CCM ni chama cha Mafisadi, Asiyeridhika arudishe kadi

Yaani kama chenge hapo alipo anasali na kufunga ili lowasa apite na akipita hii nchi si yetu tena

Hili ni kweli Kabisa.

Mabadiliko ya sasa ndani ya CCM .. kusema kweli wala hayawategemei wanadamu.

Ni more of "evolutionary" ... Lazima Kilichooza sasa kitumike kujenga kipya kwa manufaa ya wakulima na wafanyakazi.
Kitakaachoota na kushamiri kitatoa maua yeneye harufu nzuri sana ... kwa maana ya Utanzania wetu na utaifa wetu katika kuchapa kazi kama wafanyakazi na wakulima.
 
Mkuu,
Kwa maana hiyo unataka kusema hawajitambui?

Kumbuka kuna wengi wa aina ya Mzee Warioba ambao wanaielewa Tanzania kwa ndani na nje!

Au una maana gani unaposema ''bahati mbaya'', na kina nani wana ''bahati nzuri'' kuwemo CCM?

Mafisadi
 
Hakatwi Mtu hapa na ''Lowasa ni kama Mtume Mohamad''By Madabida.

Huyo Bw uliye mtaja jina hapo ni MTUME namuheshimu ndio maana Mimi sijaribu wala sidhubutu hata kumtaja jina.

Gundua kuwa Utume wake umebeba Nguvu hasi iliyotumika kuzika nguvu chanya ya uasisi wa Taifa hili. Enzi hizo waasisi wa Taifa walaifanya kazi kubwa kuasisi Taifa Chanya kabisa. Utaifa uzalendo upendo na utu vilikuwa ni Dhahiri kabisa kwa Taifa changa Tanzania.

Kama tulivyosema enzi hizo .. Uasisi huo ni kama mbegu amabayo lazima izikwe chini na kufukiwa kwenye udongo ioze ili kupatikane mmea mpya. Huwezi kubakia na mbegu ilele na huku ukapata mmea mpya wa kuota na kuzaa na kukomaa ili kupata mavuno.

Uasisi kama mbegu umebidi uoze na wa kuozesha ni nabii wako huyo. kaifanya kazi hiyo ya kifisadi vema kabisa na wenzeke. Kwakweli wamefanya kazi amabayo ikitumiwa vizuri .. ianweza kulipeleka Taifa mbali.

Kama mtu wako kashaifikisha Nchi kwenye uozo wa kiwango hicho anakazi gani tena iliyobaki. HAKIKA ATAKATWA.
Na kitakachotokea hapo ni maumivu kidogo ya hapa na pale kisha Utaota Mmea mzuri Tanzania MPYA yenye Azimio Jipya.
 
Kitu gani kinakufanya useme CCM ni chama cha mafisadi wakati unadai kuna wanachama ambao siyo mafisadi?

Kuna watu wengi wenye heshima zao ndani ya CCM kama Mzee Warioba ambao sidhani kama wako CCM kwa sababu ya kutafuta cheo au maslahi.

Umetumia kigezo gani kufahamu kama CCM inaongozwa na mafisadi?

Uanachama wa chama ni imani kama ilivyo uumini wa dini.

Kutenda dhambi kwa baadhi ya mapadri na wachungaji haiwezi ikawa ni tiketi timilifu ya kukufanya uachane na imani ya dini wanayoiongoza!

wewe imani ya dini si sawa na imani ya chama!Kama unataka kuamini hili nenda kakojolee msahafu mbele ya wahusika uone nini kitatokea,ukitoka hai nenda kakojolee bendera ya ccm mbele ya wahusika!ukimaliza njoo hapa ufanye mlinganyo!
 
Ndugu unayejiita Azimio jipya kweli unategemea CCM sisimizi anaweza kutawala na kutoa kauli? Hizi nazani ni ndoto za mchana
 
Mkuu CCM sio chama cha mafisadi coz hakikuanzishwa na mafisadi na kwa kuprove hilo soma historia yake ya kuanzishwa ila sema hao jamaa ndio wamevamia humo na ni shidaa, mnyukano wa makundi tofauti

kwa sasa unaweza kununua wanachama wote wa ccm kwa bei rahisi hadi ukashangaa ! wanaccm wana njaa kali kiasi cha kustua !
 
Nilishasema siku zilizopita kuwa kama chama kinataka kuchuja mafisadi kutoka kwenye wanachama waadilifu, wanatakiwa wakae nje utawala wa serikali kwa miaka kumi. Ndani ya miaka kumi mafisadi watakuwa wamekimbia, watakuwa wamebaki wanachama imani (waadilifu). Na wangeanza kujichuja mwaka huu 2015 kwa kukabidhi nchi kwa chama/vyama vingine vya siasa.
 
Nilishasema siku zilizopita kuwa kama chama kinataka kuchuja mafisadi kutoka kwenye wanachama waadilifu, wanatakiwa wakae nje utawala wa serikali kwa miaka kumi. Ndani ya miaka kumi mafisadi watakuwa wamekimbia, watakuwa wamebaki wanachama imani (waadilifu). Na wangeanza kujichuja mwaka huu 2015 kwa kukabidhi nchi kwa chama/vyama vingine vya siasa.

..Znz waliaminishwa kwamba dr.shein hana kashfa kwa hiyo ataibadilisha ccm-Znz.

..look at them now. Kuna mabadiliko yoyote yametokea ktk siasa za Ccm-Znz??

..sidhani Kama Ccm inasafishika kwa kuteua mgombea uraisi asiye na kashfa huku wajumbe wengi wa Ccm-nec, wajumbe wa mkutano mkuu, pamoja na wagombea bungee, wakiwa wachafu.
 
Hiki chama ccm kimechakaa sana. Na hakina mvuto wananchi wamekichoka mno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom