CCM na vyama vingine vyapanga kwenda Mahakamani kupinga matokeo ya uchauzi mdogo Pandani, Pemba

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
WAGOMBEA saba vya vyama vya Siasa walioshiriki kwenye uchaguzi mdogo nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Pandani Kisiwani Pemba wamekusudia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wakidai kwamba taratibu na kununi za Tume ya uchaguzi hazikuzingatiwa.

Wagombea hao ni kutoka chama Cha ADC, AFP, CCM, CUF,Demokrasia Makini, UPDP pamoja na Chama Cha NRA.

Wakizungumza na wandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Jamuhuri , wagombea hao wamesema watakwenda mahakamani kudai uchaguzi urudiwe kwani tume imekiuka kanuni na taratibu wakati wa kutangaza matokeo.

Wamesema moja ya kasoro ni msimamizi wa Uchaguzi kushindwa kutangaza Idadi ya kura zilizopigwa,zilizoharibika na halali jambo ambalo linawapa mashaka kwamba mshindi aliandaliwa.

Naibu Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi wa Chama cha Wananchi –CUF-Vuai Makame amesema endapo Tume itashindwa kuchukua hatua itahiki watakwenda mahakamani kudai haki.

Katika uchaguzi huo ,Mgombea wa Chama Cha ACT Wazalendo Pro Omar Faaki Hamad alitangazwa kuwa mshindi , hata hivyo amekiri kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.
 
VIDEO:

Hao wote ni familia ya ccm sasa hapo ugomvi unatokea wapi?
 
Back
Top Bottom