CCM na vilabu mmetuangusha sana wapenda soka

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,188
8,215
Kama tunavyofahmu asilimia 80 ya viwanja vinavyotumuka kwa ligi kuu Tanzania VPL ni mali ya CCM baada ya kuvibinafsisha toka kwa umma mara baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini.

SINA TATIZO HILO
TUachane na vyoo au segemu za majukwaa tuko tayari kusimama lakini hivi ni kweli CCM mmeshindwa kuajiri angalau watu wawili wa kumwagilia uwanja ili uwe kwenye mazingira bora?

Mimi ninavyofahamu jinsi kazi zilivyo ngumu hata mshahara wa laki moja kwa mtu mmoja ungetosha kuwalipa wamwagiliaji au mapato ya kila mwisho wa wiki hayatoshi?

Nanyi vilabu pia mmeshindwa kufikiria makubaliano yoyote na Hawa jamaa wa kijani ili kutunza viwanja kama CCM wameshindwa kuajiri watu, nanyi mmeshindwa kuajiri watu ambao mngewapa hata posho baada ya kila mechi kama hamuwezi kuwalipa mshahara au mapato yote mnakula?

BADILIKENI BWANA MNASHINDWA HATA NA KINA GYMKHANA, VIWANJA VYAO NCHI NZIMA KIJANI TU KAJIFUNZENI KWAO BASI
 
Miaka yote ni hivi viwanja vinachezewa mechi wala havijawai kuonekana ni vibovu. Sasa ni jukumu la TFF kupeleka taarifa kwa wamiliki wa viwanja namna gani inatakiwa viwanja viwe.

wamiliki wa viwanja watafauata maelekezo ya TFF na vitarekebishwa.
 
Tff hilo si jukumu lao hilo ni jukumu la klabu na wamiliki klabu ndie anaepeleka taarifa tff kwamba nitachezea uwanja fulani baada ya makubaliano na wamiliki

Nimependa inachofanya bodi ya ligi hivi sasa kiwanja kibovu weka rungu ni afadhali ligi ichezwe kwe viwanja vitano au 6 vyenye afadhali
 
Taasisi iliyoshindwa kuhudumia viwanja vyao vya mpira inyang'anywe na ipewe taasisi yenye uwezo wa kuvihudumia na kuviendeleza. Sisi wapenda soka tumechoka na hili suala la viwanja vibovu.
Kura yangu itakwenda kwa mgombea atakae ahidi kulishughulikia tatizo hili sugu ambalo lina interest ya wa-Tanzania wengi wakiwemo wachezaji na watazamaji.
 
Kama tunavyofahmu asilimia 80 ya viwanja vinavyotumuka kwa ligi kuu Tanzania VPL ni mali ya CCM baada ya kuvibinafsisha toka kwa umma mara baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini.

SINA TATIZO HILO
TUachane na vyoo au segemu za majukwaa tuko tayari kusimama lakini hivi ni kweli CCM mmeshindwa kuajiri angalau watu wawili wa kumwagilia uwanja ili uwe kwenye mazingira bora?

Mimi ninavyofahamu jinsi kazi zilivyo ngumu hata mshahara wa laki moja kwa mtu mmoja ungetosha kuwalipa wamwagiliaji au mapato ya kila mwisho wa wiki hayatoshi?

Nanyi vilabu pia mmeshindwa kufikiria makubaliano yoyote na Hawa jamaa wa kijani ili kutunza viwanja kama CCM wameshindwa kuajiri watu, nanyi mmeshindwa kuajiri watu ambao mngewapa hata posho baada ya kila mechi kama hamuwezi kuwalipa mshahara au mapato yote mnakula?

BADILIKENI BWANA MNASHINDWA HATA NA KINA GYMKHANA, VIWANJA VYAO NCHI NZIMA KIJANI TU KAJIFUNZENI KWAO BASI
Mwizi kazi yake ni kuiba tu siyo kuboresha. CCM wameiba viwanja vya umma. Kuboresha haiwahusu. Wao ni wezi na wanaujua wizi. Sasa wanaiba mali za umma kumfanyia kampeni Magufuli kwenye uchaguzi. Wanabomoa hazina. Mtoto wa Dada kazi yake ni kulipa tu. Uharibifu, wizi ni kila mahali. CCM rudisheni viwanja kwa Halmashauri husika. Ni Mali ya wananchi. Acheni wizi. Tumechoka.
 
Vipi ile Sera ya kunyang'anywa sehemu uliyoshindwa kuiendeleza ikitumika kuwanyang'anya hivi viwanja hawa CCM na kuzipa harmashauri kuviboresha Nina imani tutakuwa na viwanja bora nchini.

Maana hawa wana siasa hawawezi kuvitunza na kuviboresha wao wanaangalia kupata fedha ya kuwahonga wapigakura kupitia viwanja hivyo serikali ilitupie macho suala hili kwa maslahi ya maendeleo ya soccer letu.

Viwanja bora ni kigezo kimojawapo cha kupewa ticket ya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa sasa kwa viwanja vyetu hivi hatutaweza kuandaa mashindano ya CAF.
 
Back
Top Bottom