CCM ndio waasisi, walezi na vinara wa rushwa katika uchaguzi Tanzania?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ndio waasisi, walezi na vinara wa rushwa katika uchaguzi Tanzania?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MKWECHE, Oct 26, 2012.

 1. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie Mkweche napatashida na kuhuzunishwa na vilio vya Rushwa ndani ya chaguzi za CCM!
  Mwenyekiti Waoanalalamika,wazee wao wanalalamika,walioshindwa analalamika sasa jamani hii nchi inakwenda wapi!
  Hawa walioshinda kwa mashaka,kulaumiwa na kutuhumiwa kwa rushwa,kesho utasikia wameteuliwa wakuu wa mikoa au wilaya,wagombea wa ubunge au hata mawaziri!
  Na je mtu alieingia madarakani kwa njia ya rushwa kwa kupitia chama chake,Atapata wapi Nguvu,uwezo na jeuri ya kupambana na rushwa akiwa serikalini hata akiwa waziri wa nchi Utawala Bora au waziri Mkuu!
  Uuuwii!Mkweche napiga mayowe ya uchungu na Nchi yangu!Sasa naanza pata picha ya chanzo cha umaskini wa Taifa letu!Siku za nyuma kulikuwa na Shirika la Uchumi na Kilimo la Chama SUKITA lilivuma,vuu vuu likafa ghafla!Viwanja vya michezo vikakabidhiwa kwa CCM leo hii viwanja vipo hoi na vingine hata vyoo havina,wakati mapato ya kila mechi yanalipwa na timu zinazotumia au kukodiwa!
  Kama mtu anashindwa kusimamia mali ya chama chake Ataweza mali za Nchi!Mkweche nakiri,Sasa natoka gizani kurudi barabarani kwenye mwanga!
  Hivi hata wale walio Kwenye Cabinet na waliomjengoni wakiwa na nguo za kijani inawezekana wameingia bungeni kwa Njia hizi hizi Chafu!Mola isaidie Tanzania!
  RUSHWA haitaisha kwenye siasa za CCM kwa kuwa Inalelewa ndani mwake!!Na Maendeleo hayawezi patika kama chama kilichoshika dola kinakosa uwezo wa kudhibiti Rafu na Rushwa katika ngazi mbalimbali za uchaguzi ndani ya chama!
   
Loading...