CCM ndio chanzo cha ubovu wa Elimu nchini, ni makusudi ya viongozi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,159
2,000
Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya TWAWEZA juzi, walibainisha kua mtaji mkubwa na ndio sehemu ya kutokea CCM ni watu wenye elimu ya Msingi na Wazee. Hiki ndio chanzo cha ushindi wa CCM kila unapofanyika Uchaguzi.


Ndugu zangu wana JF, hivi CCM watapenda watanzania wapate elimu ili wakose wapiga kura? Hii ina maana gani hasa? Inamaana inawezekana kua kila mwaka hua kuna makusudi mazima ya kuhakikisha kua watanzania wanakosa elimu ili waendelee kuwadanganya na kujipatia wapiga kura. Kwa mujibu wa ripoti ya TWAWEZA hakuna msomi mwenye elimu kubwa anahangaika na CCM, ukiona hivyo jua ni mzee au mtoto wa kiongozi flani.Taifa la watu waliokosa maarifa litafika wapi jamani?

Uthibitisho wa hili.

Kwa sasa kuna vilio kwenye vyuo vikuu wanafunzi kukosa mikopo bila sababu, kuna ubaguzi mkubwa kwenye utoaji mikopo ya elimu ya juu. Upandishwaji wa ghafla wa madaraja kwa wanafunzi kujiunga na vyyo vikuu. Hii ni dhambi moja mbaya sana na ipo siku itawageukia CCM wenyewe.


Zaidi ni pale CCM wanapoamua kugomea mabadiliko ya katiba makusudi kuendelea kukumbatia na kulinda wanasiasa wasiokua na elimu au wenye elimu ndogo tena wengine ni kwenye nafasi muhimu.Mwanasiasa huyu mwenye uwezo Mdogo wa kufikiri na kudadisi ni lini atakua mchango kwenye kulipaisha taifa lake kimaendeleo?

Ubovu wa miundombinu mashuleni na ajira kwa walimu ni tatizo kubwa, viongozi wanasema kua hakuna uhitaji wa walimu wa masomo ya sanaa ilihali kuna shule nyingi tu hata walimu wa aina hiyo ni adimu hasa maeneo ya vijijini.Mtu anaulizwa ni kwanini wanafunzi wanatumia vitabu ambayo havina viwango kwenye kukuza maarifa ya wanafunzi yeye anajibu kua "vitabu hivyo kwa sasa havitumiki kwa sababu wanafunzi mwenyewe wako likizo" Haya yote ni kuendelea kuididimiza elimu yetu, hakuna anayejali kikubwa ni kujivunia wapiga kura ili kuendelea kukibeba chama.

Ukiunganisha haya yote na matokeo ya tafiti za TWAWEZA ndio utatambua kua CCM ni kina nani.

Taifa limefikia hapa lilipo kwa sababu ya CCM, isingekuwepo CCM pengine tungefikia mbali sana.
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,246
2,000
Chama cha Makinikia ni wajanja wajanja sana.. Wanajua na wanakiri kuwa wanapendwa na wenye elimu duni..
Hivyo wamewekeza nguvu zao nyingi kuhakikisha elimu inaendelea kuwa duni..!
Kinyume chake ni kujifuta kwenye ramani ya siasa..!
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,067
2,000
Ujinga nyumba ya njaa. Tanzania wajinga ni wengi kuliko maelezo. Angalia jinsi wanavyotumika kisiasa sasa hv kwenye suala LA mikinimia.
 

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,481
2,000
Ukitaka kumtawala mtu mnyime Elimu,Taarifa na Maarifa.
Wangeamua suala la Elimu ilikiwa sio suala la kuongelea sana ni kuwekeza tu na kutenda tu.Kila siku wanaongelea yale yale.
Hii ni Makusudi wanafanya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom