CCM na washambulaji mbumbu!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,304
12,965
Timu yoyote ya mpira makini huweka washambulliaji makini na wenye uwezo ili kuilete ushindi. Hata timu za mpira wa miguu ulaya hutumia gharama kubwa kununua washambuliaji wakali na mkini ili kupata ushindi. Mifano michache ni kama Real Madrid, Man United, Chelsea, PSG n.k. Katika siasa pia chama chochote makini huweka viongozi makini na wenye ushawishi mkubwa mstari wa mbele ili kunadi sera na kushawishi watu kukiamini na kukiunga mkono. Mara nyingi watu hawa huwa ni wenye busara sana, uelewa na ushawishi na ndio huwa mdomo wa chama.

Jambo la kushangaza CCM badala ya kuweka mstari wa mbele watu makini, waelewa, wenye ushawishi mkubwa na wenye busara kubwa, wameweka mambumbu watupu ambao kila wanapoongea hakuna la maana zaidi yakukiabisha chama na kukifanya chama kidharaulike. Angalia aina ya washambuliaji inao watumia akina Nape na Mwigulu. Hawa badala ya kufanya mashambulizi kwenye goli la wapinzani na kufunga magoli wanagfanya mashambulizi mengi kwenda upinzani halafu magoli wanafunga golini kwao. Ukisikiliza kauli za Nape na Mwigulu ndipo utajua ni kiasi chama kimekosa washambuliaji. Wakati mwingine unajiuliza kuwa hivi hiki chama kina kocha kweli kwa maana ya mwenyekiti? Maana badala ya kuleta washambuliaji mahili analeta tena mbumbu wengine kama Juliana Shonza na Mwampamba. Lipi wamefanya toka wameingia CCM zaidi ya kuhubiri ukabila, ukini na ukanda kama wanavyoongozwa na Nape na Mwigulu.

Nawashauri CCM waangalie watu makini wa kusimama mstari wa mbele badala ya Mwigulu, Nape, Shonza na Mwampamba. Ukifuatilia maneno anayosema Mwigulu bungeni na kwenye mikutano ndipo utashangaa utakapoambiwa eti yeye ni first class economist! Wakati mwingine hata wale watoto wanaofaulu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika wana nafuu kuliko huyu. Nape ndio hakuna kitu kabisa!! Yeye anachojua mdomoni mwake ni CHADEMA, udini, ukabila na ukanda hajui lolote kuhusu sera za chama chake. mwisho wa siku mahubiri yake yatakiathiri chama chake kuliko wapinzani kama anavyofikiria. CCM mpeni Kinana watu makini sio hawa kina Nape, Mwigulu, Shonza na Mwampamba kwani nafasi hizo hawazimudu!
 
Walikuwa wanasema wapinzani hawazungumzii sera zao ila wanasema na kuizungumzia ccm
Sasa na maccm sasa hali imekuwa mbaya, hawana wanchokizungumza ktk mikutano yao, yaani ni ndoa ya dr. Slaa na udini wa chadema,
Yaani wananchi wanashindwa kuelewa nini tofauti kati ya chama tawala na PPT~maendeleo
Hawana la maana wanalofanya wao ni kubeba watu na mafuso na malori kisha kupost Facebook kwamba mikutano yao inajaa,
Wangoje kunyolewa 2015
 
halafu haya majamaa yanarudia mambo yale yale miaka nenda rudi...sionagi wakisema kitu kipya...hata tuhuma wanazotunga ni zile zile miaka nenda rudi...
 
Timu yoyote ya mpira makini huweka washambulliaji makini na wenye uwezo ili kuilete ushindi. Hata timu za mpira wa miguu ulaya hutumia gharama kubwa kununua washambuliaji wakali na mkini ili kupata ushindi. Mifano michache ni kama Real Madrid, Man United, Chelsea, PSG n.k. Katika siasa pia chama chochote makini huweka viongozi makini na wenye ushawishi mkubwa mstari wa mbele ili kunadi sera na kushawishi watu kukiamini na kukiunga mkono. Mara nyingi watu hawa huwa ni wenye busara sana, uelewa na ushawishi na ndio huwa mdomo wa chama.

Jambo la kushangaza CCM badala ya kuweka mstari wa mbele watu makini, waelewa, wenye ushawishi mkubwa na wenye busara kubwa, wameweka mambumbu watupu ambao kila wanapoongea hakuna la maana zaidi yakukiabisha chama na kukifanya chama kidharaulike. Angalia aina ya washambuliaji inao watumia akina Nape na Mwigulu. Hawa badala ya kufanya mashambulizi kwenye goli la wapinzani na kufunga magoli wanagfanya mashambulizi mengi kwenda upinzani halafu magoli wanafunga golini kwao. Ukisikiliza kauli za Nape na Mwigulu ndipo utajua ni kiasi chama kimekosa washambuliaji. Wakati mwingine unajiuliza kuwa hivi hiki chama kina kocha kweli kwa maana ya mwenyekiti? Maana badala ya kuleta washambuliaji mahili analeta tena mbumbu wengine kama Juliana Shonza na Mwampamba. Lipi wamefanya toka wameingia CCM zaidi ya kuhubiri ukabila, ukini na ukanda kama wanavyoongozwa na Nape na Mwigulu.

Nawashauri CCM waangalie watu makini wa kusimama mstari wa mbele badala ya Mwigulu, Nape, Shonza na Mwampamba. Ukifuatilia maneno anayosema Mwigulu bungeni na kwenye mikutano ndipo utashangaa utakapoambiwa eti yeye ni first class economist! Wakati mwingine hata wale watoto wanaofaulu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika wana nafuu kuliko huyu. Nape ndio hakuna kitu kabisa!! Yeye anachojua mdomoni mwake ni CHADEMA, udini, ukabila na ukanda hajui lolote kuhusu sera za chama chake. mwisho wa siku mahubiri yake yatakiathiri chama chake kuliko wapinzani kama anavyofikiria. CCM mpeni Kinana watu makini sio hawa kina Nape, Mwigulu, Shonza na Mwampamba kwani nafasi hizo hawazimudu!
Uongozi ni vitendo siyo maneno mkuu, hayo unayoyasema yako sana CHADEMA na kiuhalisia wanaonekana kabisa ni wanafiki, ushabiki wa shule ndogo kichwani na kujipendekza kwa wakubwa zao.
 
Vitendo gani unavyozunguzia?Vya kifisadi,kijangili au vp?Na wewe mwenye kauli za kuwadanganya Wtz waipende ccm wakati wameichoka si kujipendekeza kwa wakubwa zako?Na inaonyesha wakikuomba 0713 a.k.a tigo hutakosa kuwapa kwa roho safi.Njaa zitawaua nyie pu..m.b.aaaaav..u!
 
Mkuu ili upate washambuliaji wazuri hasa hawa wa kulipwa lazima utenge fedha ya kutosha. Sasa ndugu yangu unadhani kwa buku 7 per day nani mtu makini atajiunga na timu yako? Lazima utawapata mbumbumbu ambao wakati mwingine hawajui hata formation wanayotumia kuwa ikileta counter attack ni goli kwa upande wao.
Wangekuwa wakweli wangepata wachezaji wa kujitolea walio makini ila ili hilo lifanikiwe lazima Kapteni awe mwadilifu sio kama hao makapteni wao Nape na Mwigulu
 
Mambumbu,machizi ,mazuzu , MACCM sasa wananchi wakiulizwa CCM ni dini gani utasikia mashetani
 
CHADEMA ni kichaka cha majambazi.
Kama Nape. Wewe ndiyo umeshika dola halafu unasema fulani ni jambazi kwanini usimkamate ili sheria ichukue mkondo wake. Hapa ni kufanya shambulizi na kujifunga goki mwenyewe.
 
Back
Top Bottom