CCM ni Chama kinachoumiza wananchi wake. Hili dubwasha likipigwa, Wananchi watashusha pumzi na watafurahia maisha

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Wiki iliyopita, kuna jirani yangu mwanaye alipata ajaliya pikipiki, Yule kijana aliumia si saana.

Alienda hospital ya wilaya, akatibiwa na kupewa dawa, Usiku wa siku hiyo akiwa nyumbani amelala, alihisi maumivu makali sana, akaamua kumeza Diclopar nne na panaldo mbili ili kutuliza maumivu.

Alipomeza zile dawa kwa nia ya kutuliza maumivu, zile dawa zilimzidia ikabidi akimbizwe hospital kwa matibabu zaidi, hata hivyo hakuweza kulazwa pale wilayani, akapewa lufaa Mhimbili.

Alifika Hospital ya Mhimbili akapewa kitanda siku hiyo, alipewa dawa kiasi na kupewa vipimo vidogovidogo, na baada ya usiku huo mmoja, asubuhi yake muda wa saa tatu asubuhi, akafariki yule kijana

Basi taratibu za ndugu kuutoa mwili wa Marehemu hapo hospitali zikaanza, Na kwa sababu hiyo, ikabidi sasa waletewe zile bili za matibabu.

Walichokishangaa ni kuona bili ya Laki sita, na waliambiwa, bila ya kulipa hizo gharama, maiti haitatoka hapo, ndugu wakajichangisha hukuhuku na huku wakapata laki nne.

bado walikataliwa, mmoja wa wanandugu akajitolea dhamana ya leseni yake ya udreva akaiacha Mhimbili

Mimi kilichonishangaza ni kwba, Bili ya laki sita ilitoka wapi, wakati ndugu wa marehemu wanasema, kwanza mtu wao hakuoata huduma ambazo zingeweza kufikisha bili kubwa kama hiyo kwa siku moja,

lakini pia, msinamo wa Raisi wetu, ni pale mtu anapofariki, Asilipishwe pesa isipokuwa kuwepo utaratibu mwingine

Licha ya agizo la mh Raisi, hakuna kinachotekelezwa na wasaidizi wake

Ni wakati umefika kiukweli bila kupepesa macho, CCM itoke madarakani, kwani inakandamiza watu, Inafanya wizi na ufisadi wa fedha za walipa kodi bila kuwajibishwa hayo majizi, lakini haitoshi, wananchi wanapohitaji huduma ambazo kiukweli zimechangiwa na nguvu za wananchi kupitia kodi mbalimbali, cha ajabu wanapohitaji hizo huduma, wanakwenda kuibiwa tena kwa kile kidogo walichonacho

CCM, hapana
 
Hofu ya baadhi ya wananchi kuhofia amani ya nchi yetu pindi CCM iking'ooka madarakani ni za kishamba sana

Wananchi waelewe, kama ilivyo majumbani mwao katika mpangilio wa vyakula, kwamba, haiwezekani mtu uwe unakula kila siku ugali na magarage, Utakula leo lakini kesho utahitaji ule mchanganyiko wa chakula kingine, ndio mwili unakuwa na nguvu na kinga mbalimbali za magonjwa zinaongezeka mwilini

Ndivyo ilivyo kwenye siasa, Kwamba, maana ya upinzani, ni kushindana kwa namna bora ya kuongoza nchi na kubuni mbinu mbalimbali ili hatimaye tufike kule tuendako

Na sasa ni dhahili kabisa, wakati huu, Tanzania inahitaji chama kingine kuiongoza nchi yetu, sisemi kwa maana ya CCM labda imechoka, hapana, ila imeishiwa mbinu bora, kingine hawa watu wanaendesha nchi yetu kwa mazoea makubwa,

Kuzoeana huko, ndiko kunakotufanya ama nchi tusitoke kwemye lindi la umasikini, ndugu zanguni, inauma sana hasa kwa watu wenye uchumi wa chiiiini kabisa, CCM haiwapelekei huduma Bora, Licha ya hivyo, wanapohitajika kuzifuata huduma nzuri, hufanywa kama mtaji wa Maccm, wanafyonzwa vibaya sana, inawalazimu kuuza mifugo yao mingi ili kukidhi mahitaji hayo na kubaki kuwa masikini wa kutupwa kabisa

CCM kwa ujumla, hsijawahi kusimamia matamko ya kiongozi mkuu, Kiongozi mkuu kwa maana ya Raisi, akisema, sasa basi utozaji fedha kwa wafu, hiyo kauli inakuwa inaelea hewani, sasa huku ndiko kuzoeana na hawawezi kuwajibishana

CCM ndio imeitia umasikini mkubwa nchi hii, Fedha huibwa na watendaji wake, lakini hakuna hata anayewajobishwa, Mf mdogo ni zile fedha zilizopotea Pale BoT kwa baadhi ya wafanyakazi kujilipa posho zisizo na sababu na hakuna aliyewajibika kuhusu ufisadi huo

Tunaposema kwamba CCM kwa sasa haifai tena kuongoza hii nchi, wananchi waelewe, Na tunapoamua kubadirisha chama, Tunataka tuone mpishi mwingine, Je yeye atakuja na aina ipi ya mapishi?

CCM hiyohiyo, ilipata kiongozi mwenye kuchukia rushwa, anayefuatilia kila fedha inavyotumika, lakini ona alivyochukiwa na haohao CCM, maana yake ni kwamba, hiki chama na wizi wa Mali za umma ni sawa na samaki na maji
 
CCM ni shida
 
Back
Top Bottom