCM ni kama mchawi na mganga

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Wakati nasoma shule ya msingi shemeji yangu alikuwa anapenda kutusimulia hadithi mbalimbali..

moja ilikuwa kuhusu tabia ya mtu aliyekubuu kwenye ukwapuaji, au mwizi..alipenda kutuambia mwizi akikosa kitu cha kuiba, ataenda mahali fulani pasipokuwa na watu, halafu atavua shati lake na kuliweka njiani,kisha atajificha na kuanza kuotea lile shati lake huku akitazama pande zote kama hakuna mtu kisha anakuja mbio analikwapua na kujificha kichakani.

Pili alipenda kusimulia kuhusu mchawi na mganga wa miti shamba, kwamba hawa watu wawili wanajuana sana. hivyo mganga ataenda kwa mchawi na kumwambia loga halafu nitatibu halafu mbuzi tutagawana au pesa tutakazopata..
kwahiyo mchawi angeloga halafu mganga anatibu.

Hivi ukijiuliza majipu yanayotumbuliwa yamezalishwa na serikali ya chama gani? jibu ni ccm. Je hao watu wachache wanaolaumiwa leo na wananchi kuaminishwa kwamba mwokozi wao amefika walikuwa chini ya uongozi wa serikali ya chama gani? jibu ni ccm. Je hao viongozi wabadirifu ni zao la chama gani? jibu ni ccm

Hivi leo ccm wanataka watuambie sasa wamebadilika wamekuwa walokole na waislamu safi kiasi cha kuwaonea wananchi huruma? Je hii siyo mbinu ya mchawi na mganga ya kuloga na kutibu halafu mganga anaonekana mwema kumbe wananjama moja? ukitafakari kwa undani utagundua ccm wanacheza na saikolojia ya watanzania ila hawana huruma na wananchi hata kidogo. Labda kama wataomba radhi maana waliitetea sana serikali ya awamu ya nne na kusema kwamba imeleta maendeleo, leo hotuba ya Rais kila wakati inaonyesha kwamba awamu ya nne imewatesa watanzania na kuwanyonya sana.
 
Back
Top Bottom