CCM ni CHAMA cha KIMATAIFA ==SMS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ni CHAMA cha KIMATAIFA ==SMS

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by QUALITY, Oct 12, 2010.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM ni CHAMA cha KIMATAIFA ==SMS
  CCM imekazana baada ya kuona maji yamekuwa ya shingo badala ya miguuni!! Usiku wa leo nimetumiwa meseji mbili., moja ilifika saa tisa dakika 26 ikieleza kama ifuatavyo “CCM iliahidi, na imefanya.. tuichague tena. CHAGUA CCM, CHAGUA KIKWETE.

  SAA 11.25 ALFAJILI CCM walinitumia sma nyingine inayosema hivi “CCM ni chama cha kimataifa, kimekomboa nchi nyingi barani Afrika” Chagua CCM, Chagua Kikwete.
  Baada ya kusoma SMS hii nilicheka sana nikamkumbuka mtu mmoja aliyekuwa anaongea katika zile picha za Tarime (uchaguzi mdogo) akisema “tumeandaliwa wajinga wengi, ili kundi dogo ndilo liendelee kutawala”.

  SMS hii ya CCM kuwa chama cha kimataifa, imeonesha kuwa CCM hawajui kuwa kuna watz ambao wanaelewa. Tangu lini CCM ikakomboa nchi za bara la Africa? Tangu lini CCM ikawa chama cha kimataifa?

  Mwaka huu wa 2010, hatudanganyiki. Endeleeni kutuma sms lakini hamuambulii kitu hapa.

  Bye CCM, Bye KIKWETE
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani sasa hivi wanaweweseka tu .walitegemea vijijini ndokwenye kura nako hawataki hata kuwasikia
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wameona thiatha dha majitaka dhinawapanditha wapindhani thatha wameamua kujipamba wenyewe? Hatudanganyiki!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kweli ccm hoi inavilaza gani hatakutengeneza msg nzuri wanashindwa, ccm kweli namkumbuka mangula katibu wetu!
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha you made my day mkuu. Yaani hawa watu wa thithiem nawashangaa mno!! Kwa nini wanatumia nguvu kubwa hivyo kuwahadhaa wananchi? Kama kweli wamefanya mambo mazuri yasiyo ya kifisadi basi wasubiri fainali za ligi kuu ya vyama vya siasa tarhe 31 Oktoba. Yaani zile message za Dr. Slaa zinachekesha sana, hata mtoto wa vidudu/chekechea atawacheka. Poleni sana.
   
 6. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Hahahahahhhh ..... na bado wataendelea kuweweseka......
   
 7. a

  allpurpose2010 Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuh inaonekana wakati mwingine hatuelewi. boss mimi pia nilizipata hizo sms, kweli inaonesha ndugu zetu wanahaha, lakini pia ngoja nikueleweshe kidogo.

  Hivi Rais wetu wa sasa niwa chama gani? na je Nyerere aliyehusika kwenye kuikomboa nchi yetu na kushiriki kikamilifu kwenye harakati za ukombozi wa nchi zingine za africa alikuwa wa chama gani? kama majibu yako ni CCM. then it is obvious CCM ni chama cha kimataifa na kimeshiriki kuleta ukombozi Africa.

  kuwa negative all the time bila ku-analyse issue vizuri wakati mwingine inaonyesha upungufu wa kufikiria.

  tutumie JF kusaidiana sio ku ongea bila kuchambua issue vizuri
   
 8. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu wengi wao ni school drop outs, failures, usalama wa taifa na polisi sasa unategemea ujumbe mzuri utokee hapo? Usishangae wengi wao hata Kiswahili sahihi hawawezi kuandika na ndo wamekasimishwa mikoba ya kuongoza kampeni, too sad!!!
   
 9. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  tehetehetehe wamefulia,wera wera hatuchagui ccm,
   
 10. TGS D

  TGS D Senior Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM bye bye!!!
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Poleni thithiem!!! Siku zote huwa najiuliza kwa nini hawa ndugu zetu wanatumia nguvu kubwa sana kujinadi? Tena nyingi zisizokuwa na busara? Always, Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
   
 12. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wakiniletea ujumbe huu nafungua jalada mahakani kwa kukashifiwa na namba yangu kupewa watu wengine bila ridhaa yangu. Lazima hawa Zain na Tigo waheshimu haki yangu ya privacy na namba yangu kutopewa watu hovyo wanaoweza kutuma message za hovyo namna hii
   
 13. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole Mkuu. Maana ya kuwa international ni nini? Kwa hiyo gharama zilizotumika kukomboa bara la Africa zilitoka CCM? Zilitoka kwa watz, hivyo ni vizuri kutofautisha CCM na Tanzania. Tanzania siyo CCM na CCM siyo Tanzania.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,860
  Trophy Points: 280
  Uwezo wako wa kuelewa unaonyesha ni duni sana. Vita ukombozi kusini mwa Africa na kwingineko ilipata msaada kutoka kwa watanzania wote na sio CCM kama unavyotaka kujiaminisha wewe na wengine. Watu walichangia rasilimali zao na hata uhai wao bila kuwa wana CCM. Maana mtasema tena kuwa CCM ilimpiga Idd Amin. Fikirini kabla ya kutamka, watanzania wa leo wameamka.
   
 15. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Umepata kutoka namba gani?Ileile inaomkashifu Slaa?Kama ndiyo hiyo basi washathibitisha kuwa ni ccm ndo waliotuma zile sms.
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  na bado watajibeba
   
 17. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  SMS haina namba simu inaandika CCM basi (no number!!!!!) Inawezekana ni kwa msaada wa TCRA na hii ni baada ya kutumia namba ya nje wakapigiwa kelele.
   
 18. v

  valour Senior Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  "Watu walichangia rasilimali zao na hata uhai wao bila kuwa wana CCM. Maana mtasema tena kuwa CCM ilimpiga Idd Amin. Fikirini kabla ya kutamka, watanzania wa leo wameamka."

  Kweli hapo umesema. Anasahau kwanza wakati huo chama kilikuwa kimoja tu na kila mtu awe na chama asiwe nacho wote tulichangia harakati za ukombozi. Tutaelimishana taratibu.
   
 19. M

  Mkerio Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 12, 2006
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna sababu ya kukataa sana hayo ambayo CCM imefanya. Ila swali muhimu kwa sasa je bado ni political agenda kwa leo? Ni kama ilivyo ukweli kwamba CCM imeleta uhuru. Je, swala la uhuru kwa leo lina maana gani? Leo inapaswa tuzungumzie elimu bora, maji, ajira, usimamizi wa raslimali nk. Mambo ya kukomboa nchi za africa si agenda za leo wala si moja ya matatizo ya Mtanzania wa leo
   
 20. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kumbe nilidhani nimekosea kusoma hiyo taito, mi niliisoma hivi.."CCM ni Chama cha kimafia" nadhani sijui lakini kwamba ndio sahihi
   
Loading...