Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm na upotou juu ya kuvunjika kwa muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Intellect, Mar 24, 2012.

 1. Intellect

  Intellect Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Chama Cha Mapinduzi CCM kimekua kikijishushia heshima kutokana na tabia yake ya kuweka maslahi ya chama mbele hata pale yanapo kinzana na maslahi ya taifa. Hii inajidhihirisha pale wanapotumia uwingi wao bungeni kupinga hoja zote zilizo kinyume na matakwa ya chama hata kama ni za manufaa kwa mwanachi. Katika muendelezo wa tabia hii chafu, chama hiki kimekua kikiutetea muungano unaoonekana kuwa mradi binafsi "private project" wa chama hiki tawala pamoja na kuwa na kero lukuki kwa wananchi hususan wa Zanzibar.

  Sasa kutokana na ari ya wananchi kutaka kizifikisha tamati sera za kizandiki za CCM, inayokua sikuhadi siku siku inawalazimu viongozi wa chama hiki kusambaza taarifa potofu juu ya hatma ya wananchi wa pande moja ya muungano walio hamia pande nyingine iwe kibiashara, makazi, nk. Viongozi hawa wamekua wakikaririwa wakisema kuwa eti wananchi wengi wa bara wameji-establish unguja "and vice versa", wengine wamezaliana hivyo muungano ukivunjika itakua tabu kwa watu hawa!

  Hawataki kuzungumzia tatizo halisi ambalo ni muungano wa kisiasa na kiuchumi. Ninacho taka kusema ni kwamba muungano wa kijamii sio kitu kinaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya kisheria, wahindi wangapi wapo wamelowea hapa nchini ilhali tanzania haina muungano na India, halikadhalika waarabu pamoja na wachina wanaozidi kumiminika, tujiulize watanzania wangapi wamelowea nchi za ulaya na hutuna muungano na nchi hizo! Baada ya kuvunjika Sudan wananchi walipewa fursa ya kuchagua aidha South Sudan au North na maisha yanaendelea.


  Muungano huu usio na faida (wa iuchumi na kisiasa) ukivunjika wanachi walio upande wa pili wa muungano watapewa fursa ya aidha kuchagua kubaki au kurudi upande wao wa asili. Maisha yataendelea kama kawaida isitoshe kero zilizopo ni sawa tu na nchi mbili tofauti! Watu wamechoshwa na vitendo kama vya TRA kutoza kodi bidhaa Across pande mbili za muungano, ushirikishwaji mdogo wa wananchi wa Zanzibar ktk maswala ya muungano, the list is endless!

  Ni hayo tu!
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,177
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  serikali tatu ndio suluhisho

  Serikali ya Tanganyika yenye makao makuu Dodoma

  Serikali ya Zanzibar yenye makao makuu Unguja

  Serikalu ya ndogo ya JMT yenye makuu Dar es Salaam.

  Kelele zote zitaisha
   
 3. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280


  Serikali tatu kwa faida ya nani? Kwa nini tusivunje muungano wenyewe? Una faida gani kwa bara au visiwani? Huu ulikuwa muungano wa Karume na Nyerer,sasa wote wamekufa, ni vyema na muungano wao ukawafuata.
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,177
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muungano hautavunjika huo ni national pride; muundo utabadilishwa period..kwa faida ya taifa na wananchi wake..
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,597
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NITAFURAHI SANA TUKIWA NA SERIKALI 1, KULIKO MUUNGANO UVUNJIKE ALAFU MAGAIDO WAJAE ZNZ BORA IJE VITA! Hivi kwa nini Nyerere hakuunganisha ikawa nchi 1?
   
 6. F

  Falconer JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Re: Ccm na upotou juu ya kuvunjika kwa muungano
  NITAFURAHI SANA TUKIWA NA SERIKALI 1, KULIKO MUUNGANO UVUNJIKE ALAFU MAGAIDO WAJAE ZNZ BORA IJE VITA! Hivi kwa nini Nyerere hakuunganisha ikawa nchi 1?


  Hahahahah ndoto hii ilimshinda babenu Julius K. Nyerere. Pale ilikuwa rahisi kuuwa Zanzibar, leo wenzenu wameamka.hahhahaahah
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  na hakuna kiongozi atakayeruhusu muungano umfie.
   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 2,964
  Likes Received: 1,144
  Trophy Points: 280

  Hakuna national pride kwenye huu muungano wa wafu. Wenyewe wameshakufa sharti na muungano wao ufe. period
   
 9. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Comrade punguza jazba kidogo ndg yng kuungana ni jambo jema kabisa na kuungana si kutokutofautiana tofauti za mapishano lazima ziwepo kusolve hizo tofauti ndio ukomavu wa Muungano.
  Serikali 3 yaweza kuwa sulruhisho
   
 10. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazanzibar hawataki muungano na makongamano/semina/warsha zinaendelea kwa fujo visiwani, nyie endeleeni na upinzani wenu feki watawasuprise mwaka huu.
   
Loading...