CCM ni chama kinachoweza kumuwajibisha yeyote wa nyadhifa yoyote wakati wowote bila kupata mpasuko!

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
Leo asubuhi nilipokuwa katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa katika kituo maarufu cha televisheni cha Star TV ya jijini Mwanza kwenye mada iliyokuwa inahusu uwajibikaji. Nilizungumza juu ya maana halisi na upana wa dhana ya uwajibikaji. Nikaugawa katika maeneo tofauti, kwa mwananchi, kwa chama na kwa serikali. Na Kwamba uwajibika unatokana na wajibu umpasao mtu kuutekeleza na akishindwa kuutekeleza wajibu huo dhana hii inamtaka kujitathimini na kukiri kuwa hana uwezo na ameshindwa kuutekeleza hivyo anawajibika kwa kujiuzulu ama kwa namna nyingine.

Lakini mmoja wa wachangiaji Ndugu Marcus Albano mwanaharakati na mkereketwa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alikishutumu Chama changu, chama makini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa hakiwajibishi wanachama wake na viongozi wake pale wanapothibitika kuwa wamekosea na wameshindwa kuutekeleza wajibu husika.

Shutuma hii ilinipasa niijibu, na niliijibu kwa sababu na namna mbili:

i) Moja si kweli kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwajibishi wanachama ama viongozi wake, hivyo shutuma hiyo sio ya kweli.

ii) Pili ni wazi kuwa mwanaharakati huyo na mwanachama wa Chadema hafahamu historia ya Chama Cha Mapinduzi, kwa maana hajui kabisa kuwa hata dhana yenyewe ya uwajibikaji imeasisiwa na Mwalimu Nyerere ambae ni muasisi wa CCM na kuiwekea CCM misingi ya uwajibikaji kwa maandiko na mfumo.

Nikaona kulisema hili kwenye TV pekee haitoshi bali nililete hapa ili kama kuna yeyote mwenye ku-challenge hilo ajitokeze, CCM imewahi katika historia yake kumuwajibisha MAKAMU MWENYEKITI wa chama ambae pia alikuwa ni RAIS wa NCHI na chama hakikutingishika wala kupata mpasuko wa aina yeyote, lakini utaratibu huo umeendelea siku zote na hata hivi karibuni kimemvua uanachama mmoja wa makada wake wakubwa walioshika nyadhifa kubwa katika Chama na Serikali kule Zanzibar Ndugu Mansoor.


TOFAUTI iliyopo baina yetu na vyama vingine ni kwamba CCM tunafuata na kuisimamia dhana hii ya UWAJIBIKAJI kwa maslahi mapana ya Chama na Serikali kwa maana ya UTAIFA na wenzetu wa vyama vingine wanajaribu kulifanya hili kwa maslahi ya mtu, ama kikundi cha watu na kwa sababu za madaraka, woga na ubaguzi.

Naomba kuwasilisha.
 
hakuna chama cha maana kama ccm vingine ni vyama vya kilaghai tu.
 
Tangu nianze kufuatilia siasa bado nashawishika kuamini kuwa ccm ni chama ambacho kitakuwa na mda mwingine wa kuaminiwa na watu kwa kipindi kijacho kwa kufanya mambo makubwa.
 
Uwajibikaji ndani ya ccm ulikuepo enzi za Mwalimu sio sasa hivi.
ndani ya ccm ya sasa hayupo wa kumnyoshea kidole hadharani mwenzio kila mmoja anamapungufu yake.

Ndio hata leo zimetafunwa bilioni 600 kwenye serikali za mitaa lakini ajabu hakuna aliewajibishwa hata mmoja wakati walaji wanajulika kwa majina na nyadhifa zao.

mfumo wa kuwajibishwa waachieni chadema, ccm mkianza kuwajibishana msishangae na Rais mwenyewe inabidi awajibishwe hivyo serikali nzima kuanguka.!!!
 
Ccm ni mfano ulio hai kwa vyama vya siasa nchini. Wakitaka wasitake ndio chama chenye nguvu na misingi imara ya kukifanya kidumu miaka 100 ijayo.
 
wez.wauza madawa ya kulevya.walala bungeni. mafisadi...wamewajibishwa?nataka majibu kwa sababu yule mzee Mangula alisema atawatimua mafisadi na waliotoa rushwa kwenye uchaguzi ndani ya chama
 
umetumiaje neno "nyadhifa" instead of "wadhifa"
Hii ishara dhahiri ya ulaghai.
 
Huyu nae ni kama ndomu tu ambayo bado haijapasuka kama ZZK. Vipi yale Magamba bado yameng'ang'ania kiunoni au yameshuka kidogo?
 
mi nadhani kama ccm wanajiamini wamvue Lowassa ujumbe wa kamati kuu tuone....mleta mada analeta mambo ya enzi za mwalimu...ccm kuna mizigo....timua yote hayo tuone uwajibikaji wenu....mleta thread kakurupuka hana UPDATES
 
mi nadhani kama ccm wanajiamini wamvue Lowassa ujumbe wa kamati kuu tuone....mleta mada analeta mambo ya enzi za mwalimu...ccm kuna mizigo....timua yote hayo tuone uwajibikaji wenu....mleta thread kakurupuka hana UPDATES
Kama Lowasa atakiuka misingi yamchama, anaweza kuchukuliwa hatua
 
Mkuu vipi kuhusu magamba yaliyong'ang'ania kiunoni shoka bado haijapatikana nendeni mkaazime chadema iliyowafyeka zzt nk
 
Jokes aside!!!

Hivi suala la kuvua gamba liliishia wapi? ????

Na mi ndo napenda kujua ilikuwaje?au gamba ni moja tu yule mbunge wa zanzibar.....bila aibu wanaongea vitu hawawez kutekeleza... unamfukuza dagaa unaacha mapapa...yatawameza 2015
 
mi nadhani kama ccm wanajiamini wamvue Lowassa ujumbe wa kamati kuu tuone....mleta mada analeta mambo ya enzi za mwalimu...ccm kuna mizigo....timua yote hayo tuone uwajibikaji wenu....mleta thread kakurupuka hana UPDATES

Hivi Uwaziri Mkuu wa Lowasa aliwajibika enzi za Mwalimu?
 
Back
Top Bottom