Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 13,036
- 30,565
Ili jamii yoyote iweze kupata maendeleo ni lazima iwekeze kiasi kikubwa kuliko inavyotumia. Serikali ya CCM kwa muda mrefu imekuwa ni ya kutumia siyo kuzalisha. JK alikwishawahi kutamka kuwa, 'sisi ni maskini na huko nje kuna pesa nyingi tu, unachotakiwa ni kueleza matatizo yako, wakikuelewa wanakupa pesa'. JK anachojua ni kutumia, wazalishaji wapo nje ya Tanzania. Kwa sasa kila mtanzania ni vema akajua kuwa tupo katika vita, vita ya kuondoa mfumo wa utawala wa ulaji.
Ili ushinde vita yoyote ile ni lazima uwe na makamanda imara, makamanda wenye upeo, makamanda wenye ujasiri, makamanda wenye falsafa moja na wapiganaji wao, makamanda wenye akili na utashi, makamanda watakaowaunganisha wapiganaji wote wawafuate nyuma yao wakiwaongoza kwenye vita vya ushindi. Vita yetu kubwa kwa sasa ni kubadilisha mfumo wa utawala 'ulaji' ili tupate mfumo wa utawala wa 'uzalishaji' LAKINI tunatumia makamanda wanaoamini falsafa ya 'ulaji', hapa hatuwezi kushinda kwa sababu adui yetu namba moja ni makamanda wanaotuongoza. Ndiyo maana nasema adui yetu mkubwa wa maendeleo ni CCM na taasisi zake ambazo zimejengwa katika falsafa ya 'ulaji', hatua yetu ya kwanza kuelekea kwenye maendeleo ni kuiondoa CCM katika uongozi, bila ya hilo kutokea jitihada zetu zote haziwezi kuleta mafanikio makubwa. Japo uchaguzi umekwisha lakini kwa wanaoitakia mema Tanzania ni lazima wahakikishe kila dakika inayopita kuna jitihada za kuhakikisha CCM ipo katika njia ya kutoka katika mamlaka ya kuwatawala watanzania.