CCM ni chama kikubwa walikuwepo Mwigullu, January na Nape wakapita sasa tunao akina Waitara, Joketi na Kafulila nao watapita!

Sema ukubwa wa dola sio cccm
Tunakumbushana tu ukubwa wa CCM maana vijana wa siku hizi wengi ni wasahaulifu.

Unapoteuliwa kuwatumikia wananchi basi uwe mzalendo wa kweli na utoe utumishi badala ya kutumia muda mwingi kujipigia promo na kuchafua watu wengine kana kwamba wewe ndio CCM peke yako.

Hebu muangaliwe January......mtoto wa " kuzaliwa" wa Katibu mkuu mstaafu wa CCM ambaye ni luteni mstaafu wa jeshi......kadhalika January amefanya kazi Ikulu kama mwandishi wa hotuba za Rais, amekuwa Naibu waziri, Waziri na mjumbe wa sekretarieti ya CCM akiwa boss wa foreign affairs......Leo hii ameshasahaulika kiasi cha kuhofia hata kugombea ubunge.

Kiukweli CCM ni chama kikubwa sana na kila kitabu kina zama zake hivyo vijana wa digitali msijisahau.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom