Mbona wanaoshangilia Viti Maalum vya CHADEMA ni CCM?

Ashasembeko

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
225
910
Nimekua nikijiuliza, hivi kwanini CCM wanashangilia sana kuapa kwa wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA kuliko hata wanaCHADEMA wenyewe?

Jibu lililowazi ni kuwa Uchaguzi wa October umefanya viongozi wateule kukosa uhalali wa uongozi ndani na nje ya nchi (haswa nchi za magharibi). Hili sio tatizo maana tunajua Jiwe hajali kuhusu uhalali wowote, angekua anajali, asingefanya aliyofanya kwenye uchaguzi.

Sababu nyengine yaweza kuwa CCM wamegundua kukaa peke yao bungeni wangeishia kulumabana wao kwa wao. Pia wasingeweza kuwaonyooshea vidole wapinzani kuwa ndo wanakwamisha maendeleo, wakati bunge lote lilikua lao.

Lakini sababu kuu, na yenye msingi ni fedha. Kabla ya hawa wabunge 19 wa CHADEMA, bunge lilikua na wabunge wawili wa kuteuliwa walioapa. Mfumo wa Bunge unahitaji uongozi wa upinzani kwenye baadhi ya kamati kama PAC kwa ajili ya oversight. Wafadhili wasingetoa pesa zao kwenye bunge lisilokuwa na mfumo wa kuchunguza pesa zao zinatumika vipi. Hata hivyo, uteuzi wa wabunge wa Africa Mashariki na Umoja wa Africa unahitaji baadhi ya wabunge watoke upinzani. Hapa pia walikwama.

Yaaani Bunge ilibidi libadilishe kanuni zake ili liweze endesha shuguli zake. Walikua wanawahitaji sana hao wabunge wa CHADEMA ili bunge liweze kuendeswa bila kubadili kanuni na ndio maana nguvu kubwa sana imetumika kuwaconvince kina Mdee.

Hata hivyo, sio siri kuwa nchi yetu kwa sasa inapitia msukomsuko mkubwa wa kidiplomasia. Hawa Viti Maalum wamempa Kabudi "utetezi" akienda kwa wafadhili na vyombo vya habari vya kimataifa. Kila wakimuuliza kama uchaguzi ulikua huru na haki atawajibu kuwa "hao waliosema haukua huru mbona wamepeleka wabunge wa viti maalumu kwa idadi ya kura za uchaguzi huu?"

Kwa namna moja ni habari njema kwa Magufuli, ila bado wanasafari ndefu sana. Kuna plenty of evidence ambazo tayari zimewasilishwa ICC na mabalozi kuhusu mwenendo wa uchaguzi. Bado itawawia vigumu sana kujitetea.

Chazo changu kinachofanya kazi kwenye moja ya hizi balozi kimeniambia kuwa traditional development partners wote, ambao ndio wanamchango mkubwa kwenye bajeti (UK,USA, EU, Cannada, South Korea, Japan na Nordic countries zote) wamekubaliana "informally" kuhusu namna watakavyojihusisha na serikali hii.

Amenihakikishia kuwa kutakua na focus kubwa sana ya kutoa financial support kwa Non government actors (NGOs, CSOs, Activists). Na misaada yao kwenye bajeti ya nchi itapungua mno in fact miradi itakayoendelea ni ile ambayo ipo kwenye utekelezaji, Ila hakuna miradi mipya itakayofadhiliwa na wao. Hii ni changamoto kwa serikali.

Uzuri ni kuwa serikali wataendelea pata support ya Benki ya Dunia na African Development Bank ambazo policies zao zinawakataza kujihisisha na kuingilia mambo ya kisiasa. Japo nchi kama Marekani inaweza tumia nguvu yake katika taasisi hizi kuzuia mikopo. Jua kwamba Marekani na UK ni wanahisani wakubwa zaidi Beni ya Dunia na Africa Development Bank.

Wanaweza wakatumia hiki kigezo washawishi bodi wasipitishe miradi, kama walivyofanya Januari mwaka huu kwenye ule mradi wa elimu wa sekondari (SEQUIP). Hata hivyo Benki ya Dunia haitotoa misaada ya policy support kama wanavyofanyaga.

Huko Zanzibar ndio kabisa, uchumi uko vibaya, na Mwinyi anahangaika sana kuhakikisha Maalim anaingia kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa ili apate uhalali.

Nawaonea huruma sana wafanyabiashara maana wao ndio watakandamizwa sana. Serikali itahitaji kodi zenu kuliko wakati mwengine wowote ule.
 
Vile MATAGA yamefurahia leo!
24577890.jpg
 
Hivi ITIKADI ya CHADEMA ni ipi?!!

Mbona wao si LEFTIST...si WAJAMAA..si WAKOMUNISTI...

Lakini kutwaa kuvaa MATURUBAI...
Lakini kutwaa kuvaa BERETI NYEKUNDU na MIBUTI MAGOTINI kama ile ya EFF...Kama ile ya akina HUGO CHAVEZ...

Eti Boniphace Jacob unasemaje JUU YA HAYA?!!!
 
Serikali iwape ulinzi makini viti maalum wa Chadema. Makamanda wenye hasira wasije wakawadhuru wabunge wetu makini.
 
Moja ya jambo kubwa la kufikiri,

Yawezekana chadema wamekubaliana kisiri na hao wanawake ili waonekane wamesaliti ili wasikose ruzuku lakini pia wakati huo huo process za ICC zikiendelea ili wasijekosa sehemu zote.

Kumbuka game ya lisu na membe kuachiana nafasi strategic.
 
Moja ya jambo kubwa la kufikiri
Yawezekana chadema wamekubaliana kisiri na hao wanawake ili waonekane wamesaliti ili wasikose ruzuku lakini pia wakati huo huo process za ICC zikiendelea ili wasijekosa sehemu zote
Kumbuka game ya lisu na membe kuachiana nafasi strategic.
Uko sahihi kabisa. Maana hata matamko yao yamekaa kiajabu ajabu
 
WanaCCM wanafurahia kwa sababu hizi:Hizo zako ni kujifariji tu)

1-Hii issue wanategemea mtagawanyika na kufukuzana.(kutokana na desturi yenu)

2-Mmezidi kuwathibitishia wapiga kura kwamba hakuna mnachokisimamia.

3-Mmejionesha kwa wapiga kura kwamba njaa kali,hakuna cha ukombozi wala nini bali matumbo tu. (Subiri propaganda zitakazofuata)

4-Kwa kupeleka wabunge mmetambua uhalali wa matokeo hivyo uchaguzi ulikuwa wa haki.(Huu ulikuwa msingi wa hoja yenu ya kususia)

5-Mmeitangazia dunia kwamba CDM ni genge la wahuni tu na si taasis imara kiasi kwamba kila mtu anajiamulia tu hata kwa kukiuka misimamo ya chama. (Jana M/Mwenyekiti na leo K/Mkuu wamedai hawata(ja)peleka majina)

Hayo yote yana manufaa makubwa kwa CCM.
 
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje CCM ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani CCM ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini CCM hawana hata chembe ya aibu.

Watanzania amkeni, hawa CCM hawana utu hata chembe, tafuteni dawa nyingine ya kudeal nao tofauti na hii ya sanduku la kura. Haishangazi waliingiza kura fake na bila aibu wakajitangaza wameshinda kwa kishindo.
 
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje ccm ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani ccm ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini ccm hawana hata chembe ya aibu..
Wao wanafuata mdundo wa ngoma toka kwa meko,ccm ilishakufa zamani imebaki kutumia pesa,police,tiss ili ibaki madarakani
 
Back
Top Bottom