CCM ni Adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ni Adui wa Maendeleo ya Tanzania na Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 20, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tuliambiwa na TANU. ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora.

  Tukaimba wimbo wa Azimio la Arusha, Azimio la Musoma, madaraka mikoani, vijiji vya ujamaa na zaidi, tukasema kuwa mkoloni, bepari na kaburu ndio maadui wa maendeleo yetu ukiongezea Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  Leo hii nawatamkieni wazi, ikiwa ni mahubiri yangu ya Jumapili ya Oktoba 19 ya mwaka 2008, kuwa Adui mkubwa wa maendeleo ya Taifa la Tanzania na ustawi wa Maisha ya Watanzania ni Chama Cha Mapinduzi, maarufu kama CCM.

  Pamoja na mazuri ya kale yaliyofanywa na TANU hata CCM, lakini ukweli usiopingika kuwa CCM hii si ile mliyokuwa mnaiamini na iliyowaletea Uhuru au Mapinduzi ya kizalendo.

  CCM si Chama cha Mapinduzi, bali ni Chama cha Ubabaishaji. Iwe ni uzembe, uvivu, uzururaji, uhujumu, uongozi mbovu, ufisadi, kutokuwajibika au lolote lile ambalo ni kizingiti cha maendeleo ya kweli katika Taifa na Jamii.

  CCM ya leo imejenga ubaguzi wa mawazo, imedumaza maendeleo ya Wananchi, inakumbatia hujuma na ufisadi, haina dira au mwelekeo wa kujenga Taifa na Uchumi wake, haina uongozi bora wala siasa safi.

  CCM ya leo inatumia vitisho na mabavu kuongoza Taifa na imefikia hatua inalihujumu Taifa ili iendelee kuongoza na kutawala!

  CCM ya Kikwete, Msekwa na Makamba zimeishia kuwa Chama cha Wababaishaji, wasio na nidhamu, utu wala aibu. Hakimjali tena yule mkulima au mfanyakazi, bali yamtukuza yule mwenye pesa.

  Watu na Ardhi, wapo, Siasa safi ilikuwepo, na hata Uongozi Bora. Lakini watu wameendelea kuwa wanyonge, dhaifu na masikini wa kutupa, ardhi imepoteza rutuba na thamani na kila kitu kinasukumizwa kwa mgeni aliye na fedha akinunue ili Taifa lipate vijisenti vya kujinusuru.

  Kwenye Siasa safi na Uongozi bora, huko ndiko kumeoza kabisa! Kwa kipindi cha miaka 13 iliyopita, CCM imepoteza uwezo wa uongozi, imepoteza viongozi safi na wenye uzalendo, imepoteza uwezo wa kuwa na siasa za kujenga Taifa na kupigana vita dhidi ya Umasikini, Maradhi na Ujinga.

  Ni kweli takwimu za Kizungu za kiuchumi na maesabu zinaonyesha uchumi ukikua, lakini ni tarakimu kwenye majedwali, na si hali halisi ya Mtanzania kuwa na uhai na tumaini la kuwa na kesho kutwa au mwezi ujao bila kuwa na hofu.

  Ikiwa tuliambiwa mapema mwaka huu kuwa asilimia 52 (52%) ya Watanzania wanacheza makidamakida au Umbali Sufuri (Zero Distance)kutoka umasikini, huku wakiwa hawajui leo wataishi vipi, iweje tujitape kuwa uchumi na pato la Taifa limeongezeka?

  Ikiwa tunaambiwa 31% ya watu wazima ambao ni miaka 18 na zaidi ni wajinga hawajui kusoma na kuandika, tutasemaje kuwa tunapiga hatua za maendeleo?

  Ni maendeleo gani ya kurudi kinyumenyume? NI maendeleo gani ya kutumia na kutumbua bila kuzalisha na kuongeza kipato? Uwiano wa Matumizi na Mapato ni karibu matumizi mara tatu ya mapato!

  Sasa tumeingia mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, lakini inabidi tuache woga na kuachana na ile methali ya zimwi likujujalo na tuachane na CCM.

  Kauli za Ari, Nguvu na Kasi mpya ni kejeli tupu. Hotuba za Maisha Bora kwa kila Mtanzania ni ujuha na tusi la nguoni!

  Nawaasa Watanzania wenzangu, achaneni na CCM, CCM si chama makini tena na hakijali maslahi yenu wala uhai wenu. Thamani yenu kwa CCM ni nyakati za uchaguzi kama tulivyoona huko Tarime majuzi au kule Kiteto!

  Ni heri tuwachague CUF, Chadema, TLP, NCCR, UDP au wengine wote nao wajaribu kutuongoza maana umahiri wa CCM tunaohubiriwa kila siku ni uozo mtupu.

  Mtanzania mpaka leo anasota kwenda tafuta kuni na maji, kulima kwa kujihemea, hana shule, dawati, daftari, dawa, mshahara mdogo huku gharama za maisha zikipanda na mbaya zaidi, hakuna hata mtu mmoja ambaye anauwezo ndani ya CCM kusema tunahitaji full stop ya ubabaishaji na kuanza kutumikia Watanzania.

  Badala yake sababu nyingi zinatolewa kila siku kuhalalisha udhaifu wa Serikali na CCM. mara leo bei za mafuta, kesho jua kali na kiangazi au la sivyo tutaambiwa kuangamia kwa uchumi wa nchi tajiri zilizoendela ni sababu Tanzania inashindwa kupiga hatua za maendeleo.

  Iweje Rwanda, Burundi na hata Congo wanaanza kutupita huku sisi tukishabikia Amani, Utulivu, Mshikamano na Umoja lakini ni masikini wa kutupa?

  Najua wengi wenu mtadai kuwa CCM kuna wanamapinduzi kina Mwakyembe, Seleli, Kilango na wachache kadhaa ambao eti ni mabingwa wa Wananchi. Lakini watakuwaje mabingwa wa Wananchi ikiwa wao ni wafungwa wa kisiasa ndani ya Chama chao pamoja na kufurukuta kwao?

  Tutasemaje eti tuwape CCM miaka mitano mingine ya majaribio huku majaribio ya mwisho yametupa Kiongozi Mkuu ambaye hana hata nguvu ya kuhamasisha umma na kila siku kuishia kulalamika kama Wananchi wanavyolalamika?

  Hivi kina Mkukuta, Ilani ya 2005 na visheni 2025 zina maana gani ikiwa anayefaidika ni James Sinclair, Jeetu Patel, Yusuf Manji, Rostam Azizi, Andrew Chenge, Benjamin Mkapa, Daniel Yona, Edward Lowassa, Gray Mgonja, Karmali Juma, Barrick Gold, Rites Corp, IPTL, Richmond na wenginewe katika kikundi hiki kidogo kinachomiliki na kutumbua maslahi ya Taifa na si mkulima, mvuvi, mfanyakazi, mwalimu, mwanafunzi, mzee, kijana na mtoto wa kawaida?

  Kuna umuhimu gani kuendela kusema tunaimani na CCM ikiwa CCM haioni umuhimu na umaana wa kuliongoza Taifa kutoka Umasikini, Ujinga na Maradhi?

  Ikiwa Nyerere alitishia kujitoa CCM na kusema CCM si Mama yake, iweje sisi tuendelee kuamini kuwa CCM ni Mama na Baba, Alpha na Omega wa kutuletea maendeleo Tanzania?

  Sana sana walichokifanya CCM kwa bidii ni kuturudisha nyuma kimaendeleo kwa kukimbilia kuua mihimili ya Uchumi wa Taifa kwa kuiuza ama kwa bei poa au dezo kwa wawekezaji na wao wenyewe.

  Mipango ya maendeleo ambayo tuliimba na kuifanya kuwa ndiyo nguzo kuu ya kujitegemea kama Taifa hasa katika nyanja za kilimo, ufugaji, uvuvi na hata ajira, CCM imezitelekeza kwa jina la kujivua majukumu ya Serikali inayofanyia kazi watu kwa kisingizio cha Utandawazi na Soko Huria.

  Badala ya kurekebisha makosa na matatizo ya awali yaliyotufikisha hapa tulipo kiuchumi ili kuimarisha Taifa letu na ustawi wetu kama jamii, CCM kupitia Serikali yake imeendelea kuturudisha nyuma kimaendeleo kwa kampeni yake maalum ya kutoa kipaumbele cha kuvuna mali ghafi na rasilimali za Taifa kwa Wawekezaji wanaotuhujumu na kugawanyana wao kwa wao umiliki wa mali na mifumo ya Uchumi wa nchi yetu.

  Sasa hivi Tanzania nzima kuna woga wa kutisha wa kutokujua kama kesho itafika kukiwa na chakula mezani au dawa za kutosha. Mgawanyiko wa wale wenye mali na wasio na mali ambau hujenga tabaka la masikini na matajiri ni kubwa mno na asilimia kubwa ya Watanzania wanaegemea kwenye Umasikini uliokubuhu.

  Tanzania ya leo, pamoja na kuhamia katika mfumo endelevu wa soko huria, bado haijaweza kujitosheleza hata kwa chakula! Kwa mujibu wa ripoti ya kiuchumi ya Serikali na Benki Kuu iliyotoka mwezi uliopita ambayo inaonyesha ukubwa wa madeni ya Taifa, mapato na matumizi ikiwa ni pamoja na uagizaji, inaonyesha ongezeko kubwa la kuagiza chakula, huku nchi ikiwa imebarikiwa na neema ya ardhi ya kutosha yenye rutuba, vyanzo vingi vya maji na watu wa kutosha kuzalisha chakula.

  Badala ya kuja na sera na mipango endelevu kuimarisha uchumi na kusu(Tusi)(Tusi)(Tusi)(Tusi) gurudumu la maendeleo kwenda mbele, CCM imekimbilia kutafuta njia fupi na gharama nyepesi kujipatia kipato na kutamba kuwa pato la Taifa linaongezeka.

  Ongezeko la uuzaji holela wa mashirika, viwanda, ardhi na vitega uchumi vya Taifa likiandamana na rushwa na uhujumu vimeongezeka.

  Badala ya kuongeza ufanisi na gharama ya ubunifu, juhudi na maarifa ili kuinua vipato, CCM imeegemea kubobea katika Rushwa na Takrima na imefanya makusudi makubwa kabisa kuhakikisha kuwa Rushwa na Takrima zinakuwa sehemu halali za maisha ya Mtanzania. Mfano hai ni chaguzi za Serikali za Wabunge na Urais mwaka 2005 na chaguzi ndogo zilizofuatia ambapo CCM ilitumia fedha nyingi kutoa hongo ili ipate kura.

  Hata pale penye ushahidi tosha wa Uhujumu wa Taifa iwe ni Ufisadi au kuzorota kwa mahusiano ya Tanganyika na Unguja, bado CCM imeendelea kupuuzia kilio cha Mtanzania na kutuhumu wale wanaopingana nayo kuwa ni wasaliti na si wazalendo au waleta maendeleo.

  CCM inajitapa kwa wananchi kuwa yenyewe ina dola na ndiyo iliyo madarakani, lakini inashindwa kumpa Mtanzania uhuru wa kujitegemea kiuchumi. Inashangaza kuwa mpaka leo kuna baadhi ya Watendaji na Viongozi wa CCM ambao wanapita vijijini na mijini wakijitapa kuwa wao ni Dola na wana nguvu. Ni nguvu gani ikiwa raia wako wanateseka?

  Kitendo cha Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM Bwana Jakaya Kikwete kuzomewa hata kutupiwa mawe ni ishara rasmi kuwa nchi iko njia panda na Watanzania wamechoshwa na mbiu ya mgambo kuisifia CCM kila siku kuwa ni bora kuliko wengine.

  Kututisha kuwa eti akija Maalim, Lipumba, Mbowe, Mrema au Cheyo kuwa Taifa litaingia katika vita na vurugu na umwagaji damu mithili ya Zimbabwe na Kenya ni uongo mkubwa!

  Yaliyotokea Zimbabwe na Kenya ni yale yale ambayo CCM imeyafanya, kumpuuzia mwananchi wake aendelee kusota huku wao CCM wakibadilishana safari za kwenda kutumbua ndani na nje ya nchi.

  Natoa wito huu kwako ndugu Mtanzania kuwa adui wa maendeleo yako ambaye amekomaza Umasikini, Ujinga na Maradhi si mkoloni, bepari, beberu au kaburu tena, bali ni CCM.

  Waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako, jihadharini na CCM!
   
 2. mtzmweusi

  mtzmweusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2014
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 4,244
  Likes Received: 2,710
  Trophy Points: 280
  Wakuu kwa masikitiko makubwa sana natangaza kukihama chama changu cha ccm maana kimepoteza dira kimekuwa chama cha kulinda majizi mafisadi sio tena chama cha walalahoi kama sisi na ili tuendelee sharti huyu adui ccm atoke
   

  Attached Files:

 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2014
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Mtahaha sana na CCM.

  Mmebwagwa hoja zenu zote, iliyobaki mnatapatapa.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2014
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  "Watanzania wanataka watatuliwe kero zao mbali mbali, hili wasipolipata ndani ya CCM watalitafuta nje ya CCM." Mwalimu (RIP) hakukosea kabisa alipoitoa kauli hii. Adui wa kwanza wa Tanzania na Watanzania ni MACCM.
   
 5. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe hoja yako ni nini hasa kwenye issue hii ya ufisadi? Unataka wananchi wakae kimya tu? Hebu lete maoni yako tuone. Ni ushabiki tu wa kitoto unafanya au labda ni mimi tu sikuelewi!
   
 6. Lancanshire

  Lancanshire JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2014
  Joined: Sep 20, 2014
  Messages: 13,775
  Likes Received: 7,926
  Trophy Points: 280
  Chama cha kipumba.vu wabunge WA ccm wameonesha wazi kuwalinda mafisadi. Tutakutana kwenye ballot box hiyo mwakani wala haina tatizo
   
 7. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280


  Mkuu hoja za PAC ni za wabunge wote kwa maana kamati ni ya bunge na inafanya kazi kwamujibu Wa kanuni...

  kamati imechambua hoja za CAG... kamishna mkuu Wa TRA na Mkurugenzi Wa PCCB.....

  Bahati mbaya Sana Muhongo hajathubutu hata chembe kugusa au kuongelea maoni ya watu hao watatu ambao ni agents wa serikali....

  Ni mtu dumb tu anaweza shabikia kinachofanyika bungeni na baadhi ya wabunge kwani wabunge walipaswa kuhoji serikali na si mashambulizi kwa PAC maana hoja ni yao....

  kwa Mara ya kwanza wabunge kuifurumua kamati badala ya serikali but wanaonunua watu cheap kupindisha taratibu wataigharimu nchi hii.....

  Wengi kwa mazoea tu na upogo Wa akili waliishambulia PAC Kama ukawa ilihali kuna wanaCCM 19 hivi kesho hao wajumbe watakaa pamoja wakaelewana??

  Tanzania inachagizwa Sana na watu Wa low profiles Kama akina Lusinde wanaopewa 30 minutes kuongea upuuzi ambao mawaziri wameupigia makofi ilhali watoto wao wakifanya Kama ya Lusinde naamini watawapiga......

  Watu mazuzu...
  mataahira...mazezeta....wapenda pombe...ngono..

  majungu.....ubwabwa na kila aina ya ushenzi wanatufanya tugharimike Sana....

  50 years after independence hatujafikia hata uchumi Wa kati halafu watunga Sera na wafanya maamuzi wetu ndo style ya kina Lusinde...

  TOO LOW!!!!!!!!!!!!
   
 8. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280

  Mkuu mi nasubiri wabunge wenye akili toka CCM nisikie wataongea nini baada ya hapo ndo ntakuwa na final conclusion sio vipapa Wa Leo.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2014
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Mkuu lusungo tuombe hili litokee maana siku hizi CCM ilivyojaa wahuni na mafisadi Wabunge kama Esther Bulaya na Deo Filikunjobe ambao mara nyingi wanatetea maslahi ya Tanzania wanachukiwa hata kutishiwa kufukuzwa ndani ya chama.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280

  Wabunge wengi Sana wanahongwa Dodoma usiku huu mpaka najiuliza Kama hoja ilikua nyepesi nguvu yote hii yanini??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2014
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,063
  Trophy Points: 280
  Duh! Kwa hiyo mgao wa pesa za wizi za walipa kodi zaidi ya shilingi bilioni 300 bado unaendelea!!! Katika jitihada zao za kupotosha ukweli.

   
 12. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2014
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Adui wa Tanzania sio chama cha siasa tu bali utamaduni mmbaya uliotambaa kila sehemu wa jinsi tunavyofanya mambo just about everywhere. Main catalyst ni ugumu wa maisha jumlisha status quo inavyo exploit their upper stakeholders position kwa sasa kutokana na political powers and financial position held iwe kwenye upinzani, chama tawala, taasisi za serikari ata uraiani kwa wenye nacho.

  Hakuna chama cha siasa Tanzania kinachosimama na mandate model yao, yaani kwa Tanzania ukisikia vikao vya chama ujue ni mkutano privately wa kwenda kusutana kwa wanachama au kutatua mgogoro wa kichama for the most.

  Nchi za wenzetu ukisikia mkutano wa chama ni kwenda kupima election manifesto na kila mmbunge au kiongozi wa chamaa ana hakikisha analenga kuona ilani ya uchaguzi inafikiwa. Watu wakirudi makazini wabunge wanajua serikari waikague vipi kutokana na malengo ya chama chao,wakuu wa wilaya, madiwani all the way to floor leaders kama ilani yao intekelezwa na wanachama wana msimamo wa pamoja kwenye hilo.

  Kwa siasa za JF nachukulia kama sura ya hali halisi ya vyama vya siasa Tanzania. Hivyo basi jinsi makada wa vyama wanavyochangia katika swala moja inaonesha ni jinsi gani hata huko kwenye vikao vyao kwamba hakuna misimamo na sidhani ata kama wanachama wanaelewa strategy za serikari katika kutekeleza ilani yao ya uchaguzi katika vitu kama: umeme, kilimo, elimu na kwengine.

  Vinginevyo watu wasingekuwa wanatofautiana sana. Michango ya wanachama humu ndani for the most ni yale mambo yanaongelewa kwenye vikao vyao na hapa ni muendelezo ule ule hata kwenye maswala yanayotakiwa kupimwa kama kuna makubaliano ya usimamizi na utetezi wa pamoja kwa sababu hoja inasimama au maamuzi yanatokana sababu a,b au c ya kichama.

  If people from the party ambao wanatakiwa kuwa wasimamizi wa serikari can have contradictory views how are they supposed to demand accountability in the interest of their group or where and when do they remind themselves of their mandate and if the government is respecting that ie their own ministers and the ministries.

  That is just a summary of uozo wa vyama vyetu vya siasa kama unatafuta accountability kutoka serikarini ambayo for the most part ina sheria na formed governing bodies jumlisha na the fact si watu wengi wanaofatalia sheria au kutaka kuzielewa kwa sababu ya usimamizi na majukumu ya taasisi za serikari. Trust me nchi ina mambo mengi sana ya kurekebisha, watu wajikaze kidogo sio kuchukua makundi kwa sababu ya maslahi. Sisi bado sana katika usimamizi ndio tatizo letu na kujua maana kuwa kundini.
   
 13. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280
  Watu wanajilia vyao tu ila baadhi ya wabunge wenye ubongo kichwani wamegomea hizo pesa wanaozishobokea ni wale waliojaza ute kichwani....

  Hili fukuto halitokwisha kwa mipasho litagharimu watu yetu macho...
   
 14. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2014
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwakuwa wewe upo karibu unatakiwa utuambie kutokana na facts zilizopo so far.

  Tuache kwanza nani kalipwa nini.

  Ni wapi unaona kuna makosa ya kifisadi given the facts ili tupate upande wako vizuri habari za watu wanalipwa sasa hivi aitoshi kutuamunisha kuna cover up; what needs justifiable is the wrongdoings?
   
 15. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280
  Soma hii kuna mwenzio nilimjibu huenda ikakusaidia.....  Kuna malipo ya aina mbili ambayo TANESCO
  wanakatwa kwenye mkataba wa IPTL....
  1. Gharama za ununuzi Wa umeme (kwa unit)
  hizi hazikua na mgogoro na TANESCO wamekua
  wakinunua umeme unaozalishwa na kulipa bila
  shida.
  2. Capacity charges ( gharama za uwekezaji) hizi
  IPTL izalishe ama isizalishe lazima walipe...
  Katika fungu la 2 ndipo palipoibuka mgogoro
  kwamba TANESCO wamelalamika kutozwa zaidi
  ya gharama halisi.
  Kabla ya kuendelea naomba tu nikwambie hela
  hizi hazihusiani na ubure Wa umeme kwakuwa
  TANESCO inanunua tena si kwa IPTL pekee wapo
  symbion aggreco songas etc....
  Fedha inayoongelewa ni hiyo iliyokua na mgogoro
  ambapo wizara iliamuru ilipwe ktk kiza kinene na
  Shaka kubwa.....
  PAP walilipwa fedha kabla ya kununua hisa za
  VIP na walilipa fedha za ununuzi Wa hisa kwa VIP
  Mara tu baada ya kulipwa mabilioni ya escrow
  sasa jiulize je PAP walipewaje PESA zote bila
  kununua kwanza hisa zote?
  Pili ni kodi gavana Wa BOT aliuliza Mara nyingi
  juu ya tozo ya VAT akaambiwa hailipwi wakati
  kisheria ilipaswa ilipwe je huu si uhujumu??
  Sijui Kama unachangia kwa utashi ama unatania
  lakini ishu hii itatugharimu Sana.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2014
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Rev. Having read your post line to line and word to word, nimesikia uchungu sana. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wanyonge ndiyo wanoendelea kuumia siku hadi siku. Ufisadi sasa ni sera rasmi ya CCM. Yaani mwansheria mkuu, ambaye alipaswa ndiye awe anahakikisha sheria inafuatwa na kufungulia mashtaka wezi wa aina hii. Yeye naye ni kinara mla rushwa. Aibu gani hii? Hata enzi zile za mzee ruksa CCM haikuwahi sink this low.

  Cha kuchekesha kuna vi-middle men vya mafisadi hapa katikati ambao inainclude hata top govt officials, wabunge, the so called learned brothers etc.

  Leo hii watanzania wanaminishwa eti ukiwa against huu upuuzi ni kwa sababu hukupata mgao, really? Utetezi mkuu wa wizi huu wa escrow kutoka vigogo wa serikali ni kuwa eti zile hazikuwa hela za umma. Hawasemi kuwa hawakupokea what a joke?
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2014
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,343
  Likes Received: 2,679
  Trophy Points: 280
  Duh!!! naona wadau mnafukunyua hadi sredi za miaka 6 iliyopita...
   
 18. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2014
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa hivyo hili tuliondoe sio tatizo kwa sasa, kukukumbusha ndio mzozo wenyewe ulianzia hapa.

  Kutokana na ushahidi wa pande mbili ni kwamba ili shauru liliamuliwa na mahakama ya kimataifa ambapo TANESCO walirekebishiwa kiwango. Na kwakuwa awakufungua shauru jengine tena ina maana shirika liliridhia doesnt mean they were happy.

  Wewe ulitaka hili swala litatuliwe vipi na nani?

  Whilst you are at it shauri la capacity charge waliofungua standard charter si shauri la TANESCO ni wao wenyewe walifungua hata kabla ya kufuata sheria za umiliki wa IPTL kama sheria za Tanzania zinavyotaka.

  Kwa mujibu wa ushahidi na facts zilizopo yaani jaji Utumwa order, Tenesco public report, extensive research on the saga and facts on business conducts; ni hivi unapouza biashara au bidhaa si lazima ulipwe cash cha muhimu ni makubaliano ya kulipana na kuridhia. Kwa hivyo on VIP perspective wao walichotaka ni kulipwa makubaliano ni kati yao na PAP jinsi watavyolipana na ni private matter it could also be tactical in this instance but nevertheless legal.

  2...Jaji Utumwa asingeweza kumkabidhi "IPTL", PAP kwa sababu mgogoro ulikuwa wa VIP na mechmar (wabia wanaotambulika na TANESCO) kwa hivyo hilo lazima liwe lilitatuliwa kwanza mbele ya mahakama kabla ya lolote kufanyika, na isitoshe Utumwa aliwaita wadeni cum wabia wa SCH ambao awakutokea hivyo basi ndio sababu zulizompelekea PAP kupewa IPTL baada ya VIP kuithibitishia mahakama kuwa yeye shares zake pia kamwachia PAP na wanaweza kulipana muda wowote ki biashara si lazima malipo yawe papo kwa hapo.

  Kwa hivyo labda kisheria kosa liko wapi PAP kutumia hela escrow kumlipa VIP?

  VIP angekuwa ameshafungua shauri mahakamani kama PAP alipewa hela ambayo imetengwa kwa sababu ya mgogoro bila ya yeye kuafiki ama?

  Facts zilizoletwa ni kwamba TANESCO waliacha kuweka hela kwenye escrow account kwa muda mrefu hata zile ambazo walistahili kulipa kutokana na kutumia umeme wa IPTL takribani zaidi ya millioni $100.

  IPTL walipoletewa swala la kodi walidai inabidi TANESCO nao walipe hela ambayo TANESCO by law wanadaiwa kutokana na mkataba na kutumia umeme.

  Kilichofuata walikaa chini na kuafiki kwamba kuwe na tax exemption based on the debt; iwapo TANESCO wangelipa deni lao IPTL wangelipa kodi na kuondoka na faida zaidi. Hili IPTL isilipe kodi ilibidi iingie hasara ya zaidi ya $70m that is the money after paying their debt.

  wewe hapo ulitakaje kwa faida za walipa kodi na TANESCO?

  Hiwapo kuna watu wataendelea kupotosha facts of the matter dont you think?
   
 19. lusungo

  lusungo JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 18,139
  Likes Received: 9,022
  Trophy Points: 280
  Hujajibu chochote zaidi Sana ulijitahidi uonekane mjuvi kumbe zoba

  Sina mda nawe tena nyie type ya kina kisangi na Lusinde huwa naona najisi kubishana nanyi....

  Mjadala unaendelea bado Una nafasi ya kujifunza mengi ila Nina rekebisho moja tu

  Jina la jaji ni Utamwa sio Utumwa.
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2014
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna watu hapa wana hoja ya udini na uCCM, Kwa mtu anayeelewa maana ya Stockholm sydrome ataelewa nini maana yangu.

  wa mtu mwenye macho, mwenye akili timamu hata siku moja hawezi kukaa kimya kutokana na kilichotokea.

  Kumbuka EPA....rais alitangaza mwenyewe kuwa wezi waliiba hela

  Drug barons ku-bank roll baadhi ya wanasiasa, kama mtakunmbuka kulikuwa na bendi inaitwa TOT ilikuwa inafadhiliwa na hela za drugs

  Richmond,

  Escrow

  haya yote kwa mtu mwenye akili timamu anatakiwa kujiuliza ni bahati mbaya au ni mpango mzima?
   
Loading...