Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,873
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa 5 Feb 1977, Baada ya muungano wa vyama viwili (TANU na ASP ). TANU ni chama kilikuwa kinaongoza Tanganyika lakini ASP ni chama kilikuwa kinaongoza Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi kimejengwa katika imani ya mambo matatu:-
1. Binadamu wote ni sawa
2. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
3. Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
Hapa Africa ndicho chama bora chenye utaratibu mzuri. Vyama vingi barani Africa vimeiga taratibu za CCM.
Ni moja ya vyama vichache vya kuaminika barani Africa.
Chama cha Mapinduzi na Chinese Communist Party (CCP) ni moja ya vyama vya siasa duniani vilivyo na urafiki wa kudumu. Hivi vyama vinashirikiana kwa karibu ili kuhakikisha nchi hizi mbili zinafikia maendeleo kwa haraka.
Hivi karibuni CCM na CCP vitajenga chuo kikuu cha kufundisha wanachama hapa nchini.
Chuo hicho kitafundisha wanachama wa chama cha Mapinduzi ili kukuza uelewa wa chama na matarajio mapana ya chama.
Chama cha Mapinduzi kimejipanga zaidi kujitegemea na kuweza kukusanya mapato yake chenyewe. Chama hiki kipo na hazina na kubwa na vitega uchumi. Kwa hiyo mali na vitega uchumi vikisimamiwa sawa sawa, chama kitapata mapato mengi na kuweza kuimarika zaidi.
Chama hiki kimepitia misuko suko mingi sana. Lakini pamoja na hapo CCM imebaki kuwa Chama kimoja na wana CCM wameendelea kuwa wamoja.