getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,812
Nimetafakari kwa kina baada ya kuurudia huu wimbo kichwani kwangu mara kadhaa
Ccm ni ile ile, hata atokee kiongozi mwenye maono mazuri kiasi gani bado Ccm ni ileile baada ya muda itarudi kulekukule..
Nimemuona Polepole kule Monduli akimpokea Lowasa mwili ulikuwa pale lakini ninaamini kabisa nafsi yake yamkini haikuwa pale, bila shaka ilikua umbali mrefu sana ikibebwa na tafakuri.kadhaa ndani yake,
Nimejaribu kuvuta picha ya Mh Balozi W Slaa huko aliko nikawaza picha aliyo nayo kichwani kwake kwa wakati huu.
Nikavuta taswira Ya Watanzania waliokuaa wameanza kuiamini Ccm na kujivunia ubora wake hisia zao baada ya ugeni ule wa monduli na mbwembwe zake.!
Nikajikuta taratiibu ninaanza hatua za kujisogeza kando na chama hiki kikongwe barani Afrika, taratiibu mapenzi yaliyo anza kuchipua kwa chama hiki naona yanaanza kufifia na kuvunjika moyo naamini hali hii itawakuta vijana wengi sana walio amua kuiunga mkono Ccm wakiamini ni safi
Sitashangaa harakati za akina.
Kafulila, Machali, Kisandu, na wengine wengi zikizaliwa upya ndani ya Ccm na hii itakuwa ni CCM B au CCM academia..
Zao la vijana wanaoitakia Mema Nchi hii bila shaka kutakuwa na Vuguvugu fulani jipya ndani ya CCM, Muda ni hakimu mzuri..
Sent using Jamii Forums mobile app