CCM ni chama SIASA

kilulu

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
282
225
Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine kama CHADEMA ,CUF , NCCR n.k, CCM wamekuwa wakibeza sana muungano wa hivi vyama 3 vilivyoungana, swali ni je, wao hawawezi kuungana na ACT, TLP kuunda nguvu ya umoja wao?

Kwa kuwa ni chama kinachoshika dola hakiwezi kuwa na umoja wao na ACT na TLP? ama CCM wameishiwa sera ndo maana wanaibeza UKAWA?

Nawasilisha.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
20,411
2,000
ngumu kumeza!!

Umoja wa Kutetea Serikali Mbili - UKUSEMBI.

Umoja huu unaundwa na vyama vya CCM, ACT, TLP na UPD.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine kama CHADEMA ,CUF , NCCR n.k, CCM wamekuwa wakibeza sana muungano wa hivi vyama 3 vilivyoungana, swali ni je, wao hawawezi kuungana na ACT, TLP kuunda nguvu ya umoja wao?

Kwa kuwa ni chama kinachoshika dola hakiwezi kuwa na umoja wao na ACT na TLP? ama CCM wameishiwa sera ndo maana wanaibeza UKAWA?

Nawasilisha.
CCM tumeshaungana na CUF kule Zanzibar
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Wapi? Kama ni Tanzania CCM bado inakubalika sana.

Sidhani hata wewe kama unaamini hayo maneno. Ukweli ni kwamba kama CCM ingekuwa inakubalika hivyo unavyotaka watu waamini, wala msingekuwa mnahangaika kubeba watu na malori kuhudhuria mikutano. Wala msingekuwa mnaiba kura, ya nini kuiba, si mnapendwa? Subirini wawapigie! Na wala kusingekuwa na haja ya kulazimisha ushindi kwa kutumia Tume ya uchaguzi, polisi, jeshi na Usalama. We unaonaje? Mi naona hata wewe unaona na unajua ni kiasi gani hampendwi.

Kama mnakubalika, acheni kulazimisha watoto wa shule na wafanyakazi wa serikali kwenda kwenye mikutano yenu na msipeleke malori muone ni watu wangapi wanakuja mikutanoni. Na kama kweli mnapendwa na kukubalika, jileteni kwetu kama CCM, acheni kuiba kura wala kubebwa na polisi. Acheni kupiga watu mabomu na risasi halafu muone mnapata kura ngapi! nakuhakikishia kupata kura 5000 kwa nchi nzima itakuwa shida!
 
nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,395
2,000
ccm siipendi sitakujakuipenda kabisa, na wakija na jezi zao ofisini huwa naondoka naenda kunywa chai
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
ngumu kumeza!!

Umoja wa Kutetea Serikali Mbili - UKUSEMBI.

Umoja huu unaundwa na vyama vya CCM, ACT, TLP na UPD.
Taja vyote mbona vingine umeacha kifupi ni kwamba vyama vyote vilivyosajiliwa vinataka serikali mbili ukiacha nccr,cuf na kadima ndiyo wanataka serikali tatu.
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Sidhani hata wewe kama unaamini hayo maneno. Ukweli ni kwamba kama CCM ingekuwa inakubalika hivyo unavyotaka watu waamini, wala msingekuwa mnahangaika kubeba watu na malori kuhudhuria mikutano. Wala msingekuwa mnaiba kura, ya nini kuiba, si mnapendwa? Subirini wawapigie! Na wala kusingekuwa na haja ya kulazimisha ushindi kwa kutumia Tume ya uchaguzi, polisi, jeshi na Usalama. We unaonaje? Mi naona hata wewe unaona na unajua ni kiasi gani hampendwi.

Kama mnakubalika, acheni kulazimisha watoto wa shule na wafanyakazi wa serikali kwenda kwenye mikutano yenu na msipeleke malori muone ni watu wangapi wanakuja mikutanoni. Na kama kweli mnapendwa na kukubalika, jileteni kwetu kama CCM, acheni kuiba kura wala kubebwa na polisi. Acheni kupiga watu mabomu na risasi halafu muone mnapata kura ngapi! nakuhakikishia kupata kura 5000 kwa nchi nzima itakuwa shida!
Haya maneno yatakutokeeni puani na rafiki zako kaaeni chonjo ccm hii ya kinana mtajuta kuijua watanzania wengi wenye akili wanaiamini sana ccm wewe unaropoka tu.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Haya maneno yatakutokeeni puani na rafiki zako kaaeni chonjo ccm hii ya kinana mtajuta kuijua watanzania wengi wenye akili wanaiamini sana ccm wewe unaropoka tu.

Data na ushahidi vingeleta uzito wa hoja yako. Maneno peke yake hapana....bado
 
kilulu

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
282
225
Haya maneno yatakutokeeni puani na rafiki zako kaaeni chonjo ccm hii ya kinana mtajuta kuijua watanzania wengi wenye akili wanaiamini sana ccm wewe unaropoka tu.

ndugu kivipi tena watajuta au unataka kutuamisha nakudhihirisha kuwa CCM ni chama cha Kigaidi, kikosolewa kinaanza kuhenyesha raia wake walokiweka madarakani.kama ndo hivyo CCM kinakosa mvuto. Raia watakihama si mda mrefu,swali langu ni je, nivibaya kwa CCM kuungana na vyama vingine vya kisiasa wakawa na
muungano wao kama UKAWA?
 
ngorope

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
1,112
0
Taja vyote mbona vingine umeacha kifupi ni kwamba vyama vyote vilivyosajiliwa vinataka serikali mbili ukiacha nccr,cuf na kadima ndiyo wanataka serikali tatu.

Vyama hivyo vinawakilisha asilimia ngapi ya wananchi maana serikali 3 ni maoni ya wananchi na sio vyama vya siasa
 
ngorope

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
1,112
0
Ofisi yenyewe mnauza bangi na unga mda wote mko juujuu kuhofia kukamatwa.

Mkuu usitoke nje ya mada kanusha hoja kuwa hamtembezi jezi maofisini ikiwezekana weka na ushahidi ili jamaa aumbuke kukimbilia kashfa ni picha ya upeo mdogo wa kulinda hoja
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom