CCM ni Chama chenye uwezo thabiti wa kuiongoza Dola ya Tanzania

Azizi J Hamad

JF-Expert Member
Sep 20, 2020
442
230
Jambo kubwa nililojifunza kutoka Chama Cha Mapinduzi, ni kuwa ni Chama chenye uwezo thabiti wa kuiongoza Dola ya Tanzania, kwa maana kimejipanga vizuri katika kila nyanja. Mathalani ukiangalia kwenye Ilani yao ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, kwenye Kifungu cha 251(e) ukurasa wa 299.

(e)Hatua nyingine muhimu kwa Chama katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ni kuhakikisha kuwa, Chama kinatenga siku maalum kila wiki ili kisikiliza kero za wananchi na kuzifikisha serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Na tukifuatailia kwa umakini, tokea uchaguzi uishe hata mwaka mmoja bado, lakini tayari Chama Cha Mapinduzi kimeanza kufanya utekelezaji wa miongoni mwa vitu ambavyo vimeainishwa katika Ilani yao ya Uchaguzi.

Nadiriki kusema Chama Cha Mapinduzi, kimestahili na kinastahili kuendelea kuiongoza Dola ya Tanzania.

Kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Humphrey Polepole, tumeona ameanza kuchanja mbuga katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025, kupitia kipindi cha PAPO KWA PAPO, kinachorushwa kwenye kurasa za Chama za mitandao ya kijamii na chaneli mbalimbali lengo likiwa ni kukidhi Kifungu cha 251 (e) kutoka katika Ilani ya uchaguzi ya 2020-2025.

Nachelea kusema tena Chama Cha Mapinduzi, kinafaa kuiongoza Dola ya Tanzania kwa maana kipo tayari kushughulika na kuzitatua Changamoto za Watanzania.

Nimalizie kwa kusema kuwa, kila Jumamosi nitahakikisha kuwa nafuatilia kipindi hicho cha PAPO KWA PAPO, ili kuwasilisha Changamoto za jamii yangu na kujifunza namna ya uongozi bora unavyotakiwa kuwa.

 
Habari kama hizi nasomaga heading tu,nakuja kumwaga sifa zangu kwa mkuu mwenye uzi.
Hongera kijana.
#sasa tuchape kazi
 
Umesahau kuweka namba ya simu, bado kuna nafasi chache za viti maalum
 
Hahaha unatuomba ridhaa wananchi au unataka tufanye nini?!

Tuliisha ikataa ccm kwenye sanduku la kura, mkapindua meza sasa fanyeni mliyotaka kuyafanya, mnahangaikia nini na mlisema kila kitu kiko kwenye ILANI?!
 
Papo kwa papo isiishie meza kuu.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba mjini hivi haoni wizi wa ardhi ulio wazi wazi unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM kwenye kata.Kuna hadi mwenyekiti wa kijiji katoroka kukimbilia Dar-es-salaam baada ya kudhurumu wananchi wawili.
Kama leo ungefanyika uchaguzi ulio huru na haki zipo kata kibao Bukoba mjini zingeenda upinzani.
 
Mleta mada , chakubanga anafanya maigizo kwenye TV. Kipindi chake hiki hakina tofauti na FUTUHI.
 
Back
Top Bottom