Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
Timu yoyote ya mpira makini huweka washambulliaji makini na wenye uwezo ili kuilete ushindi. Hata timu za mpira wa miguu ulaya hutumia gharama kubwa kununua washambuliaji wakali na mkini ili kupata ushindi. Mifano michache ni kama Real Madrid, Man United, Chelsea, PSG n.k. Katika siasa pia chama chochote makini huweka viongozi makini na wenye ushawishi mkubwa mstari wa mbele ili kunadi sera na kushawishi watu kukiamini na kukiunga mkono. Mara nyingi watu hawa huwa ni wenye busara sana, uelewa na ushawishi na ndio huwa mdomo wa chama.
Jambo la kushangaza CCM badala ya kuweka mstari wa mbele watu makini, waelewa, wenye ushawishi mkubwa na wenye busara kubwa, wameweka mambumbu watupu ambao kila wanapoongea hakuna la maana zaidi yakukiabisha chama na kukifanya chama kidharaulike. Angalia aina ya washambuliaji inao watumia akina Nape na Mwigulu. Hawa badala ya kufanya mashambulizi kwenye goli la wapinzani na kufunga magoli wanagfanya mashambulizi mengi kwenda upinzani halafu magoli wanafunga golini kwao. Ukisikiliza kauli za Nape na Mwigulu ndipo utajua ni kiasi chama kimekosa washambuliaji. Wakati mwingine unajiuliza kuwa hivi hiki chama kina kocha kweli kwa maana ya mwenyekiti? Maana badala ya kuleta washambuliaji mahili analeta tena mbumbu wengine kama Juliana Shonza na Mwampamba. Lipi wamefanya toka wameingia CCM zaidi ya kuhubiri ukabila, ukini na ukanda kama wanavyoongozwa na Nape na Mwigulu.
Nawashauri CCM waangalie watu makini wa kusimama mstari wa mbele badala ya Mwigulu, Nape, Shonza na Mwampamba. Ukifuatilia maneno anayosema Mwigulu bungeni na kwenye mikutano ndipo utashangaa utakapoambiwa eti yeye ni first class economist! Wakati mwingine hata wale watoto wanaofaulu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika wana nafuu kuliko huyu. Nape ndio hakuna kitu kabisa!! Yeye anachojua mdomoni mwake ni CHADEMA, udini, ukabila na ukanda hajui lolote kuhusu sera za chama chake. mwisho wa siku mahubiri yake yatakiathiri chama chake kuliko wapinzani kama anavyofikiria. CCM mpeni Kinana watu makini sio hawa kina Nape, Mwigulu, Shonza na Mwampamba kwani nafasi hizo hawazimudu!